Misaada kwa waathirika wa mabomu au kujitangaza kibiashara na kisiasa?

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,506
2,409
Nimeona kampuni, taasisi na asasi mbalimbali zikitoa misaada ya kiutu kwa wahanga mabomu Gongo la Mboto kwa staili ya kujitangaza na kujinadi zaidi. Nimeona pia WANASIASA wetu na wake zao wakiende kutembelea sehemu zilizoathirika na mabomu haya sanjari na wagonjwa waliolazwa mahospitalini kwa kujitangaza na kujinadi zaidi.
Nilidhani misaada pamoja na kuona wagonjwa lilikuwa halihitaji kuandamana na Televisheni na vyombo vingine vya habari. Nilitarajia hatua zitakazochukuliwa kuzuia majanga kama haya yasitokee tena ndizo tungearifiwa kwa kina. Tungefurahi zaidi kuona hatua zinazochukuliwa kama kuna uzembe, uvivu na kutojali kwa baadhi ya tuliowakabidhi majukumu haya.
Tunatumia majanga kama haya kujinufaisha kibiashara na kisiasa? Watanzania wapi tunakoelekea?
 
Misaada na kujitangaza vyote wanavifanya kwa pamojai.e wanaua ndege 2 kwa jiwe moja..............wana si-hasa,makmpuni,taasisi n.k
 
kwa kweli inasikitisha sana. Ni kama vile 'watu hao' walikuwa 'wanaombea' haya yatokee ili wapate nafasi ya kujionesha.
 
kwa kweli inasikitisha sana. Ni kama vile 'watu hao' walikuwa 'wanaombea' haya yatokee ili wapate nafasi ya kujionesha.

Halafu misaada yenyewe uratibu mzuri haina. Ingechaguliwa taasisi moja yenye uzoefu na mambo haya kama Chama cha Msalaba Mwekundu sisi wengine tukapeleka misaada hiyo huko. Misaada kama hii ni kama zaka na sadaka haipaswi kutolewa kwa kujinadi.
 
wafanyabiashara wapo kwa ajili ya faida tuu ni sivinginevyo, wakitoa msaada bila kujitangaza unadhani soko la bidhaa zao litakuwaje????? shida zetu faida kwaoo,,, halaaaaaaaaa
 
Halafu misaada yenyewe uratibu mzuri haina. Ingechaguliwa taasisi moja yenye uzoefu na mambo haya kama Chama cha Msalaba Mwekundu sisi wengine tukapeleka misaada hiyo huko. Misaada kama hii ni kama zaka na sadaka haipaswi kutolewa kwa kujinadi.

Naunga mkono maoni yako kwa 100%! Uratibu wa misaada kwa waathirika wa majanga unapaswa kuendeshwa na watu wenye uzoefu katika majanga kama hao uliotaja, Caritas, UNHCR n.k. Hili suala la kila mwenye 'kamsaada' anataka kwenda mwenyewe uwanja wa taifa ama Gongolamboto ni upuuzi. Halafu unakuta misaada yenyewe ni juisi za shilingi 200 katoni kumi ama katoni tano.
 
Back
Top Bottom