Misemo ya Mpoki jamani!

jamaa misemo mingi anaipataga kwenye nyimbo za Hip Hip
mfano utazunguka sana kutafuta mshkaki wenye mfupa. hiyo line iko kwenye ngoma ya Songa- ushauri wa bure
 
Alipokuwa MC ktk ile KSS mbele ya JK, alisema: "Nzi akiacha ujinga kidogo, atatengeneza asali!" Mbavu ziliniuma usiku ule, mpaka wife akanionea huruma!
Sasa nini cha maana kilikuchekesha hapo? Kweli wanaume nchi hii hatuna
 
hahahah...............tumbo linauma
kuna moja alisema ile tabia ya watu wa kigamboni wakishuka kutoka kwenye pantoni kukimbia baadaye watakuja kuwa wanariadha mahiri.................hafu hii ni kweli najiuliza sana kwanini uwa wanakimbia?
Kile kilima cha kupandish kutoka ktk pa nton kinachosha so wanakimbia kukimaliza mapema
 
Naona una kasumba ya wabongo kuchukia ukweli ama umehamua tu kuwa mbishi wa kuelewa vitu. Toka lini kusema ukweli kukawa ni tatizo ama kuponda kitu? Kuwa mzalendo si lazima upende hata upuuzi ila unatakiwa pia kukosoa kwa niaba ya wahusika na ndicho nilichokifanya, je kuna kosa? Unajuwa wewe na mimi tunaweza kuangalia kitu kwenye TV na tukawa na mawazo tofauti kabisa ya tulichokiona. Mimi naweza kufagilia tulichokiona wewe ukaponda na pengine sote tukawa hatuna point katika kusifia na ukosoaji wetu. Sasa nikuulize wewe Mpoki, kwa sisi kuwa na mawazo tofauti ya tulichokiona ni kukosa uzalendo ama? Ishu hapa ni kwamba ninashangazwa na acting ya Ze Comedy, kwangu haichekeshi hata kidogo kwani acting yao is pathetic to me. Umeelewa mpaka hapo ama nirudie? Na nikasema ninashangazwa na uchekeshaji wao kwani ni wa ngumbalu, maana ngumbalu ndipo unakuta jokes kama zile za Mpoki. Sasa hapa kosa ni lipi? Na nikaongeza kusema kwamba nafurahia series zingine za kibongo kama Mze Small na King Majuto pamoja na zingine kwani zinachekesha. Sikusifia sinema hata moja ya nje ya Tanzania, sijuwi mwenzangu umeona wapi hayo maneno niliyoandika wakati hayapo, ebu naomba uniambie. Usitoe vitu tu kwenye mawazo yako finyu na kusema fulani kasema wakati si kweli. Usiwe mvivu wa kusoma na kuelewa vitu, soma na uelewe ndipo utoe mada usikurupukie tu kujibu watu ili upate kuonekana kwenye quotes.
Mkuu, naona umeandika gazeti kubwa sana, binafsi yangu ni mara chache naweza kucheka nikitazama comedy za kitanzania, ni sababu yangu binafsi na makuzi yangu inabidi mtu atumie nishati ya kutosha ili kunichekesha, sasa kuna watu wanacheka na hawajilazimishi kufanya hivyo, mpoki au comedian hawakuumbwa kuchekesha watu wote, sasa ninakushangaa unavyowashangaa watu wanaofurahia comedy ya mpoki! sasa kwa kuwa mpoki ajakidhi vigezo vyangu na vyako ili tucheke ndio tumwone kila mtu anayecheka kuwa anajichekesha? eti unashangaa wabongo wanavyocheka! are you seriously? basi soma coments humu ndani, inaonyesha more than 90% ya wachangiaji wana muelekeo wa kukubali kazi ya mpoki, unahisi wamekosea.. usilazimishe kila mtu akawaza au akapokea kitu kama unavyokipokea wewe,
 
Na hiki ni kicheko? There are some jokes that make you laugh ila tusilazimishe kuchekeshana jamani. Ze Comedy wanahitaji msaada wa kuchekesha.
mkuu sijajua ushamba wako umefikia uzito kiasi gani, kuna kipimo chochote cha kitu au neno kuwa kichekesho? kwa comedian anaweza kuongea neno la kawaida lakini watu wakacheka kutokana na uwasilishwaji wa neno hilo? anaweza akalitaja jina lako tu watu wakacheka, na comedian kuna level anafika watu wakimuona tu anafanya shoping wanaanza kucheka, ndio maana nakuuliza unaijua comedy? maana unashanaa neno kwa kuwa halichekeshi as if mpoki anafanya comedy ya kuandika kwenye gazeti.
 
mwajuma ndala ndefu....ng`ombe anakula nyasi za kijani lakini maziwa meupe
 
Siishi Bongo ila kwa sasa nipo hapa huu mwezi wa tatu nakaribia kuondoka tena. Ninajaribu sana kuelewa ni nini haswa watu wanacheka kwenye ze comedy. Kiukweli hata acting yao is pathetic. Siyo kama nakandia ze comedy (maana mtanzania mkimwambia ukweli anadhani unakandia), ila jamaa hawana ishu. Mbona nina enjoy drama series nyingi tu za kibongo na hata comedi za king majuto na mze small zinafurahisha shinda hata hawa ze comedy. Tatizo siyo kuishi nje, ila sioni uchekeshaji wao, ni wa kitoto mno dizaini ya ngumbalu.
ukipwendwa na wote utakuwa mnafiki ww usiwakubali wa kuwasapoti ze comedy tuachie wenyewe
 
Sikumbiki vizuri. .huwa anasema kama kuoga usafi kwanini unafua taulo. .
 
Hahahaha mpoki bwana kuna posti ililetwa uku eti alitaka kugombea ubunge wa kigamboni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom