Misafara ya viongozi nje kupungua

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Misafara ya viongozi nje kupungua

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 18th June 2009 @ 14:02 Habari Leo

Rais Jakaya Kikwete ameagiza kuangaliwa upya kwa idadi ya watu wanaosafiri na Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu nje ya nchi ili kupunguza gharama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe leo amekiri bungeni mjini Dodoma kuwa, misafara ya viongozi nje ya nchi inatumika fedha nyingi.

Waziri Membe amelieleza Bunge kuwa, baada ya muda, kutakuwa na idadi maalum ya watu watakaosafiri nje na viongozi hao. Kwa mujibu wa Membe, katika bajeti ya mwaka wa sasa wa fedha, bunge liliidhinisha sh bilioni nane kwa ajili ya safari za viongozi nje ya nchi.

Mwanadiplomasia huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhonga Ruhwanya aliyetaka kufahamu kuna mpango gani wa kupunguza ukubwa wa misafara ya viongozi ili kupunguza gharama.

Awali, Mbunge wa Viti Maalum, Zulekha Yunus Haji alitaka kufahamu ni utaratibu gani unatumika kuwachagua viongozi wanaofuatana na Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu wanapofanya ziara nje ya nchi.

Membe amesema, utaratibu wa kuchagua nani afuatane na viongozi hao nje huzingatia vigezo kadhaa likiwamo suala la kusudio na madhumuni ya safari hizo, jinsia, uwakilishi wa pande zote za muungano na uwakikilishi kutoka Kambi ya Upinzani.

Kwa mujibu wa Membe, ofisi za viongozi hao kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa upande wa Zanzibar na ofisi ya Spika wa Bunge kwa upande wa wangunge ndiyo wanaoteua watu wa kusafiri na viongozi wa kitaifa.

"Kila wakati viongozi wakuu wanaposafiri nje ya nchi waandishi wa habari wamekuwa wakijumuishwa katika misafara hiyo. Inapotokea kuwa viongozi wamekaribishwa kutembelea nchi jirani, basi wakuu wa mikoa inayopakana na nchi hizo huteuliwa kufuatana na viongozi hao" amesema Waziri Membe.

Membe amesema, kwa kuzingatia vigezo hivyo, makundi ya viongozi yanayofuatana na viongozi wakuu wa nchi ni mawaziri mbalimbali kutoka pande za muungano, wabunge wa Bunge la Muungano, watendaji kutoka idara za serikali kwa kuzingatia madhumuni ya ziara hizo.

Amesema, ukiacha viongozi hao, wengine wanaosafiri na viongozi hao kwa kuzingatia itifaki ni maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na wapambe wa viongozi hao.
 
Good, it is high time. Wakati wa BWM nasikia alikuwa anaitisha manifest kabla ya kwenda nje ya nchi kwa madhumuni ya ku-filter wale ambao alidhani hawastahili kusafiri nae. Hapa linakuja pia swala la ndege ya rais, alikuwa anapendelea kuitumia ndege hiyo kusafiri nje ya nchi, na nasikia ndege hiyo inaweza kusafiri masafa marefu bila kujaza mafuta. It is more economical rais akitumia ndege yake baadala ya kutumia commercial airlines akiwa ziarani majuu na itasaidia kuwachuja wale vimbele mbele wanaojipenyeza kwenye misafara hiyo.
 
Misafara ya viongozi nje kupungua

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 18th June 2009 @ 14:02 Habari Leo

Rais Jakaya Kikwete ameagiza kuangaliwa upya kwa idadi ya watu wanaosafiri na Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu nje ya nchi ili kupunguza gharama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe leo amekiri bungeni mjini Dodoma kuwa, misafara ya viongozi nje ya nchi inatumika fedha nyingi.

Waziri Membe amelieleza Bunge kuwa, baada ya muda, kutakuwa na idadi maalum ya watu watakaosafiri nje na viongozi hao. Kwa mujibu wa Membe, katika bajeti ya mwaka wa sasa wa fedha, bunge liliidhinisha sh bilioni nane kwa ajili ya safari za viongozi nje ya nchi.

Mwanadiplomasia huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhonga Ruhwanya aliyetaka kufahamu kuna mpango gani wa kupunguza ukubwa wa misafara ya viongozi ili kupunguza gharama.

Awali, Mbunge wa Viti Maalum, Zulekha Yunus Haji alitaka kufahamu ni utaratibu gani unatumika kuwachagua viongozi wanaofuatana na Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu wanapofanya ziara nje ya nchi.

Membe amesema, utaratibu wa kuchagua nani afuatane na viongozi hao nje huzingatia vigezo kadhaa likiwamo suala la kusudio na madhumuni ya safari hizo, jinsia, uwakilishi wa pande zote za muungano na uwakikilishi kutoka Kambi ya Upinzani.

Kwa mujibu wa Membe, ofisi za viongozi hao kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa upande wa Zanzibar na ofisi ya Spika wa Bunge kwa upande wa wangunge ndiyo wanaoteua watu wa kusafiri na viongozi wa kitaifa.

"Kila wakati viongozi wakuu wanaposafiri nje ya nchi waandishi wa habari wamekuwa wakijumuishwa katika misafara hiyo. Inapotokea kuwa viongozi wamekaribishwa kutembelea nchi jirani, basi wakuu wa mikoa inayopakana na nchi hizo huteuliwa kufuatana na viongozi hao" amesema Waziri Membe.

Membe amesema, kwa kuzingatia vigezo hivyo, makundi ya viongozi yanayofuatana na viongozi wakuu wa nchi ni mawaziri mbalimbali kutoka pande za muungano, wabunge wa Bunge la Muungano, watendaji kutoka idara za serikali kwa kuzingatia madhumuni ya ziara hizo.

Amesema, ukiacha viongozi hao, wengine wanaosafiri na viongozi hao kwa kuzingatia itifaki ni maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na wapambe wa viongozi hao.

This is really nonsensical, folly and shameful if the Government operated, from time immemorial, without a policy but the discretion of President, and perhaps bankrolled by cronies benefiting from foreign trips!
A perfect reason for endemic underdevelopment!
Pole watanzania. Mmevumilia vya kutosha kuongozwa na wasiiona, si kwa macho, bali kwa 'vichwa' vyao!
 
Bubu, tangu jana nina tuma post kuchangia post zako lakini sizioni, i think kuna shida somewhere.
 
Back
Top Bottom