mbwigule
JF-Expert Member
- Jan 21, 2012
- 235
- 103
Kweli kabisa. Uhuru wa mmoja huishia unapoanzia wa mwenzake. Mitandao ni chombo bora na muhimu kabisa katika kuijenga jamii na kukosoa masuala yanayoenda arijojo, lakini si lazima watu kutumia lugha chafu ili kuwasilisha jumbe mbalimbali. Binafsi siipendi kabisa CCM na hata JK mwenyewe lakini namheshimu kama Rais aliye madarakani na naamini anapokosolewa hufanyika hivyo kwa maslahi ya nchi zaidi kuliko binafsi. Hivi karibuni nilichangia thread moja iliyokuwa ikimsifu kwa kutumia busara kufanya uamuzi wa kuurejesha muswaada wa mabadiliko ya Katiba Bungeni na nilisema waziwazi kwamba mara nyingi Kikwete anapotoshwa na wapambe wanaomzunguuka na ambao hufanya hivyo kwa maslahi yao zaidi kuliko ya taifa. Mimi naamini mtandao kama wa JF ni chombo chenye faida pande zote mbili yaani kwa serikali inayotuongoza kupima mwonekano wake kwa umma na kwetu tunaoongozwa kujadili na kutoa mapendekezo na hata kupumua hasira zetu; lakini bado nasisitiza bila kutumia lugha za matusi. Ni kwa mantiki hii naungana kikamilifu na Mhariri wa Tanzania Daima kuwasihi wanamitandao ya jamii kuepuka lugha za matusi dhidi ya kiongozi wetu mkuu licha ya mapungufu yake.Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.
Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-
1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.
Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.
Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.
Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012