Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Jamani wadau naomba na mimi niingie jamvini nichangie huu mjadala,japo nawaomba mnielewe sana kwa tafakuri jadidi ya kile nitakachoeleza.
Kwanza kabisa nakuomba mkuu kubwa jinga utoe hiyo picha hapo,yaani picha uloitumia inayomwonesha lowasa hapo kwani true reflection yake inatafsiriwa kama defamation(slander) kwa huyo jamaa,usije ieletea jf matatizo bure.Labda ukitaka kukwepa liability tafuta kikatuni chake lakini sio pseudomatic photo kama hiyo.Anyway huu ni ushauri tu.
Pili,mimi nimebahatika kusoma na huyu bwana Ridhwani high school na pia university kwenye faculty moja huku tukifukuzana madarasa.Kuhusu ufisadi naomba niiri wazi kwamba kwa huyu kijana siujui,ila nachofahamu kwake ni kwamba ni mtu asiye na makuu anayeweza kuinteract na mtu yeyote yule.Hata alipokuwa mkwwa ni watu wachache sana waliojua ni mtoto wa jk waziri wa mambo ya nchi za nje.Tulijua tu kwa kuwa alikuwa anafanana naye na jina la ubini wake.Sote tulikula DH na hakutumia cheo chake.Ila cha ajabu wale waliojua ukweli kuhusu yeye walikuwa wanajitahidi kujipendekeza sana wakati yeye hana mpango.Sawa navyomjua wakati huo labda sio sasa kwani watu wanabadilika.
Kumbuka kuwa hata Mkapa naye alikuwa na sifa karibu hizi zote kabla hajaanza kufanya kazi ikulu.
Vivyo hivyo alipokuja mlimani kitivo cha sheria hakubadilika bado aliendelea kuwa social na mtu asiye mjivuni,kila mtu alimahamu na hadi alipewa ungozi kuwa mwenyekiti wa kitivo cha sheria kwa tiketi ya daruso.Kama kawaida cha ajbu hapa kuna watu walijikomba sana na kujitafutia sifa toka kwake lakini yeye hakujali,akiwamo rais wa daruso wa wakati huo aliyeamua kumpa uwaziri wa mambo ya nchi za nje wa daruso ili afanane na baba yake.Wakina beno malisa wanajua jinsi walivyohusiana na ridhwani.
Kuhusu uwezo wake kimasomo,si kweli kwamba alikuwa na uwezo mkubwa sana kama masha anavyodai.Alikuwa na uwezo wa kawaida tena naweza kusema ni wa chini,kwani supp alikuwa nazo kadhaa hivyo kufanya GPA yake isiwe ya kutisha sana.Hata hivyo kuefli mitihani au kuwa na uwezo fulani ni kitu cha kawaida tu kwa mwanafunzi kwani uwezo wa mtu hautegemei yeye ni mtoto wa nani.Nachojua mimi IMMA huchukua watu cream sana.Tena ukiomba internship pale mnapigwa hadi pepa ikiwa ni pamoja na wao kuomba matokeo toka kitivo cha sheria.Bahati nzuri niliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya faculty inayopitisha matokeo hivyo suala la matokeo si geni kwangu.IMMA mara nyingi huchukua watu wenye first class na wakiwakosa sana sana watawachukua wenye upper second ya point 3.7 mwisho.Na wakikosa kabisa huchukua waganda kwani wao kiingereza kinawasaidia kuwaondosha watanzania kwenye kinyang'anyiro.Ridhwani hakuwa na first wala second class upper na wala kiingereza hajui sana tena alikuwa anababaisha tu hadi tunacheka kwenye vikao vya bodi.Hili nalo si tatizo kwani wengi pia hatujui,tunabwabwaja tu,lakini alichukuliwa IMMA.Vigezo walivyomchukulia wao wenyewe wanavijua na havikofixed wanaweza kuvubadili hivyo sitawaingilia sana huko.Sasa kama navyosema aliyejipendekeza hapa huenda ni hao jamaa lakini sio bwana mdogo,kwani wao huenda azma ya baba yake walikuwa wakiijua mapemaaaaaaa.
Hili swali la jinsi alivyoingia IMMA na jinsi alivyowapita wenzie ni kubwa lakini kwangu sio big deal sana hapa.
Kuhusu wanasheria jamaani,hapa mtajadili wee lakini tutajadili kitu ambacho hatukifahamu.Mwanasheria anaruhusiwa kumtetea mtu yeyote hata kama amekiri mbele yake kwamba kweli aliua na hata kama alimwona akiua ili mradi mwanasheria huyo hakuitwa kama shahidi mahakamani.Vilevile hata kama kampuni ni ya kifisadi au vinginevyo,bado ina haki ya kutetewa kisheria na kupata egal services zote,kwani izo huwa ni tuhuma zisizothibitishwa.Na kwa tanzania hatuna sheria inayomkataza wakili kumtetea au kuisajili kampuni yeyote ile,kwani kanuni ya kisheria inayotawala biashara inasema "buyer be ware" caveat emptor hivyo wewe unayeingia makataba na mwizi ndio unatakiwa kuwa makini,kwani kampuni kama richmond inapokuja tanzania,ni vigumu mwanasheria kujua itakuwa ya kitapeli au la,yeye anaisaidia usajili anapokea mkwanja wake basi mkataba na hiyo kampuni inaisha.Ni kazi ya wanasheria wa serikali kuchunguza mtu wanayeingia naye mkataba.
Hakuna makosa kwa wanasheria kutetea wauaji. Wanasheria wanakuwa na matatizo pale ambapo wao wanapokuwa wahusika wa crime (kumbuka wanasheria wa Nixon).
Hivyo basi sheria zinazotawala uwakili tanzania ni moja au mbili tu, ADVOCATES ACT na Tanganyika law society Act.Wanasheria wanabanwa na professional ethics ambazo kwa ufupi zinawakataza wasijitangaze,na ndio maana huoni matangazo yao redioni,au kwenye bill boards,wasiende kusolicit biashra yaani wasijipigie debe ama kupigiwa debe(tauting) wala wasiingie njama na mteja kumdhuru mteja mwingine (champerty) na vilevile kanuni kama vile kuvaa suti,joho kuheshimu mahakama n.k ndizo zinazowabana.Na mwisho na kubwa sana ni rule agaisnt conflict of interests. Kwa mana ya kwamba mwanasheria huwezi kuwatetea wateja wawili wanaopingana,huwezi leo ukaisajili richmond afu kesho ukawa unaishtaki au unahusika katika uchunguzi wake.Wala huwezi kutengeneza mkataba fulani halafu kesho wewe mwenyewe unakuwa wakili wa upande mwingine unaopinga makataba huo huo.Au kama masha huwezi kuwa waziri wa mambo ya ndani halafu idar yako ya polisi inaichunguza deep green ambayo wewe ulihusika kuisajili.Unatakiwa uachie ngazi kumoja ili uruhusu uchunguzi huru kwingine.
Kutokana na mwanga wa maelezo haya,sasa nadhani tunaweza kuona kuna upungufunupi katika sheria za mawakili na maadili yao,suala zima la ridhwani na mambo mengine yanayohusiana na sula hili,maswali maoni welcome
Hapa maswali machache tu yanatakiwa kujibiwa. Ni nini uhusika wa IMMA kwa Tangold na Deep Green? Kwa nini Kikwete hataki uchunguzi huru ufanyike?