Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,406
- 31,387
- Thread starter
- #81
CONFLICT OF INTEREST (COI) YAANI MGONGANO WA MASILAHI
Mgongano wa masilahi ni mwingiliano wa masilahi ya mtu/taasisi/shirika yawezayo kukwaza utashi au matakwa katika kutekeleza majukumu
Tumeona jinsi mgongano wa masilahi ulivyoleta kizaa zaa bungeni. Matatizo yanajengwa na mgongano wa masilahi (COI)
Kwa mfano huo, bunge la 11 limeanza vibaya sana, hata kupelekea Spika/Serikali kujichanganya
MASHIRIKA YACHANGIA HAFLA YA BUNGE
Hafla ya bunge imetokana na michango nje ya pesa za bunge au serikali. Pengine ni ya makampuni, mashirika n.k.
Hilo lilisemwa kwa kuzingatia ukweli kuwa milioni takribani 250 ni nyingi kutoka bajeti ya umma
Yangekuwepo malalamiko juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma
Rais aliamua sehemu kubwa ipelekwe hospitali ya Muhimbili kununua vitanda
Mchana kabla, Rais lihutubia bunge na kutilia mkazo suala la kupambana na rushwa
Alisema kazi hiyo ni ngumu kwasababu ina watu wazito na kuliomba taifa limuombee afanikiwe
SIKU ZA NYUMA
Wabunge kadhaa walituhumiwa kwa kuwa na mgongano wa masilahi.
Wengine wakisemwa kuchukua posho kutoka serikali na kule kwenye mashirika wanakofanya kazi zinazohusu bunge
Iliwahi kupendekezwa wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za taasisi au mashirika ili kukwepa mgongano wa masilahi
INASHANGAZA
Kuwa bunge linalosubiri miswada mbali mbali ya kupambana na rushwa, limeingia katika mgongano wa masilahi
Inawezejanaje chombo cha umma kinachotunga sheria na kusimamia serikali kupokea pesa za nje?
Bunge litawezaje kuwa huru ikiwa tayari linapokea 'misaada' nje ya utaratibu unaolizewesha kuwa huru bila (COI)?
Lakini pia pesa hizo hazikupaswa kuelekezwa katika matumizi ya umma.
Haina maana kuwa pesa hizo ni haramu, la hasha! bali zinaleta mgongano wa masilahi
Tumeona matatizo yaliyopo yanayotokana na migongano ya masilahi, je tunahitaji somo zaidi?
Haya yanatokea kwasababu hakuna umakini katika kusimamia sheria, kanuni, maadili na taratibu zetu
Tunaweza kuishi kwa kupinda pinda tu mambo, bora liende
Tusipobadilika, hatutafanikiwa. Tunaona matatizo hatujifunzi, tunarudia mako
Tusemezane