Nchi zilizoendela kwa kutegemea msaada wa nguvu za Nyuklia ziko hatarini kurudi nyuma kimaendeleo na hata kuhatarisha Afya za raia wao baada ya kugundua kuwa Mitambo yao haiko salama kutokana na Tetemeko la ardhi la Japan ambalo limeitikisa mitambo yake ya nguvu za nyuklia!!!!
Hivi sasa viongozi wa nchi zinazojiita Tajiri sana duniani wako Ufaransa kwa mkutano maalum na mada kuu inahusu mitambo hiyo huku Mawaziri wa Nishati wa nchi za EU wakikutana Ubelgiji kuzungumzia Tetemeko hilo na hatari ya kuisambaratisha mitambo yao ya Nyuklia!!
Tayari Serikali ya Ujerumani imeamua kudurusu mitambo yake na kuhakiki uwezekano wa kuathiriwa na majanga kama ya Japan!!
Hali hii imesababisha Hisa ktk Ulaya, Asia na USA kuporomoka kwa kasi tangu mkasa huu utokee Japan na kuna hatari ya uchumi wa Dunia kutikisika tena na kusababisha maafa na umaskini zaidi ktk Dunia yetu hii!!
Sasa nchi Tajiri zikiwa zinajiandaa na mikakati ya kujinusuru na maafa na majanga ya Mitambo yao Nyuklia sijui sisi Walala hoi wa Dunia ya 3 tunajiandaaje???
Habari zaidi gonga hapa: BBC News - Japan earthquake: Radiation levels fall at Fukushima