Miss Kenya V/S Miss Tanzania

Na mi nawaombea wasiwe na uwezo wa kujieleza zaidi ya walio nao hivi sasa, manake tutashindwa kujiexpress nao kirahisi. Na bado hatujapata products za shule za Lowassa (Sekondari za kata), hapo ndipo tutazidi pata burdani nzuri zaidi.

teh teh..kweli kaka..shule za kata zikishaanza gombea umic itakuwa balaa tupu..
 
Firstladdy,
Jiulize wewe ulipokuwa au kama haujafikia age 21 au form 6 -uwezo wako wa kujieleza ulikuwaje hata ukiulizwa maswali na baba na mama tu.Matatizo ni mengi kuanzia mfumo wa elimu,wengine ndio inakuwa mara ya kwanza kushiriki kwenye mambo kama hayo,wengine Tv huwa wanaangalia michezo ya kuigiza tu,ukija ukachanganya na ulimbukeni wetu kuwa english ni kigezo muhimu inakuwa shida tupu maana hawajui miss China au India huwa wanazungumza kikwao.

JF niliangalia miss kenya na kwa aliyebahatika kuiona lol wenzetu kidogo naona wame advance na mabinti wanaconfidance sijawahi kuona

watoto wanajieleza kama hawana akili nzuri mengineyo yalikuwa makosa madogo madogo

Mbona warembo wetu wa Kitanzania upeo wa kujieleza ni mgumu sana???
 
Firstladdy,
Jiulize wewe ulipokuwa au kama haujafikia age 21 au form 6 -uwezo wako wa kujieleza ulikuwaje hata ukiulizwa maswali na baba na mama tu.Matatizo ni mengi kuanzia mfumo wa elimu,wengine ndio inakuwa mara ya kwanza kushiriki kwenye mambo kama hayo,wengine Tv huwa wanaangalia michezo ya kuigiza tu,ukija ukachanganya na ulimbukeni wetu kuwa english ni kigezo muhimu inakuwa shida tupu maana hawajui miss China au India huwa wanazungumza kikwao.

sasa kama nimeamua kuwa "mimi ni kisura najitambua kwa sifa na vigezo vyote inabidi niwe nazo;)
 
mimi nadhani tatizo letu ni kwamba sanaa kwa wabongo wengi ni sehemu ya kupita tu sio serious business kama kwa wenzetu,hatujaamua kuwekeza kwenye sanaa na michezo kabisa,kwahiyo kinachotokea kwa mfano kwenye uwanja wa umiss mabinti wenye sifa na ujasiri unaohitajika walio wengi hawashiriki kabisa wanabaki kwenda kuangalia wenzao wanavyopita jukwaani,nimewahji kuhudhuria shindano moja la urembo nikakuta ukumbini mabinti wenye sifa wapo wengiiiiiii,na wengine wana sifa kuliko washiriki,ila hawashiriki,nchi za wenzetu mtu anashiriki kwa bidii na anajua hata akishindwa ile inaweza kuwa ni hatua moja mbele kwenda kwenye mafanikio katika sanaa ,hapa kwetu ukishindwa ndio umeshindwa,wachache sana wanaoshindwa na ukaendelea kuwaona wanaendelea na sanaa
 
Mabinti wetu kukosa confidence kunatokana na tabia yetu ya uswahili tangu mitaani tunakokulia. Watanzania kwa jumla hatuna confidence na jambo lolote, ndiyo maana akija mtu mgeni tunatetemekea kama nini. Hebu angalia sasa hivi karibu nchi nzima imechukuliwa na wageni na wala hatusemi kitu. Viongozi wetu wanaiba halafu bado tunaandamana kuwapongeza. Kenya hawana ujinga wa namna hiyo, ndiyo maana hata walipoibiwa kura walipigana, sisi tunanyamanza na kusema huo ndio uzalendo. Waziri wa Kenya aliyekula rushwa alivuliwa madaraka papo kwa papo, juzi tumesikia uteuzi wa kijinga uliofanywa na Rais Bunge likakataa papo kwa papo. Mambo hayo hayawezi kutokea Tanzania. Tunajua kabisa kuwa mfanyakazi wa serikali anaiba pesa za serikali lakini ama tunamsifia au tunamwonea wivu.

point taken Kenya na Tanzania kuna tofauti kubwa sana ..watanzania sisi ni waoga sana sijui hali hii itaisha lini?
 
Kuhusu rushwa ya ngono....hivi mnaishi dunia gani nyie??? wee unafikiri unaweza kumpa tu mtu umiss na benefits zote bila kuchojoa kweli???...kuna ambao tunao mtaani walishiriki tangu ngazi za mwanzo na walipigwa chini sababu ya misimamo yao ambayo haina faida kwa waandaaji...hata wanaotoa zile zawadi lazima wawachague wa kuwapa kwanza.....it make sense au vipi???....ungetaka kuelewa ungefika pale kambini kwao girraffe uone wenyewe wanavyoshughulika....tembea uone....
 
Mabinti wetu kukosa confidence kunatokana na tabia yetu ya uswahili tangu mitaani tunakokulia. Watanzania kwa jumla hatuna confidence na jambo lolote, ndiyo maana akija mtu mgeni tunatetemekea kama nini. Hebu angalia sasa hivi karibu nchi nzima imechukuliwa na wageni na wala hatusemi kitu. Viongozi wetu wanaiba halafu bado tunaandamana kuwapongeza. Kenya hawana ujinga wa namna hiyo, ndiyo maana hata walipoibiwa kura walipigana, sisi tunanyamanza na kusema huo ndio uzalendo. Waziri wa Kenya aliyekula rushwa alivuliwa madaraka papo kwa papo, juzi tumesikia uteuzi wa kijinga uliofanywa na Rais Bunge likakataa papo kwa papo. Mambo hayo hayawezi kutokea Tanzania. Tunajua kabisa kuwa mfanyakazi wa serikali anaiba pesa za serikali lakini ama tunamsifia au tunamwonea wivu.

Hapa husemi kweli nadhani kenya ndo ilinunuliwa na mafisadi to enzi na enzi. Huyu anayesema wakenya wana confidence.....labda kiingereza lakini vinginevyo ni maskini tu kama watanzania.
 
huyu lundenga anastahili kubakwa na yeye siyo anamega tu watoto wa maskini
 
sio mamiss tuu wasioweza kujieleza hata wasomi wetu wa vyuo vya juu wakiwa wageni huku utawaonea huruma,nafikiri ile culture ya nidhamu ya woga inasababisha yote haya
 
Mbona warembo wetu wa Kitanzania upeo wa kujieleza ni mgumu sana???
Tatizo wengi wanaoingia katika fani hii ya urembo hapa tanzania hawana IQ ya kutosha na huwa hawajui kama wanatakiwa awe mtu wa aina gani..wanachojua ni kuwa na umbo zuri na kuvaa vizuri tu ili waonekane warembo, Hawajui hata current affairs kuhusu nchi yao.. wapo baadhi hata hawajui nchi hii ilianzisha lini mfumo wa vyama vyingi..

Tena sio warembo tu,wapo wengi, angalia kipindi cha Maisha Plus TBC1 uone ujinga wa vijana wetu.. Nothing kwa kweli..
 
wa kwetu hawa wanajilazimishja kuongea kiingereza wakati hawakijui...watwange hata kisukuma na kingoni si watawekwa wakalimani jamani...hii kasumba ya kuona kuongea kiingereza ndo unajua inaleta taabu sana..
 
Kuna ukweli wowote kama TZ kuna rushwa ya ngono?? mmh

wewe ndo peke yako unaeuliza swali hili,,,,
wasichana wajanja wengi hawagombei na wengi wanaogombea wanatoka
familia za chini,wanakuwa tayari kwa lolote,hata kutoa ngon,ili washinde
 
Hapo umepatia vizuri,hata wakati mwingine kwenye mavyuoni mwenu kuna haya kwa saaana hasa kwenye mitihani,ukitaka kuchunguza nenda vyuoni!
 
Back
Top Bottom