Miss Tanzania kuna nini jamani...?

Irizar

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
217
18
Tarehe 25/09/2009 nilikwenda Giraffee Hotel kwenye Miss Tanzania Talent show. Kulikuwa na washiriki 8 tu wa mashindano ya talent show kati ya 29:

1- alicheza kihindi
3- wakacheza ngwasuma
2- wakaimba nyimbo za Whitney Houston na Celine Dione wakachemka sana.
1- akacheza TAARABU na siyo ya kistaarabu MATUSI MATUPU YA USWAHILINI.
1- Akafanya play - aliigiza kuwa mama wa kijijini mwenye mimba kubwaa, anakwenda shambani kulima, wkt analima uchungu ukaja akazaa akiwa shambani, jamani it was very tourching, and very sad. Yaani mimi hadi nililia, huyo dada alikuwa amejiandaa vizurii sana, alitengeneza na CD, wkt anajifunguwa tukawa tunasikia mtoto analia yaani kama kweli.

Jamani cha ajabu tarehe 02/10/2009 aliyeshinda TALENT ni mchezaa taarabu, na hiyo taarabu ilikuwa matusi matupu ya aibu sanaaaaa. Baada ya kushinda yule msichana aliyetoa message nzuri kwa jamii kashinda mkata viuno, inasikitisha sana.

Sasa hii kamati ya Miss Tanzania wana maana gani???, wanawafundisha nini watoto wetu?? ndiyo wasichana wakiingia huko inakuwa ni RUSHWA, NGONO, UFISADI ETC.
Tutajikomboaje namna hii?? Maana hata kwenye miss World pia kuna mashindano ya Talent.

Kweli mimi nimesikitishwaaa saanaaa Miss Talent kuwa mcheza taarabu. Maana hata dada hapo nyumbani kwangu nikimfunga kanga anaweza kucheza taarabu, kwa hiyo ana talent!! Siyo kwamba naichukia taarabu, hapana, ila kuicheza siyo talent.

Asanteni
 
waacheni watumie nafasi waliyonayo kwa manufaa binafsi.......kila mtu hula kulingana na ufupi wa kamba yake....akina lindenga hiyo ndiyo kamba yao acha wawafaidi..........
 
Maana hata dada hapo nyumbani kwangu nikimfunga kanga anaweza kucheza taarabu, kwa hiyo ana talent!! Siyo kwamba naichukia taarabu, hapana, ila kuicheza siyo talent.

Ndugu yangu unayozungumza ni ya kweli au? basi Tanzania tunasafari ndefu bado hatujui tunatafuta nini hata huko miss world
 
Ndugu yangu Irizarm, Wasichana 29 wanaopita nusu uchi wakiangaliwa na watu 70,000 waliopo ukumbini kwa raha zao, hawatakiwi kukunyima raha wewe na watanzania wengine 36,000,000 na kutufanya tuache kufikiria masuala nyeti ya nchi yetu na maendeleo ya nchi yetu.
 
What do you expect from Hashim Lundenga and his co!!??

Umeshawahi kukaa nae kumsikiliza upupu anaoongea? Hivi kuna credibility gani kati ya kama kamati yenyewe imejaa shoddy personalities? Yes they are shoddy!!!

SAsa kazi tafuta majaji wa mwaka huu wakueleze jinsi walivyopata washindi na uulize ni jinsi gani wafadhili [wanaoonekana na wasioonekana] wanavyopanga matokeo!!!

Kisha nenda ndani zaidi ujiulize tutafika???

Haya mambo yataleta maana tu iwapo wale watu waliotulia, weledi wa masuala ya urembo, women dignity na natural intelligence wataamua kuandaa yao!!!!! na nina hakika wapo, tukianzia kwa baadi ya previous miss tanzania na wadada repurtable - and there i will support watu kama WOS kuwa ndani ya hiyo kamati, kurudisha hadhi ya wanawake warembo tanzania

TANZANIA BILA UPUPU HUU INAWEZEKANA
 
Yap hilo limepita ngoja tugange yajayo na tuone miss wetu ataifanyia nini jamii
 
Umeongea kitu cha maana, hadi wanawake wenye akili zao wakiandaa mashindano hayo ndipo yataleta maana , lakini hii ya sasa wizi mtupu
 
kwanza mimi nafikiri wazazi wawa elimishe mabinti zao wazijihusishe na ujinga huu wa miss na takataka nyingine.
 
Back
Top Bottom