Misamiati Mipya ya Kiswahili

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Katika gazeti la RAI la Jana (09/08/2012) katika maoni kulikuwa na misamiati mipya ya kiswahili. Misamiati hiyo ni:
  1. ICU (intesive care unit) = SADARUKI.
  2. Serikali ya Mseto (coalition government) = SERIKALI MAHUTUTI.
  3. Viumbe vyenye JINSI zote mbili (Me na Ke) = HUNTHA (wingi ni mahuntha)

WanaJF nimeona niwaletee misamiati hiyo ili muanze kuitumia kwa nia ya kukienzi Kiswahili chetu. @Erotica kwa vile siku hizi kisu imekuwa njia maarufu ya kujifungua, ukitoa katika chumba cha upasuaji utapelekwa Sadaruki (usiseme ICU).

Ndimi Bazazi!
 
Hilo huntha [Khuntha] ninalitumia katika mazungumzo ya kawaida

[Serikali mahututi].....sidhani kama ni Kiswahili sanifu
 
Hilo laweza kuwa kweli.

Lakini serikali mahututi haiwezi kutumika kama mbadala wa serikali ya mseto kama ilivyoanishwa na mtoa mada
In the first place, kuna shida gani na neno SERIKALI YA MSETO? mbona ni clear?
Mi naona kuna maneno yanayohitaji zaidi kiswahili kama CPU, REDIO,GARI, BAISKELI etc!
Nasikia wenzetu Wanigeria walipooma baiskeli kwa mara ya kwanza waliita "Iron Horse"!.. at least inaleta sense!
 
Katika gazeti la RAI la Jana (09/08/2012) katika maoni kulikuwa na misamiati mipya ya kiswahili. Misamiati hiyo ni:
  1. ICU (intesive care unit) = SADARUKI.
  2. Serikali ya Mseto (coalition government) = SERIKALI MAHUTUTI.
  3. Viumbe vyenye JINSI zote mbili (Me na Ke) = HUNTHA (wingi ni mahuntha)
WanaJF nimeona niwaletee misamiati hiyo ili muanze kuitumia kwa nia ya kukienzi Kiswahili chetu. Erotica kwa vile siku hizi kisu imekuwa njia maarufu ya kujifungua, ukitoa katika chumba cha upasuaji utapelekwa Sadaruki (usiseme ICU).

Ndimi Bazazi!

We need the etymology of these new words. Words do not come from ones invention from nowhere
 
Last edited by a moderator:
Viumbe vyenye JINSI zote mbili (Me na Ke) = HUNTHA (wingi ni mahuntha)

Kwa hiyo unatujulisha kuwa ww ni Huntha! Unatangaza biashara....

Kweli ww Bazazi......kuna siku nitaku bazazuwa
 
In the first place, kuna shida gani na neno SERIKALI YA MSETO? mbona ni clear?
Mi naona kuna maneno yanayohitaji zaidi kiswahili kama CPU, REDIO,GARI, BAISKELI etc!
Nasikia wenzetu Wanigeria walipooma baiskeli kwa mara ya kwanza waliita "Iron Horse"!.. at least inaleta sense!
iron horse - noun Older Use .a locomotive. (archaic a steam-driven railway locomotive) Origin: 1825–35

Hongera kwa kuendeleza Lugha ya kiswahili,lakini neno SERIKALI MAHUTUTIsioni mantiki ya kutumika kama mbadala ya neno SERIKALI YA MSETO.
 
Siyo serikali "mahututi". Ni serikali "mahuluti". Kama waliandika serikali 'mahututi' basi walikosea tu tahajia kwa sababu "mahututi" na "mahuluti" tahajia zake zimepishana herufi moja tu.

Kwa hiyo serikali "mahuluti" ni Kiswahili sanifu kabisa.
 
Mkuu Ngabu, tatizo la hawa wapya ni kutokusoma uzi wote. The #1 post is enough for them. Baada ya hapo anarusha tu bandiko lake.Thanks for correction and elaboration.
 
Siyo serikali "mahututi". Ni serikali "mahuluti". Kama waliandika serikali 'mahututi' basi walikosea tu tahajia kwa sababu "mahututi" na "mahuluti" tahajia zake zimepishana herufi moja tu.

Kwa hiyo serikali "mahuluti" ni Kiswahili sanifu kabisa.
Katika maneno hayo mawili, 'mahututi' na 'mahuluti', fonimu 't' na 'l' ni mofimu kwa sababu ndizo zilizosababisha tofauti ya maana. Ni muhimu sana, kwa mantiki hiyo basi, kila mara tunapoandika msamiati tujiridhishe na otografia husika kuepusha uwezekano wa kupotosha wafuatiliaji wa nyuzi zetu. Hata hivyo tunamshukuru mleta uzi na mchango ulioutoa kwa wanajamvi wengine.
 
Sijakuelewa hata kidogo. Ni nani kapotosha wafuatiliaji wa nyuzi hapa?
 
Nyani Ngabu nakuhakikishia kuwa sikupata kiwi ya macho kiasi cha kutoelewa mchango wako kuntu juu ya mada iliyoko jamvini. Ukisoma michango ya wachangiaji wengine ni lazima utamaizi nililolisema.
 
Back
Top Bottom