Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,854
Mimi naona Mheshimiwa anaikuza ishu! Ile ni kampuni binafsi na it is nobody's business nani wanayemuajiri au kumpa upartner. Pamoja na kusema hivyo ni kuwafanya watanzania wapumbafu kudai kuwa nafasi za wazazi wa huyu kijana na yule dada hazikuingia kwenye mahesabu wakati wa kuwaajiri/kuwafanya partners! Wao kama wafanya biashara wangekuwa wajinga kutokufanya hivyo. Si kila kitu kinategemea performance, ni utaleta nini kwa kampuni. Kama kuwepo kwako kutawafungulia milango kwa nini wasikuajiri hata kama kuna wengine ni vichwa kuliko wewe? Ndiyo biashara, ndiyo ukweli. No shame in it! Sasa kama walitumia kuwepo kwa hao vijana kwa kujifaidisha baadaye, hilo ni suala lingine.