Misukosuko kipindi cha nyerere!!

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
1) Nakumbuka wakati mi mdogo kutoka angani kulipeperushwa karatasi zenye picha ya Mwalimu Nyerere wakati huo akiwa Rais. Picha hiyo ilikuwa ikimuonyesha Rais akiwa ameshika kichwa huku akionyesha sura ya huzuni, majuto na masikitiko! Pembezoni mwa picha hiyo kulikuwa na picha ya mtu mwingine akiwa anatabasamu na kuonyesha furaha na bashasha huku akijaribu kumdhihaki Baba wa Taifa!

Naomba anaekumbuka tukio hili anieleze hiyo picha nyingine ilikuwa ni ya nani? Jee, haya yalitokea kote TZ au ni huku kwetu Kaskazini? pia nakumbuka watu waliamriwa kuchanachana hizo picha haraka na atakae kutwa nazo atakamatwa kama Mhaini!

2) Tukio lingine ambalo liko kichwani mwangu mpaka leo ni kutekwa kwa Ndege ya TZ na kupelekwa Uingereza, Jee, nani anakumbuka majina ya Watekaji, Wako wapi sasa, na walihukumiwaje?

3) Nakumbuka Mwalimu Nyerere alitangaza miezi 18 ya kujifunga mkanda! jee, hiyo miezi 18 ilikuaje? iliisha kama ilivyotarajiwa?

4) Nakumbuka Mwalimu alikuwa na Bakora aliyoipenda sana, jee, ni kweli kuna siku Malkia Wa Uingereza alimpa Mwalimu mkono uliovishwa mpira na Mwalimu kujibu kwa Bakora yake?
 
Mi nilikuwa bado sijazaliwa mwaya hivi ni kweli hayo lakini?
 
We mjomba unajua kila kitu kuhusu haya maswali yako, sema kuwa unataka kulinganisha unavyojua wewe nA wanajamvi wengine.
Kama UNAKUMBUKA kwa kiasi hicho, si ueleze ?
 
Ule mkanda tuliofunga baada ya vita na uganda bado haujafunguka lmpaka leo. tena vita yenyewe ya kujitakia.
msiishie hapo, vita hiyo tulianza tangu 1973 pale wapinzani wa Amin walipoweka kambi zao sehemu mbalimbali hapa nchini na gharama tulizowagharamia. Inauma sana nikifikiria.
 
hatukumbuki!, kwa vile we unakumbuka nenda kawaulize watu kama mzee butiku aliekuwa nae ikulu, warioba na salim watakujibu na mtajadilina!, sasa hivi tuko bize tuna kula rushwa na kupambana na mafisadi at same time!
 
nimeipenda hii
 
Hao wote uliowataja wamo humu JF sasa wewe kama kumbukumbu zimekuishia utaona mwenyewe hao vigogo wakitukumbusha ingawaje wanaingia humu na majina bandia!!
 
Ule mkanda tuliofunga baada ya vita na uganda bado haujafunguka lmpaka leo. tena vita yenyewe ya kujitakia.
msiishie hapo, vita hiyo tulianza tangu 1973 pale wapinzani wa Amin walipoweka kambi zao sehemu mbalimbali hapa nchini na gharama tulizowagharamia. Inauma sana nikifikiria.

Unafiki mwingine mbaya sana. Yaani wewe yanakuuma ya mwaka 1973 haya ya Dowans ya miaka ya 2011 wala hayakuumi??
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom