Misri yatoa rushwa kuteka maji ya ziwa victoria

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,142
3,217
Stars yaalikwa Misri

• POULSEN KUANZA KIBARUA NA WENYEJI

na Mwandishi wetu, NAIROBI, Kenya




TIMU ya taifa soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ni kati ya timu tano zitakazoshiriki michuano maalumu ya Nile Basin itakayorindima jijini Cairo, Misri kuanzia Januari 5 hadi 17.
Mbali ya wenyeji Misri, timu nyigine ni Sudan, Kenya, Uganda na Tanzania itakayoanza kibarua dhidi ya Misri.

Ingawa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), halijathibitisha, michuano hiyo ni kipimo kizuri kwa Stars kujiandaa na kampeni ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN).

Stars chini ya kocha wake Mdenish Jan Poulsen, kwa sasa inakamata nafasi ya tatu katika kundi lake la nne, ikitanguliwa na Afrika ya Kati na Morocco huku Algeria ikiwa ya mwisho.

Katika mechi ijayo, Stars itacheza na Afrika ya Kati, kati ya Machi 25 na 27, mwakani hapa nchini.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo ya Misri, siku ya ufunguzi, kutapigwa mechi mbili; Sudan itacheza na Kenya Uwanja wa Jeshi, huku Stars ikicheza na Misri Uwanja wa Taifa wa Cairo.

Januari 8 kutakuwa na mechi mbili kati ya Uganda dhidi ya Sudan itakayochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Kijeshi.

Michuano hiyo itaendelea tena Januari 11 kwa mechi kati ya Kenya na Uganda kwenye Uwanja huo huo wa Jeshi.

January 14, itakuwa zamu Kenya kukipiga na Tanzania kwenye Uwanja huo wa Chuo cha Jeshi, wenyeji Misri dhidi ya Kenya.

Januari 17 Stars itaivaa Uganda huku mechi ya itapigwa uwanja wa taifa wa Cairo, kati ya wenyeji dhidi ya Sudan.
 
Kweli hii ni rushwa na kwa kuwa wabongo wanaotutawala hawana uchungu na taifa letu they will do nothing but seeking their own interests.
 
..JK si alipitia hapo wakati akienda Ubelgiji.

..hili suala la maji ya ziwa Victoria litasababisha watu watoane ngeu ktk jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
..JK si alipitia hapo wakati akienda Ubelgiji.

..hili suala la maji ya ziwa Victoria litasababisha watu watoane ngeu ktk jumuiya ya Afrika Mashariki.
wakenya, waganda, warundi, warwanda watashtukia na kukataa gestures za Misri, Tanzania na huyu Kikwete atawasaliti wenzie, watch!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom