Miongoni mwa mambo yanayomkera mwanamke!

Yaani nimecheka hadi basi! Hapa ninapoishi kuna mwanaume mmoja alikuwa anamtongoza binti mmoja ambaye yuko sekondari form 5 anamkataa. Mwanaume alikuwa akijisifia pesa, mali na kutoa ahadi kem kem lakini binti hakujali kabisa. Siku moja aliendelea na kumbembeleza huyo binti bila mafanikio yoyote na binti alitishia kumwambia mkewe(yaani huyo jamaa ameoa). Jamaa akajivuta pembeni kidogo, simu yake kubwa ya kichina akaiweka sikioni akajifanya anaongea na mtu. "halo, kama nilivyokwambia, uniletee milioni 3 tu, zingine 11 uniwekee benki" "halafu hivi ule mzigo mliokusanya unatosha SCANIA moja? Haya kesho pakia...." Wakati mwanaume huyo akiendelea na maongezi yake feki simu yake ikaita kwa sauti kubwa!Huyo binti alicheka, hakuwa na mbavu. Yeye yuko "hii simu yangu sijui vipi? mimi naongea na mtu yenyewe inaita! itakuwa na matatizo.
 
Bila kuambiwa hivyo hamuelewi somo....
Hiyo njia inatumika sana kwa sababu inaonekana wanaume wanafanikiwa sana kuwapata wale wanaovutiwa nao..
Kuna mmoja nilimsikia katika daladala anaongea na binti kwa simu..........oooh naelekea eapoti hivi sasa naenda Uholanzi, kupitia J'berg, Dubai. baada ya wiki tatu unitafute nitakuwa nimerudi. Jamaa mwenyewe kapanda daladala ya Ubungo Kibamba, anaelekea kibamba usiku...

hahaah hii kali.
 
Kuna mshikaji alikuwa na apointment na dada mmoja alipofika eneo la tukio jamaa akaanza kuonyesha funguo za gari demu akasepa
 
Back
Top Bottom