Mishahara ya madaktari!

Huyo Asha Kigoda kwanza qualification zake sio za Daktari kamili wa Degree, halafu kutokana uwaziri wake analipwa zaidi ya hao wataalamu.
Pili tatizo ni letu sisi la kukubali Professional issue kutolewa uamuzi na watawala.
Eg Madaktari Bingwa walitakiwa washirikiane na Junior Doctors, na wasikubaliane na hii divide and rule, maana madaktari bingwa labda wao wanalipwa vizuri, wanasahau kuwa nao walikuwa junior doctors hapo mwanzo, na pia watoto wao watakuja kuwa junior doctors, wakati wao wamestaafu, hivyo wana hitaji msaada wa watoto wao, au ile hali ya kuwatakia mafanikio na maendeleo katika maisha yao
Cv ya Naibu waziri wa Afya hii hapa

School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
AMO Training School - KCMC Advanced Diploma in Clinical Medicine 1985 1987 ADV DIPLOMA
Medical Assistant College - Bugando Diploma in Clinical Medicine 1975 1977 DIPLOMA
Korogwe Girls' Secondary School Secondary Education 1969 1972 SECONDARY
ST. Annes Girls' Primary School Primary Education 1966 1968 PRIMARY
Mswaki Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY

--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list

--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Ministry of Health & Social Welfare Deputy Minister 2006
RAS-Dodoma Ag. District Medical Officer 1992 1998
Dodoma Region Medical Officer 1992 1998
Tanzania Parliament MP's Medical Doctor 1992 1998
Dodoma Region Senior Assistant Medical Officer 1987 2000
RAS-Dodoma Medical Assistant 1977 1985

--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member, UWT National General Council 2003 2008
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Regional Exec. Committee & NEC 2002 2007
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Parliament of Tanzania 2000 2005
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of the Regional Political Committee 1997 2005
TANU Youth League Member 1966 1968
 
Naomba wanaJF mnisaidie katika mjadala huu, maana nahisi labda mwandishi wa habari kakosea hii figure, labda kafuta sifuri moja mwishoni! Hasa Ndugu Dotori naomba mchango wako maana ni wewe pekee ninayekumbuka katika forum hii ambaye umejitambulisha ni daktari. Na wengine pia tafadhali.

Ati ni kweli daktari bingwa huko Zanzibar baada ya kupandishwa mshahara mwaka huu ndo sasa analipwa sh laki na nusu (150,000) kwa mwezi?
Gazeti la Majira la leo lina habari kuwa wamegomea mishahara hiyo, kama nilivyobandika hapa chini.

Madaktari Zanzibar wagomea mishahara


Na Ali Suleiman, Zanzibar

WAFANYAKAZI wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwamo madaktari bingwa, wamegomea mishahara mipya iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa madai kwamba ni midogo kulingana na taaluma zao.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Sultani Mungheiry, alikiri jana kuwapo tatizo hilo na kusema wizara yake inafanya marekebisho ya viwango vipya vya mishahara.

"Ni kweli tatizo lipo tunalifanyia kazi, kuona viwango vipya vilivyotangazwa na Serikali vinawanufaisha wafanyakazi wa Wizara ya Afya, wakiwamo madaktari," alisema.

Yamejitokeza malalamiko kwa watumishi wa SMZ baada ya kutangazwa kwa viwango vipya vya mishahara na Serikali.

Ofisa wa Idara ya Utumishi, alikiri kuwapo kwa tatizo hilo na idara hiyo kutoa tamko la wafanyakazi kuchukua mishahara hiyo hadi itakapofanyiwa marekebisho.

Kasoro kubwa zilizojitokeza katika mishahara mipya ni kwamba baadhi ya watendaji wakuu wa Serikali, wakiwamo wakurugenzi wa Serikali kupata mishahara midogo, tofauti na watumishi wao.

Hatua hiyo imefanya baadhi ya wakurugenzi kutishia kugoma kupokea mishahara mipya, iliyotangazwa na SMZ.

Hivi karibuni, Rais Amani Abeid Karume, aliwataka watumishi wa SMZ kuvuta subira huku marekebisho ya mishahara mipya yakifanywa.

Daktari bingwa katika Wizara ya Afya ambaye hakutaka jina lake litajwe, iliitaka wizara hiyo kurekebisha mishahara haraka au vinginevyo wahame na kutafuta maslahi bora sehemu nyingine.

Madaktari bingwa Visiwani hapa, hulipwa kati ya sh.150,000 kwa mwezi, kiwango ambacho kinalalamikiwa na wataalamu hao kulinganisha na wenzao wanavyopata Bara.
Ni 1.5M sio 1.5K
 
Kweli mkuu. Mm nauza matikiti hapa Zanzibar, wengi wa wakuu wa wilaya, wakuu wa polisi, na wengineo hapa wanatembea kwa miguu na wanaomba omba matikiti yangu mpk aibu
Duu wanakuomba hadi matikiti aisee, Jecha Mungu anakuonaa.
 
Sawa,
1. Wafanyakazi Afya walipwe 2.4m hata zaidi.... haina neno! Kwani hayo mashangingi na gharama la kuyaendesha ni kiasi gani?
Kama Mshahara wa daktari mmoja ni 2.4m *12 = 28.8 m. (Kwa mwaka). Kununua shangingi 1 analotumia Mkurugenzi wa Kawaida tu Wizarani utalipa madaktari watatu! Achilia mbali gharama ya uendeshaji wa hilo shangingi!

2. Sii kweli serikali haina pesa- ni matumizi tu makubwa ya kifahari na kuwasahau walalahoi! Kama serikali ikiamua kudhiditi matumizi na kuachanana na ufahari- then itapatikana pesa kuwalipa vizuri tu wafanyakazi!
Wewe unataka kuturudisha huko kwenye mateso na machoziii. Hujui kama sasa hivi tunafutwa mateso na machozii?? Mashangingi yathamani yataendelea ilitufurahie kabisaa
 
Back
Top Bottom