Misemo na Maneno ya zamani

GARBAGE-mwanamke

Hii ya miaka ipi jamani?

Haya nami niongeze machache:
Mchiki - msichana
goma - mwanaume
kuua nyuki - ku curl nywele
mnaa - mnoko - mkali
mshua- mtu wa hali ya juu (status)
Dingi - baba
**** - mjinga
kilaza- mjinga hasa kielimu
ghetto -
njagu - polisi
kula kobis - kujikausha
wagrovesu - wakulima
 
nimekumbuka hili neno/jina kamanyola hivi lina maana gani
Kamanyola lilikuwa ni jina la kikosi cha jeshi huko Zaire (wakati huo). Lakini kwa hapa kwetu TZ ilikuwa ni mtindo wa dansi wa bendi moja hivi (jina limenitoka). Wengine waliwaita wana-kamanyola. Huo ndio uelewa wangu. Kama kuna maana nyingine, wanaJF watasema.
 
Binti mrembo: super kibao, ngushi
Siasa: kabaila, kupe, mnyonyaji, mabwanyenye
Tabia: msela, mchizi, chekiyee, kwenda kibega, makalubandika
Mavazi: njiwa, maksi, dengrizi, buga, pekosi, coast
Matendo: shakila, dobi, sokomoko, songombingo
 
Bwana Ndugu,
ukipenda maneno ya kale nachangia vipimo asilia kadhaa vya Kiswahili:
frasila, morta, ratili, shubiri, wanda, ziraa

Sijui kama bado vinaeleweka?
 
Wanajamii tujikumbushe baadhi ya misemo ambayo zamani ilikuwa kwenye chati na sasa haitumiki tena..

Kwa mfano nakumbuka misemo kama kuachwa kwenye mataa, Viatu vya Ndula, lakuchumpa n.k, Pia nakumbuka majina kama Chekibobu.

Karibuni.
mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba.huu msemo naupenda sana
 
wanajamii tujikumbushe baadhi ya misemo ambayo zamani ilikuwa kwenye chati na sasa haitumiki tena..

Kwa mfano nakumbuka misemo kama kuachwa kwenye mataa, viatu vya ndula, lakuchumpa n.k, pia nakumbuka majina kama chekibobu.

Karibuni.
ada ya mja ni kunena muungwana vitendo
 
Kamanyola lilikuwa ni jina la kikosi cha jeshi huko Zaire (wakati huo). Lakini kwa hapa kwetu TZ ilikuwa ni mtindo wa dansi wa bendi moja hivi (jina limenitoka). Wengine waliwaita wana-kamanyola. Huo ndio uelewa wangu. Kama kuna maana nyingine, wanaJF watasema.

Maquiz du Zaire enzi za King Kiki (mtindo wa Kamanyola bila jasho)
 
hahah umefikiria nini mpaka kukumbuka haya maneno yote?? watu wabunifu humu ndani. asanteni sana kwa kutukumbusha.
 
Tuna imani na Nyerere hoya hoya hoya,
ooo Tanu yajenga nchi,ooo Tanu yajenga nchi,
Zidumu fikra za Mwalimu Nyerere,
Wako wapii walio wakali sana,sisi twawataka,
Kule kule kwa Chinova,kule kule kule kwa Chinovu,
Baba Paka akasema twendeni kuwinda Paka etc etc etc ongezeni nyingine vijana wa zamani!
 
Mambo mchafukoge,
varangati
mkuda
duniamsongamano
gwala, masai, dala (fedha)
kosovo
kidosho
 
Wanajamii tujikumbushe baadhi ya misemo ambayo zamani ilikuwa kwenye chati na sasa haitumiki tena..

Kwa mfano nakumbuka misemo kama kuachwa kwenye mataa, Viatu vya Ndula, lakuchumpa n.k, Pia nakumbuka majina kama Chekibobu.

Karibuni.

msinikumbushe zile enzi za kujikata kisilesi, kuyakata mangoma, vishtobe, kuruka debe, kuyeya na maneno mengine kibwena
 
Wanajamii tujikumbushe baadhi ya misemo ambayo zamani ilikuwa kwenye chati na sasa haitumiki tena..

Kwa mfano nakumbuka misemo kama kuachwa kwenye mataa, Viatu vya Ndula, lakuchumpa n.k, Pia nakumbuka majina kama Chekibobu.

Karibuni.

maneno haya hakika yamenikumbusha mbali kwa kuchangia acha niyatumie machache katika kutengeneza kijistori.

safari ya kuelekea debe ilifika,nilichukua dodoki na sabuni yangu ya mbunju na kwenda kuoga,nilivaa pensi nyanya langu na kijasti bikozi chini lakuchumpa lakuparama nililotumiwa toka mamtoni nikampitia gangwe mwenzangu aliyevalia shati la bahama pembeni alikuwa na kishtobe wake ambaye kichwani aliweka zazuu chini alivalia kokoko na gauni la marinda, tukachum zetu kwenda kuruka majoka.
 
We mwenyewe utabakia mkufu........ yaani unaachwa hoi
mie homaa ....... yaani unaachwa umeduwaa
Kafa Ulaya - Mazishi Africa - Mitumba ilipoanza kuingia
chachacha - viatu vifupi hasa vya kuchezea break dance
 
Back
Top Bottom