Mishahara midogo Madaktari Visiwani- hadi lini?

Hoja yako ya madktari wakimbie mimi naona ni dhaifu!

Je waendelee kukimmbia nchi hadi lini na kwa faida ya nani?

Kwa nini isirekebishwe wakae Visiwani wawahudumie Watanzania mliotuacha tunateseka mkakambilia ugenini?

Uzalendo maana yake ni nini?

Uzalendo?? r u kidding me??. Pesa zinaliwa na waziri wizarani halafu wewe unaongelea uzalendo!!? tena ukikimbilia kukandamiza muungano, wakti suala hili si la muungano. Yes, soln ni kuingia mitini, labda then wataelewa na hao wananchi pia wataelewa kuacha kuchagua majiserikali mabovu.
Wallahi naomba itokee siku, mmoja wao apate emergency wakose hata mtu wa kum-stabilize kabla ya kumpeleka huko wanakopelekana kwa matibabu, pia labda then wataelewa.
Kwa taarifa yako ni umoja tu hakuna, ama sivyo majority ya MDs bongo hasa vijana wangekuwa wameshakula kona zamani!.
 
Kama nilivyosema hapo juu, mie si mshabiki wa muungano. Hata bara mishahara ya madaktari ilikuwa midogo mpaka watu wakagoma. Taaluma nyingine pia mishahara si mikubwa kihivyo na wahusika wanajua jinsi ya kufanya kushinikiza serikali kuwaongezea. Kuna mtu hapa katoa mfano wa wawakilishi mia kwa pop ya 1mil visiwani uki-compare na wabunge 300 including toka visiwani kwa pop ya karibu 40mil ktk muungano...........huoni hapo kwamba watu wabara wanaweza kulalamika kwamba uwakilishi wao serikalini ni mdogo!!!?. Ukweli ni kwamba hata huo uwakilishi ni mkubwa sana ukifananishi na nchi za magharibi kwa pop ya 40mil. Point yangu hapa ni kwamba, matatizo yetu tunajitakia kwa ku-spend kidogo tulichonacho ktk masuala yasiyo muhimu na hasa ya kisiasa!!!.
Punguza serikali, weka uwajibikaji wizarani na e.t.c...then pesa ya mishahara itapatikana. Lakini kuja moja kwa moja na kukandamiza muungano ni makosa, kwani kwa mtu kama mimi naona ni kisingizio na ndio maana tunashindwa ku-solve matatizo yetu kwasababu hatwishi visingizio.! Dili na wizara husika, wabaneni au madaktari wagome kama wenzao wa bara mwaka ule uone nini kitatokea...........lakini hilo yengele la muungano this, muungano that halitabadilisha chochote.
mawazo yako ni mazuri sana kaka yangu ,lakini unaonekana ni mgeni kiasi fulani wa siasa za zanzibar,kugoma ama kuandamana kwa kudai haki yako zanzibar ni sawa na kupoteza muda wako kwani hilo tatizo halitatuliwi na badala ya yote utafutwa kazi ndani ya sekunde,si hasha pia ukaishia gerezani kwa kuambiwa umeipotezea serikali nyanzo. kuna migomo kadha imefanyika zanzibar na badili ya kuleta mageuzi imeleta balaa zaidi.mfano wa hayo ni pale wanafunzi wa pemba walipogoma na wakaishia kufukuzwa shule na hadi leo wanamangamanga na njia huku wakijuta kwanini waligoma?ipo mifano mingi ,ukiitaka nambie ni ku PM. zanzibar ni kwetu lakini hakuna politic kuna poll trick.
 
Kaka,
Nimekupata vizuri hasa, kwahivo tatizo ni la Zanzibar na si suala la muungano.....ukikubali hilo tu, utakuwa tayari umepiga hatua moja kubwa sana kuelekea ufumbuzi wa kudumu wa matatizo ya aina hii. Matatizo ya zanzibar yatatatuliwa na wazanzibari wenyewe, hivo basi tuache kuupaka matope muungano..........don't get me wrong, I aint a muungano supporter in any way, type or shape!!. I wish uvunjike hata sasa hivi, ili kila watu wabebe mzigo wao wenyewe na sio kutupiana shutma ziso msingi.
 
u have my support. kwa hili nadhani tuilaumu SMZ.
 
Uzalendo?? r u kidding me??. Pesa zinaliwa na waziri wizarani halafu wewe unaongelea uzalendo!!? tena ukikimbilia kukandamiza muungano, wakti suala hili si la muungano. Yes, soln ni kuingia mitini, labda then wataelewa na hao wananchi pia wataelewa kuacha kuchagua majiserikali mabovu.
Wallahi naomba itokee siku, mmoja wao apate emergency wakose hata mtu wa kum-stabilize kabla ya kumpeleka huko wanakopelekana kwa matibabu, pia labda then wataelewa.
Kwa taarifa yako ni umoja tu hakuna, ama sivyo majority ya MDs bongo hasa vijana wangekuwa wameshakula kona zamani!.

YournameisMINE,
Seikali mbovu tu unayoiona ni SMZ? Naamini pengine kuna la kurebisha! Change of govrt- is just one thing siyo jawabu-Kwani Malawi na Zambia tumeona upinzani in power- are they better than Tanzania today?

What happened in Bara hadi kpandisha mishahara ya sector ya Afya for 100% je ni CUF au CHADEMA waliingia madarakani?

Bado sioni kwa haswa wafanyakazi wa sekto ya afya kutopewa kupaumbele Visiwani- mtu hutambua umuhumu wa hawa watu pale tuu anapougua!
 
kugoma ama kuandamana kwa kudai haki yako zanzibar ni sawa na kupoteza muda wako kwani hilo tatizo halitatuliwi na badala ya yote utafutwa kazi ndani ya sekunde,si hasha pia ukaishia gerezani kwa kuambiwa umeipotezea serikali nyanzo

Nilikuwa nahoja tofauti kidogo na wewe mkuu.

Kwani hao wa bara hiyo laki sita wameanza kuipata lini? cha kujiuliza waliipataje? 'No seet without sweat'
Kwa bara migomo na maandamano ya ma MD haija anza leo wala jana. Hii ya mwisho ilikuwa kubwa kuliko na kweli ikaleta ahueni katika sekta ya afya, kwani baadae na kada nyingine zikajiunga katika huo mgomo. Pamoja na kuwa watu walifukuzwa kazi, waliokuwa vyuoini walifutiwa ufadhili, serikali ikasema itaajiri wataalamu kutoka kyuba n.k.

Mimi naamini SMZ inaweza kuwalipa madaktari wake wakiamua
Kwani hao madaktari wako wangapi?
Statistics zinasema ni 0.02/1000 (TZ) population, (kama 24 hivi kwa population ya 1.2 M-ZNZ)

Kukimbia nchi si suluhisho, mabadiliko ya kweli katika nchi yanaletwa na wananchi wenyewe.
 
In the perfect situation, serikali ingejitoa katika huduma za afya na ku encourage sekta binafis sio tu kutengeneza ajira bali ajira zitakazowafanya wananchi wamudu kununua huduma zitkazowalipa madaktari kima cha chimi cha 600,000 (bara na visiwani)

Mimi si mtaalamu wa mambo ya uchumi,
Ku encourage Private sector katika afya ni jambo zuri, kwanza serikali itapunguziwa gharama kubwa za uendeshaji, na pia huduma za afya zitakuwa bora.

Tanzania tunachangamoto nyingi ili kufikia equitable access katika afya.
...Angalia tofauti ya health services distributions kati ya mijini na vijijini. Vijijini private facilities zilizopo ni za kidini.
...Urban/Rural population ratio 24/74
...Angalia pato la mwananchi wa kawaida na hasa wa kule kijijini.
Angalia.
...Anaglia prevelence ya HIV/AIDS, TB and other infectious diseases.
....Accessibility of safe water, (hii ndio tiba ya magonjwa mengi ya maambukizo yanayokability wananchi vijijini)

Na nyumbani hakuna price control ya huduma za za afya.
Coverage ya insurance nafikiri iko kama 4%ya walio katika ajira fulani.

Je serikali itajitoa vipi?
 
Kasana,
Tuchukulie Health care kama special good- tofauti na zingine, what do you mean by private sector- kwani sasa hazipo?

The specialness of health care- inafanya mataifa mengi kutoa huduma hizi bure- au kuchangia tu ni kwa wele wenye uwezo! Afadhali uwe maskini uende hospitali utibiwe kuliki kushidwa kabisa kwa kukuosa pesa na kukaa home husubiri kifo au kudra za Mwenyezi Mungu!

Serikali ipunguze matanuzi tu- hayo mashangingi na madereva ya kila mkurugenzi pesa sinatosha- kuwapa wananchi wasio na uwezo huduma- angalia Cuba ni maskini kiuchumi- ila unajua Afya za Wacuba ni Bora leo hii (Life Expectancy) kuliko US? US in watu mil. 50 hawana Insurance yoyote...si sawa na Cuba...kila mtu na uhakika wa tiba!
Ni sera tu- ya serikali, kwani afya ni muhimu kila mtu akiugua we maskini wala tariji apewe huduma!

Shangingi 1 ni 120m kununua ni gari ya mkurugenzi 1 tu kumpeleka ofsini na kwenye vikao- kama ukiamua kuajiri na kulipa madaktari vizuri at 1 m kwa mwezi kila daktari- kwa mwaka utalipa madaktari 10! Je yako mashangingi mangapi? Na kila siku yananunuliwa!

The problem sii kuwa tu maskini- we have a far much bigger problem ya matanuzi- nenda China au India kisha angalia magari ya serikali- ni ya kawaida tu!

Kwanza we set our spending priorities 1st- then tuwalipe wataalamu wetu vizuri- hawatakimbia- na walioko nje watarudi!
 
Kasana,
Tuchukulie Health care kama special good- tofauti na zingine, what do you mean by private sector- kwani sasa hazipo?

Kuencourage private sector ina maana kuwe na hospital nyingi za private kuliko za serikali. Sehemu nyingi mikoani health facililties za serikali ni 84%.
kuwe na Private-Public Mix, kwa ajili ya kuongeza physical access na ushindani katika kutoa huduma, (demand and supply)
Lakini ili kuweza kuwa na balance ya hizi huduma katika private na public ni lazima price ziwe controlled/regulated.

The specialness of health care- inafanya mataifa mengi kutoa huduma hizi bure- au kuchangia tu ni kwa wele wenye uwezo!

Kila kitu kina pro na cons.
Kutoa huduma bure - kuna ongeza overutilization of health services,
ukichangisha - Create barrier to poor people na kutapunguza health care utilization n.k.
Kuchangisha kwa wale tu wenye uwezo- How do you know that? which extent utasema huyu hana uwezo?. Huko vijijini wengi hawana uwezo.
Hapa pana dilema. Sababu hata hicho kinachochangwa ni kidogo, ikumbukwe kuwa huduma za afya katika hospitali nyingi za serikali price zake ni karibu 50% off ya actual price. (Dar inaweza kuwa tofauti)

Afadhali uwe maskini uende hospitali utibiwe kuliko kushidwa kabisa kwa kukuosa pesa na kukaa home usubiri kifo au kudra za Mwenyezi Mungu!

Mkuu ,
hapa ninapingana na wewe kidogo.
Hospital zetu za serikali ikiwemo na vituo vya afya, chance ya kufa ni kubwa kuliko kupona unapolazwa huko.
Nyingi hazina madawa ya kutosha, vitendea kazi, madaktari wenyewe hawaonekani, ukimtafuta umvizie kwenye zahanati yake binafsi au private anakobangaiza (kuongeza maslahi).
Mfano pale muhimbili, wa issue ya Didas na Mgaya, Medical officer incharge alikuwa wapi kuidhinisha majina ya wanaotakiwa kufanyiwa oparation? ni wazi majunior Dr. huwa wanafanya hivyo, ndio maana operation ziliendelea pamoja na kuwa kulikuwa hakuna signature ya mkuu wa wodi.
Hapo ni Dar tena MOI, vipi kule Nanjilinji? Kilwa kivinje, au Tandahimba?

Serikali ipunguze matanuzi tu- hayo mashangingi na madereva ya kila mkurugenzi pesa sinatosha- kuwapa wananchi wasio na uwezo huduma-

Hapa nakubaliana na wewe,
ila cha muhimu ni lazima tuwaelekeze wananchi wetu wasisubiri kupewa, wanatakiwa kutafuta kwa bidii.
Kingine ni kudhibiti matumizi yasiyo na lazima, matumizi hewa, over invoicing of supplies including drugs etc

angalia Cuba ni maskini kiuchumi- ila unajua Afya za Wacuba ni Bora leo hii (Life Expectancy) kuliko US? US in watu mil. 50 hawana Insurance yoyote...si sawa na Cuba...kila mtu na uhakika wa tiba!

Hapa mkuu napingana na wewe, pamoja kuwa sijafika Marekani, Insurance for 'poor people' ipo huko.
Milioni 50 kati ya watu wangapi? ni sawa na asilimia ngapi? How about social security system? is not supportive?

Ni sera tu- ya serikali, kwani afya ni muhimu kila mtu akiugua we maskini wala tariji apewe huduma!

Kweli, na ukizingatia sera yetu iko kwenye curative zaidi, kuliko preventive. Ndio maana waheshimiwa walifuta michezo mashuleni na tukawa na Aspen Miss Tanzania.

The problem sii kuwa tu maskini- we have a far much bigger problem ya matanuzi- nenda China au India kisha angalia magari ya serikali- ni ya kawaida tu!

Kweli, si unajua tunapenda makuu,
Hivi yale mabenzi yaliyonunuliwa wakati ule kwa ajili ya kukodishwa, bado yapo? au yalishayeyuka?
Huu utaratibu wa kupenda makuu upo hadi kwa wananchi, tunashindana kununua simu za bei ghali. Kina mama wanakopa mikopo ili kununua WAX, wakati mwanae hata chupi ya kuzuia mkojo hana.

Kwanza we set our spending priorities 1st- then tuwalipe wataalamu wetu vizuri- hawatakimbia- na walioko nje watarudi!

Naungana na wewe asilimia zote.
Na ili kusaidia na kufanikisha hayo yote, tunawaomba warudi nyumbani ili kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Nchi nyingi tu zimeendelea kutokana na raia wao walioenda kusoma ughaibuni, kurejea na kutumia ujuzi waliojifunza huko kwa mazingira ya nyumbani kwao na kuchochea maendeleo.
 
Kasana,
Kuencourage private sector ina maana kuwe na hospital nyingi za private kuliko za serikali. Sehemu nyingi mikoani health facililties za serikali ni 84%.
kuwe na Private-Public Mix, kwa ajili ya kuongeza physical access na ushindani katika kutoa huduma, (demand and supply)
Lakini ili kuweza kuwa na balance ya hizi huduma katika private na public ni lazima price ziwe controlled/regulated.
Mimi siamini sana private in health- health care is a special commodity- hii inawafanya wachache kufaidika na wengi kuwa segregated- basic care iwe tu free kwa wote- na watu walipe tu kodi! To put health in the hands of private- je serikali inajiondoa ktk wajibu? kwa nini watu wanalipa kodi? Private should be for rich people or other expensive conditions na siyo primary care! Serikali ijenge tu Vituo vya afya kila kata- huu ndo wajibu!

Mkuu ,
hapa ninapingana na wewe kidogo.
Hospital zetu za serikali ikiwemo na vituo vya afya, chance ya kufa ni kubwa kuliko kupona unapolazwa huko.
Nyingi hazina madawa ya kutosha, vitendea kazi, madaktari wenyewe hawaonekani, ukimtafuta umvizie kwenye zahanati yake binafsi au private anakobangaiza (kuongeza maslahi).
Mfano pale muhimbili, wa issue ya Didas na Mgaya, Medical officer incharge alikuwa wapi kuidhinisha majina ya wanaotakiwa kufanyiwa oparation? ni wazi majunior Dr. huwa wanafanya hivyo, ndio maana operation ziliendelea pamoja na kuwa kulikuwa hakuna signature ya mkuu wa wodi.
Hapo ni Dar tena MOI, vipi kule Nanjilinji? Kilwa kivinje, au Tandahimba?
Ubora pia ni jukumu la serikali pia- ipunguze matumizi pengine au dhahabu inayouzwa iboreshe hizi huduma. Wafanyakazi wa afya walipwe tu vizuri- wapewe contract interns wakimaliza wasign 7 years kufanya kazi serikali. Pia serikali viongozi watibiwe Tz- hii itaboresha hizi huduma- pia wanaweza hata kuchukua madaktari wa nje!

Hapa mkuu napingana na wewe, pamoja kuwa sijafika Marekani, Insurance for 'poor people' ipo huko.
Milioni 50 kati ya watu wangapi? ni sawa na asilimia ngapi? How about social security system? is not supportive?
Ni kweli in the US 50 mil kati ya 300m population hawana any insurance! Cuba wote wana free care na Life Expentance ni 76 wanaume na 80 Wanawake! Insurance ya poor US ndo serikali imepitisha proposal Congress- bado kuna debate- na hata kama wameanza ni mwaka huu tu- ila pia it does not cover all 50m uninsured poor poeple! Bado Cuba wana advantage- Health Care sii kama missile technology it is a special good- na Cuba inawazidi US kwa hili!

We just need to re-visit our national priority spending- we spend kwa vitu visivyokuwa na maana na pia we collect only 25% of our taxes in private seactor! Ziko pesa nyingi tuu- tuache hizi nadharia za vitabuni na machapisho (with funding from US)yanayoendeleza sera za kuwalazimisha watu wazee, maskini, na akina mama kuchangia afya wakati ni jukumu la serikali kuhakikisha usalama wa afya zao- kama wanadamu na pia kama wapiga kura!
 
Mzalendohalisi Cuba propaganda nyingi hata hizo figures haziko reliable.Kuna watu kibao wamefanya research ndani ya Cuba ku=dispute hizo figures.
 
Mzalendohalisi Cuba propaganda nyingi hata hizo figures haziko reliable.Kuna watu kibao wamefanya research ndani ya Cuba ku=dispute hizo figures.

Pundit,
Lolote linasemwa over Cuba linainekana ni propaganda! Tusiingie ktk debate tofauti!
1. Life Expectancy data ni UN na WB na ndo hutoa hizi data kwa mataifa yote.
2. 2004 Wizara ya Afya na key officials Tz walikuwa na 3 week working visit Cuba- waulize walioona in health care!

Tatizo jingine naona pia media, journals na utandawazi za mgharibi zinatufanya tunaacha kuangalia mambo on the other side! All are not roses in Cuba- ila angalau mtu akifanya vizuri- hata kama ni moja please we learn to acknowledge!
 
MzalendoHalisi. Nakuunga mkono. Hakuna anayebisha kuwa Cuba kiafya wamepiga hatua kubwa. Nchi nyingine kama sikosei ambayo imepiga hatua kubwa kulingana na uchumi wake ni Sri Lanka. System ya afya ya marekani ni bomu! Heri ulaya. Kama ulivyosema, cha msingi ni kupriotise. Maofisini wakubwa wote wana self-container(?) kwa hiyo vyoo vya wengine vina hali mbaya! Tuwekeze kwenye hospitali zetu na tubanane mbavu humohumo na wakubwa utaona mabidiliko. As long as jamaa wao wanapima macho ulaya hali itakuwa mbovu. hili halikwepeki.
 
Kama ulivyosema, cha msingi ni kupriotise.

Naungana katika hii ya priorization. Kwani ni ji jambo la muhimu si katika maendeleo ya nchi peke yake, bali hata katika ustawi wa mtu binafsi.

Priority katika National level haitoshi kusukuma maendeleo, kama hizo priorities kwa watendaji zitakuwa hazijaeleweka. Watendaji wetu hawajawezeshwa kuwa na elimu ya kuprioritize vitu au kuinterpret na kuweka hizo priorities katika practice. Sijasoma MKUKUTA, lakini naamini umeainisha hizo priorities ili kupunguza umasikini na kukuza uchumi.

Mimi napenda kuona huduma za afya zinatolewa katika hali sawa, kukiwa hakuna tofauti ya Private or Public, na mtu achague mwenyewe kwenda kutibiwa popote bila kuwa na hofu ya gharama. Hii inawezekana kama serikali itasubsidise. (Tax & social security funds).

Watendaji karibu wote katika serikali wanamushikeli, kuanzia National Level hadi vijijini.Kwa ajili ya hili hakuna wa kumwajibisha mwenzake, kwani wote wanapokea rushwa, wote wanafuja mali za umma.

Kunahitajika mapinduzi ya kifikra na kiutendaji ili kusonga mbele.
Naamini hata watu ukiwapa millioni kadhaa kwa mwezi, kama wameshazoea kuiba na rushwa (ufisadi), hawataacha.Ndio maana viongozi wetu kila kukicha wanafanya bidii ya kujitajirisha zaidi.

Mabadiliko ya kweli yanatakiwa yaanze katika ngazi ya jamii, vituo vya afya. Na wananchi kuparticipate katika hizo priority/mission/vision.
 
•
SMZ yabembeleza madaktari wake

Habari Zinazoshabihiana
• Waziri Kiongozi akemea madaktari 21.10.2006 [Soma]
• Miili ya madaktari waliokufa Nijeria kuwasili kesho 03.11.2006 [Soma]
• Madaktari Zanzibar wagomea mishahara 22.12.2007 [Soma]

Na Ali Suleiman, Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewabembeleza madaktari na wafanyakazi wa taasisi za afya, kuacha kugomea mishahara yao huku tatizo lao likishughulikiwa kwa ufumbuzi.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Sultani Mungheiry, akizungumza na waandishi wa habari jana alisema dosari katika mishahara ya madaktari inashughulikiwa.

"Tatizo hilo tunalifanyia kazi...tunawataka madaktari kuvuta subira katika suala hilo ambalo ufumbuzi wake utapatikana hivi karibuni.

Bw. Mungheiry alikiri kujitokeza kwa dosari katika suala la mishahara ya watumishi wa sekta ya afya wakiwamo madaktari bingwa katika hospitali mbali mbali za Unguja na Pemba.

Katibu wa Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar, Bw. Talib Mbwana, aliitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kulipatia ufumbuzi tatizo hilo haraka, ili kuepuka hasara zaidi, ikiwamo kukimbia kwa wataalamu hao kwa ajili ya kutafuta maslahi bora zaidi.

"Yapo malalamiko ya mishahara kwa watumishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar...tunaitaka Serikali kulipatia ufumbuzi wake haraka kabla ya kukimbiwa na wafanyakazi," alisema Bw. Talib.

SMZ imetangaza mishahara mipya kwa watumishi wake ambayo ilianza kulipwa mwezi huu, lakini kumejitokeza kasoro mbali mbali ikiwamo baadhi ya watumishi kupunjwa mishahara yao.

Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Omar Hassan, alikiri kupokea malalamiko ya baadhi ya watumishi mishahara yao kukosewa na kusema tatizo hilo linashughulikiwa.

Aliwataka wafanyakazi kuwa wastahimilivu sana katika kipindi hiki na kuongeza kuwa dosari zote zilizojitokeza, zitapatiwa ufumbuzi haraka.

Baadhi ya madaktari mishahara yao imepungua kutoka sh.200,000 hadi kufikia sh. 150,000.
Wakati huo huo, Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) itafanyiwa marekebisho makubwa kwa lengo la kuimarishwa na kuongeza wingi wa mapato yanayokusanywa.

Ofisa wa Mipango na Utawala wa ZRB, Bw. Ahmed Sadatti, amesema taasisi hiyo itafanyiwa marekebisho makubwa na kampuni ya Ernst and Young ya Uingereza yenye tawi lake Tanzania Bara.

Miongoni mwa marekebisho makubwa yatakayofanyika katika Bodi hiyo ni pamoja na kutolewa elimu kwa wafanyakazi wake ya jinsi ya kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza mapato.

"Hiyo ni moja ya mikakati mikubwa katika Bodi ya Mapato...kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato katika maeneo mbali mbali, ambapo utawafanya wafanyakazi wake kuwa wabunifu sana," alisema Bw. Sadatti.

Alisema katika mikakati hiyo, suala la maslahi bora kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo litazingatiwa, ili kuona wanapata maslahi bora na kufanya kazi vizuri na kuepuka vishawishi mbali mbali.

ZRB ni taasisi ambayo inajishughulisha na masuala ya ukusanyaji kodi za ndani za SMZ, huku ikiwa na ushirikiano wa karibu sana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo hukusanya kodi zilizopo chini ya Muungano.

ZRB imekuwa ikifanikiwa kuvuka malengo yake mwezi hadi mwezi ambapo kwa sasa inakusanya kodi ya sh. bilioni 3.6.

Some of them wamepata kutoka 200,000 hadi 150,000!
My take sijui ya mawaziri imeshuka kiasi gani
 
Hoja yako ya madktari wakimbie mimi naona ni dhaifu!

Namuunga mkono YNIM katika hilo. Kukimbia nje ya nchi ni moja ya suluhisho. Hii hoja si dhaifu hata kidogo. Ni uzalendo gani mnaotaka hawa wataalamu wa sekta ya afya waonyeshe wakati kuna wenzao wachache wanatumia mwamvuli huohuo wa uzalendo kujineemesha??? Kwa sababu tupo kwenye mfumo wa utandawazi na soko huria, waacheni hawa wataalamu watafute green pastures kokote kule katika hii planet.

Je waendelee kukimmbia nchi hadi lini na kwa faida ya nani?

Faida ni kwa hawa madaktari. Maana huko watakapokwenda watalipwa vizuri, watasaidia familia na ndugu wa karibu wanaowazunguka. Vilevile taifa linaweza kufaidika kwa kupata "remittance".

Kwa nini isirekebishwe wakae Visiwani wawahudumie Watanzania mliotuacha tunateseka mkakambilia ugenini?

Hilo ndilo la muhimu. Hakika hapo ndio kwenye kiini cha mgogoro. Wizara husika na serikali kwa ujumla wakae kitako kurekebisha mambo.
 
Back
Top Bottom