Mitandao isitumike kumchafua Rais

amkane basi kwamba yule sio mwanae ili ajitenge na 'uchafu' ............kama mwanae kupata Div 4 ni uchafu.

mwanaume mzima kuhongwa nguo unakuwa ushajichafua kabisa mbele ya wanaume wenzako, hata mbele ya wanawake wa maana.
 
sikubali wala kukataa kinachojadiliwa, ila najaribu tu kuwaza,

Kama Mwanaasha Jakaya Kikwete angepata Division 1 na au angeongoza katika kumi bora ingekuwaje?

Maana lazima watu tungemsifu kuwa mtoto wa raisi kapasua kwenye mitihani yake, je, mngelalamika pia kwamba tuna'mkashifu' mtoto wa raisi?

At the end of the day as long yeye ni raisi hakuna cha maisha binafsi, tutamjadili kwa jema au baya, awe tayari kukubali tu.

Tena tunamjadili papendikulali kuliko HASHEEM THABEET........kwa kuwa Rais anatumia pesa yetu katika umaarufu wake
 
Kama unadhani hahusiki na matokeo ya mtoto wake, nani aliyekuwa akimsomesha? Hujui kuwa watoto na wake za viongozi huheshimiwa kwa sababu ya viongozi wenyewe? Imetokea hata wakuu wa wilaya husoma taarifa za wilaya zao mbele ya mke wa rais. Hivyo utendaji mbovu wa rais au hata wa mke na/au watoto wake unahusihusishwa na viongozi kwa jinsi wao wanavyojihusisha na masuala ya wazazi au waume/wake zao.

Ni sawa kwa hoja zako si sawa kutukana, mafano Jk kichwa cha panzi kwa sababu ya matokeo hayo.
 
si lazimiki kukisoma tanzania daima.........hoja hii ya huyu mtoto imejadiliwa kirefu hapa labda hukusoma.......ni kuwa mtoto kama huyu mwenye kuishi katika mazingira bora pengine kuliko watoto wote wa tanzania hii kwanini anashindwa kupita mitihani yake?

Hapo kwenye red Safari_ni_Safari sijui kama umetumia kiswahili vizuri.... nilifuatilia sana na kuchangia hoja unayoisema, lakini ni watoto wangapi wa wakubwa na wenye fedha wanafeli mitihani huku wakiishi katika mazingira bora na shule wanazosoma ni nzuri? Unataka kuniambia mwanaasha ndiyo wa kwanza? Na pengine tu unieleze, kufeli kwa huyu binti kuna uhusiano gani na urais wa baba yake?
 
amkane basi kwamba yule sio mwanae ili ajitenge na 'uchafu' ............kama mwanae kupata Div 4 ni uchafu.

mwanaume mzima kuhongwa nguo unakuwa ushajichafua kabisa mbele ya wanaume wenzako, hata mbele ya wanawake wa maana.

wewe ulipata Div. ngapi?
 
Hapo kwenye red Safari_ni_Safari sijui kama umetumia kiswahili vizuri.... nilifuatilia sana na kuchangia hoja unayoisema, lakini ni watoto wangapi wa wakubwa na wenye fedha wanafeli mitihani huku wakiishi katika mazingira bora na shule wanazosoma ni nzuri? Unataka kuniambia mwanaasha ndiyo wa kwanza? Na pengine tu unieleze, kufeli kwa huyu binti kuna uhusiano gani na urais wa baba yake?

Never mind Kiswahili changu...........Mtoto wa Magufuli(a real PhD holder) amefeli na amejadiliwa pia na hakuna lalamiko lolote lile......uhusiano wa mtoto na baba sidhani kama katika umri ulonao nahitaji kukuelewesha......
 
Tena tunamjadili papendikulali kuliko HASHEEM THABEET........kwa kuwa Rais anatumia pesa yetu katika umaarufu wake

Rais ni madaraka kama yalivyo madaraka mengine na matumizi ya fedha yenu si kwa yeye tu.... hata wewe kama ni muajiriwa wa serikali kwa nafasi yako ndogo unapata umaarufu kwa kutumia pesa yetu pia.
 
si lazimiki kukisoma tanzania daima.........hoja hii ya huyu mtoto imejadiliwa kirefu hapa labda hukusoma.......ni kuwa mtoto kama huyu mwenye kuishi katika mazingira bora pengine kuliko watoto wote wa tanzania hii kwanini anashindwa kupita mitihani yake?

mkuu wangu naamini unaelewa kwamba licha ya mazingira bora ya kuishi na shule nzuri siyo waranti ya mtoto kufaulu mtihani. tushukuru kwamba baba yake hakutumia wadhifa wake kuiba mtihani ama kulazimisha apandishwe daraja la juu. inawezekana huyo mtoto ana kipaji cha jambo jingine ambacho kikitumika vizuri atakua msaada kwa familia yake na taifa. kufeli mitihani siyo kushindwa maisha!
 
Kuna album ya snoop doggy inaitwa "Da cost to be da boss"

Kwahyo issue ya mwanaasha kuwa wa mwisho feza girlz nzima ni kumchafua? Watu wanajadili iweje mtoto kama huyo home anafacilities zote na shule facilities zote lkn kafeli hauni ni kitu cha ajabu? Haiwezi kua story hiyo?
 
Rais anahusika vipi na matokeo ya mtoto wake? uzumbukuku huu.

Rais ndio kiongozi mkuu wa taifa hili i mean he is above us alll.. tunategemea awe role model wetu sote ili tuige kutoka kwake ndio maana tunaingia gharama za kumweka pale magogoni yeye pamoja na familia yake..(the first family), kwa mantiki hiyo mwanae pia automatically anatakiwa kua kioo cha jamiii, sasa kama first daughter anakua wa mwisho darasani tena kwenye matokeo ya mtihani wa kitaifa mnataka tukae kimya?:smash:

Rais and the whole first family wanatakiwa wawe mfano kwetu.. wakiboronga lazima tuseme
 
Rais ni madaraka kama yalivyo madaraka mengine na matumizi ya fedha yenu si kwa yeye tu.... hata wewe kama ni muajiriwa wa serikali kwa nafasi yako ndogo unapata umaarufu kwa kutumia pesa yetu pia.

Nani kakwambia mimi ni muajiriwa serikalini? Unadhan madaraka ya Rais ni sawa na ya mwalimu?
 
Mitandao isitumike kumchafua Rais

Tanzania Daima. 15 Feb, 2012

HIVI karibuni, Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo ya kidato cha nne yaliyofanyika nchini mwaka 2011.

Na miongoni mwa wahitimu waliofanya mtihani huo ni mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, aliyemaliza katika moja ya shule za sekondari jijini Dar es Salaam.

Kwa bahati mbaya sana, matokeo ya mtoto huyo hayakuwa mazuri licha ya shule yake kufanya vizuri kitaifa katika mitihani hiyo na kuwa moja ya shule kumi bora.

Hoja yetu si kurejea matokeo hayo, bali tungependa kukemea matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii hasa wakati wa kujadili masuala kadhaa na hata mengine ambayo kimsingi ni ya kibinafsi lakini yanahusishwa moja kwa moja na maslahi kwa umma.

Tunasema hivyo kutokana na baadhi ya wachangiaji kwenye mitandao hiyo, kuchukulia matokeo mabaya ya mtoto wa Rais kama suala la kitaifa lenye kuhusishwa na uongozi wa baba yake, na hivyo kumshambulia kiongozi huyo bila sababu ya msingi.

Kwanza, lazima tutambue kuwa kufanya vibaya katika mitihani ni jmabo la bahati mbaya ambalo kimsingi linamuumiza mtahiniwa na vile vile wazazi au walezi wake, lakini tunapaswa kuelewa kuwa mtoto wa Rais ameshindwa kama walivyoshindwa wanafunzi wengine pasipo kujali amesoma shule gani au mzazi ana wadhifa gani.

Pili, tunapaswa kulichukulia jambo hili kama funzo na changamoto kwa elimu yetu, kwani ni watoto wachache sana wa viongozi wetu wakuu wanasoma shule za hapa Tanzania, na kwa ubabaishaji uliyopo kwenye usimamizi wa mitihani bado Rais angeweza kutumia nguvu yake kuhakikisha mwanaye anapendelewa lakini haikuwa hivyo.

Ni vyema wakati wa kujadili na kuchangia maoni hasa kuwahusu watawala wetu, tukazingatia majukumu na wajibu wa msingi tunaowapa viongozi ili watekeleze, na hivyo tunapaswa kuwahukumu kwa kuzingatia mipaka hiyo si kuingilia hata mambo yao binafsi na familia zao.

Mtoto wa Rais kushindwa mtihani si jambo la kutufanya tumtukane baba yake, yeye si malaika kwani huo ndiyo uwezo aliopewa na Mungu na walimu wake wakaongezea ujuzi wao.

Kama hoja ni kwamba kila anayeshindwa mtihani wazazi wake wasakamwe kwa matusi, basi hebu tuwatazame kwanza wa kwetu.

Tunaamini umefika wakati kwa wale wamiliki wa mitandao hiyo kuwa makini na hoja zinazoletwa hewani kujadiliwa na kujifanyia uhakiki kabla ya kuzichapisha, vnginevyo tutajikuta tumegeuka taifa linalovunja haki za msingi za binadamu kwa kuingilia masuala binafsi ya watu wengine.

Kama hoja ni kufeli kwa mtoto wa Rais, basi kafeli kama wale wa kwetu ambao tunawasomesha kwenye shule duni au zile za mamilioni lakini mwisho wa siku hawafaulu, sasa iweje tumwandame kiongozi wetu kwa suala lisilohusiana na kazi tuliyompa?

Tundhani kwa hili Rais alipaswa kusifiwa kuwa si mbinafsi kwa kuwa hakumpeleka mtoto wake kusoma Ulaya kama ambavyo viongozi wengi wa nchi hii wafanyavyo hata kwa watoto wao wasiokuwa na uwezo kimasomo.
 
Never mind Kiswahili changu...........Mtoto wa Magufuli(a real PhD holder) amefeli na amejadiliwa pia na hakuna lalamiko lolote lile......uhusiano wa mtoto na baba sidhani kama katika umri ulonao nahitaji kukuelewesha......

Nilicho hoji si uhusiano wa baba na mtoto, nimekuuliza kufeli kwa huyu binti kuna uhusiano gani na Urais wa baba yake?
 
Na yeye rais asitumie nafasi yake kutukejeli na kutuibia wananchi,rejea mazungumzo yake ya wazee wa dar yote miwili pia angalia riz1 na yeye wanavyojitajirisha
 
mkuu wangu naamini unaelewa kwamba licha ya mazingira bora ya kuishi na shule nzuri siyo waranti ya mtoto kufaulu mtihani. tushukuru kwamba baba yake hakutumia wadhifa wake kuiba mtihani ama kulazimisha apandishwe daraja la juu. inawezekana huyo mtoto ana kipaji cha jambo jingine ambacho kikitumika vizuri atakua msaada kwa familia yake na taifa. kufeli mitihani siyo kushindwa maisha!

Utetezi wako ni mzuri tu........niambie kwa high standards za FEZA GIRLS huyu alifikaje Form IV?.....una hakika gani baba yake hakujaribu kuratibu majibu yake wakati anadaiwa kuratibu kura za watanzania 2010?.....na ni nani kasema kufeli kwake mtihani ndio kafeli maisha?
 
Hivi mtu msafi atachafuliwa??? mimi sikubaliani na mtoa hoja pamoja na mhariri wa tanzania daima hiyo ni mitazamo yao. Kiukweli msafi atasifiwa na mchafu ataambiwa ukweli ili ajirekebishe na ujumbe utafikishwa kwa namna tofauti. Bado hatujafikia hatua ya kuwarushia mayai mabovu, utasemaje??. Pia ni fundisho kwa yoyote anayetaka kugombea uongozi anatakiwa awe muadilifu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom