Viongozi wa mwanzo wa Taifa la Tanzania kote Tanganyika na Zanzibar hawawezi kupuuzwa kuwa hawakuwa na moyo wa dhati kuanzisha miradi mikubwa iliyo na nia thabiti ya kunufaisha Watanzania.
Kwa leo mimi naanza na mradi wa reli ya TAZARA ambayo Mwalimu Nyerere na Abdulrahman Babu walipitia mitihani migumu ya 'nchi rafiki kama USA, RUSSIA, CANADA, IMF' kukataa kutoa msaada kwa ujenzi wa reli hiyo.
Lakini kutokana na mikakati na ufahamu mkubwa wa viongozi wetu, Mwl. Nyerere na waziri wake Abdulrahman Babu pamoja na Rais wa Zambia Kenneth Kaunda waliweza kuishawishi China ya Mao Dze Tung na Chou En Lai kufadhili ujenzi wa mradi huo mkubwa kabisa wa kihistoria.
Miradi mingine mikubwa iliyotekelezwa ni ya mabwawa ya nishati ya umeme n.k ambavyo mpaka leo tunavitumia. 'Sijui' viongozi wa sasa ni miradi gani mikubwa ya kutambulika iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2000 itakumbukwa miaka 40 ijayo, yaani mwaka 2050?!
London School of Economics wanachambua ushirikiano wa China na nchi kama Tanzania na Zambia kipindi cha 'Cold War' Video clip http://www.youtube.com/watch?v=Z0IZV4cplDM&feature=related hii inatupatia historia ktk dakika 3:59 za changamoto kutoka kona mbalimbali za ulimwengu kujaribu kuhujumu mradi huo wa TAZARA hata kabla haujaanza ikiwemo South Africa chini ya utawala wa kibaguzi (apartheid).