mkush
JF-Expert Member
- Aug 19, 2011
- 214
- 161
Habari wana jamvi!!!
nimepata kukisoma kitabu cha mwalimu Nyerere kiitwacho UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA.katika kitabu hicho mwalimu anaelezea namna alivyopambana kufa na kupona katika kuunusuru muungano-kazi ambayo(kwa wakati huo) ilishadhihirika wazi kuwa iliwashinda rais(MWINYI) na waziri mkuu(MALECELA JOHN) dhidi ya wale wabunge waliojiita G55,anaelezea zaidi kuwa ilifika wakati akajikuta anatoa machozi kwa kulia(nadhani changamoto zilimzidia).hapa sasa ninahitaji wale wenye data za uhakika waturushie majina ya hao wabunge 55 japo kumbukumbu za hii historia ikae sawa hasa kwa sie ambao kipindi hicho tulikuwa wadogo kuweza kufuatilia matukio mbalimbali ya nchi yetu.pia kama kuna lolote la ziada juu ya hili tukio si vibaya likawekwa hapa kwa faida ya wote.
ndaga fijoo!!!