Misamiati maarufu vyuo vikuu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
1.'Boom'(fedha za kujikimu zitolewazo na Bodi ya Mikopo ya Elimu Ya Juu kwa wanachuo/wanafunzi)
2. 'Kuuza chai'(Kupiga stori hasa za kuchekesha/au sizizo za kweli)
3.'Nyanga'(Supplementary exams)
4.Kutiwa nyavuni/kukamatwa(kufeli somo hivyo kutakiwa kulirudia)
5.Nondo(vitu visivyoruhusiwa mtihanini lakini vinavyoingizwa kimagendo)
6.Exile(kumpisha mwanachumba mwenzako 'atumie' chumba pekeyake kwa muda fulani
7.'Kupiga Dash'(kushinda bila kula kwasababu ya kuishiwa fedha za kujikimu)
8.Kipanga(mwanafunzi anayejiweza darasani kwa kuelewa haraka au kutosahau haraka)
9.Kilaza(mwanafunzi ambaye uelewa wake ni wa mashaka/haelewi mapema na hachelewi kusahau)
10.'Ungwini'(Masomo ambayo hayaambatani na mahesabu)
11.'Kudesa'(kuiga kwa mwanafunzi mwingine au kuandika kitu kama kilivyokutwa mahali fulani au kwa mtu fulani)
12.'Desa'/'Madesa'(Kitabu/Vitabu visivyo rasmi

Wana JF tuendelee...
 
Kudownload maji-Kuchemsha maji.
Mara ya kwanza niliachwa kwenye mataa niliposikia mtu anakunywa maji ya kudownload.
 
Back
Top Bottom