Mishahara ya wake zetu

Inategemea busara zako , kwa maana ukianza maisha na busara ya matumizi ya pesa, mkeo pia atakuwa na busara katika pesa na kushiriki moja kwa moja katika kuchangia maendeleo ya familia. hii inamaanisha kama matumizi ya pesa zako yatoonekana yanaleta maendeleo, mkeo atafuta nyayo. msiogope kuoa wafanyakazi.
 
mwanaume aliambiwa na muumba, uzae uwe na familia na mtakula kwa jasho lako. mwanamke akaambiwa utazaa kwa uchungu. Labour naingia mwenyewe kusukuma mtoto kwa machungu, halafu eti mshahara wangu niweke mezani..! nyie wababa vipi? mbona hamnazo? wanaume wa kileo kupenda dezo! hebu tuleeni sisi na watoto wetu kwa jasho kama mlivyotumwa, achaneni na mishahara yetu. nikisaidia ni mapenzi yangu lakini sio wajibu wangu na huna sababu ya kuuliza au kukwazika juu ya hilo.
 
Anadamka asubuhi kwenda kibaruani, anachelewa kurudi kibaruani sababu ya foleni afu nisiujue mshahara wake na unatumikaje?....... I better marry my mom!

Othetwise akae nyumbani anilelee wanangu.... PERIOD!
 
Jamani kuna malalamiko miongoni mwa wanaume waliooa wanawake wafanyakazi kuhusu mchango wa mishahara yao ktk matumizi ya familia. Nina marafiki wangu kadhaa (waliooa wake wafanyakazi) wote wanadai eti ukitaka kuishi kwa amani na mkeo usimuulize kuhusu mshahara wake. Nilishangaa sana kusikia hivi kwani mara nyingi huwa nasikia vijana wengi wanataka kuoa wasichana wenye kazi ili waweze kusaidia ktk kupunguza ukali wa maisha. Naombeni uzoefu wenu ktk hili jamani. Natanguliza samahani kama topic ilishaongelewa huko nyuma, ila ningetamani kuona hizo sred ili nisome maoni ya wadau!

Nimeipenda hii!
 
Anadamka asubuhi kwenda kibaruani, anachelewa kurudi kibaruani sababu ya foleni afu nisiujue mshahara wake na unatumikaje?....... I better marry my mom!

Othetwise akae nyumbani anilelee wanangu.... PERIOD!

Well said mkuu!
 
Mkuu sioni kwanini niulize mshahara wa wife unakwendaje..., lakini tashangaa kama kila siku naulizwa chumvi na vitu vidogo vidogo.., siwezi kumpangia matumizi lakini yeye mwenyewe kwa busara nina uhakika kuna mengi atafanya na pindi nikiwa juu ya mawe sidhani kama ataniangalia tu..

Cha maana put your cards on the table.., kwamba this is what we have..., here is where we need to go.., and here is where we are..., kwahio kufika huko tunakotaka and the way we are spending something needs to be done. Kwahio mnapanga jinsi ya kutumia na ku-invest na sio kumuuliza pesa yako ipo wapi utafikiri wewe ndio benki ya kumuwekea (mshirikishe kwenye miradi yenu na mshauriane)
 
ni vitu muhimu sana kuvijadili kipindi cha uchumba. lazima muelewane how to save our salary, kiasi gani tule. panga mipango yenu kwa pamoja ya siku, ya mwezi , ya miezi mitatu, ya nusu mwaka, ya mwaka, ya miaka mitatu nk hayo yote yatajiseth. lazima awepo accountant nk ndo maana kuna aina nyingi za account.

Mnachojadili wakati wa uchumba, haki-apply mkishaoana; ukitaka ndoa ife mapema, lete mambo ya uchumba!
 
Kama ndo hivyo basi mimi namshukuru sana Mungu kwa ajili ya mke wangu. Maana yeye mshahara akipata tu anajua ni mali ya familia. Ni ama atafanya shopping ya humo ndani chakula na mazagazaga yote ya mwezi mzima au atauleta tupange pamoja tunataka kufanya nini katika mwezi husika.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Mkuu sioni kwanini niulize mshahara wa wife unakwendaje..., lakini tashangaa kama kila siku naulizwa chumvi na vitu vidogo vidogo.., siwezi kumpangia matumizi lakini yeye mwenyewe kwa busara nina uhakika kuna mengi atafanya na pindi nikiwa juu ya mawe sidhani kama ataniangalia tu..

Cha maana put your cards on the table.., kwamba this is what we have..., here is where we need to go.., and here is where we are..., kwahio kufika huko tunakotaka and the way we are spending something needs to be done. Kwahio mnapanga jinsi ya kutumia na ku-invest na sio kumuuliza pesa yako ipo wapi utafikiri wewe ndio benki ya kumuwekea (mshirikishe kwenye miradi yenu na mshauriane)

Nimekusoma!
 
Inategemea busara zako , kwa maana ukianza maisha na busara ya matumizi ya pesa, mkeo pia atakuwa na busara katika pesa na kushiriki moja kwa moja katika kuchangia maendeleo ya familia. hii inamaanisha kama matumizi ya pesa zako yatoonekana yanaleta maendeleo, mkeo atafuta nyayo. msiogope kuoa wafanyakazi.

Ushauri wako umetulia!
 
Kwa avatar yako hii inaniwia vigumu kufuata ushauri wako juu ya kutumia busara. Sijui kama wewe una-apply hiyo principa
 
mshahara wa mwanamke ni kuishia saluuni babu,hujui sie wanawake ni mapambo ya nyumba lazima tupendeze muda wote?lol....

ukiwa una date na mtu jaribu kuwa muwazi kwa mkeo mtarajiwa,mipango yako ya baadae na kumshirikisha pia. ....eg umeona kiwanja na unataka kununua,unaweza ukamshirikisha kwa kumwambia akuongezee kiasi fulani cha pesa...sio lazima iwe nusu kwa nusu.................,na hata mkitoka sio ujionyeshe wwe ndio kidume kwa kulipia kila kitu...unaweza kumwambia unalipia chakula yeye alipie drinks....ukijenga tabia hii tangu mwanzo...utamfanya achukue rensponsibilities na yeye,awajibike hata kwa mambo yanayofuata ktk ndoa yenu....wengi wanakosea tangia mwanzo anamjenga mpenzi wake kuwa tegemezi kila kitu hadi vocha baadaye inakuwa ngumu kubadilisha system........

na pia mkeo ni rafiki yako,tangu mwanzo kuwa na tabia ya kuwasiliana naye jambo unalopenda na usilopenda....hii itakurahisishia baadae kumface na kumwambia jambo lolote kama unaona anaenda sivyo.usiwe mtu wa kunyamaza kimya au kujifanyia mambo mwenyewe itakucost siku moja.

Too theoretical mama labda wewe upo hivi. Wakati wa uchumba ubahili, uchunaji, matumizi mabaya ya fedha vinafichwa sana na wadada wakishaingia ndo utajuuta kuwafahamu
 
Mbona picha ninayoipata siku hizi ni ya wanawake wengi kuwa ndio watunza familia na waume zao? kadri siku zinavyoenda wanaume wanasahau majukumu yao sio kama kizazi cha wazazi wetu. Wanawake wengi (katika circle ya marfiki na watu wa karibu) wanalalamika sana kuhusu waume zao kuwepo tu kama picha hawajali maendelea ya familia wao ni pombe na vimada nothing else.
 
simuuliz mke wangu mshahara coz she is
da best house keeper and budgeter ever!
Hajawahi lalama nimempa pesa ndogo so it means mayb anaongeza na zake samtimes.
.... mkeo ana HEKIMA..... nawewe una HEKIMA........ halafu..... UMEMZIDI KIPATO.......!!!!
 
Mwanaume si ndio kichwa cha nyumba, sasa maswali ya mshahara wa mke yanatoka wapi? kwani wewe wakati unaoa hukujiandaa? hadi uje uulize mshahara wa mkeo?
 
Back
Top Bottom