Minister belittles link with JK's son

Masha hana njaa ya hela kazaliwa kwao zipo, kusema ni kijana mh huo upara je si wautu uzima kweli! huyu ni mkomavu wa uongozi na anastahiki kuwepo alipo. Kwenye vikao vya madiwani hupenda kumwita wakili masha, ni mtu mkweli makini na mahiri.

Ushauri wangu kwake awaachie maPR kujibu hoja uchwara, yeye achape kazi tu, tunajua anakazi kubwa ya kuandaa vitambulisho vya kitaifa.
 
Hii hapa habari yenyewe waungwana:
Kashfa ya ufisadi Waziri amtetea mtoto wa Kikwete

Habari Zinazoshabihiana
• 'Baadhi ya wabunge CCM wanafiki' 23.01.2008 [Soma]
• Bodi ya BoT yatakiwa kurejesha imani 22.01.2008 [Soma]
• ...Wapinzani kuandamana Dar 19.01.2007 [Soma]

*'Magaidi' ziara ya Bush waachiwa

Na Gladness Mboma na Eben-Ezery Mende

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Bw. Laurence Masha ameibuka na kumtetea mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Bw. Ridhiwani Kikwete kufuatia kuhusishwa kwake na ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na ajira yake.

Kuhusishwa kwa Bw. Ridhiwani kumekuja baada ya gazeti moja (sio Majira ), kudai mtoto huyo ameajiriwa na anafanya kazi kwenye kampuni inayodaiwa kushiriki kusajili Kampuni ya Deep Green Finance Ltd ( DGF) inayotuhumiwa kukwapua mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Gazeti hilo linalotolewa kila wiki, lilidai kuwa na taarifa kwamba Kampuni ya Mawakili ya IMMA Advocates and Co. anayofanya kazi Bw. Ridhiwani, ndio ilisadia usajili wa DGF inayotuhumiwa kuchota sh. bilioni 8 kutoka BoT.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Masha alisema alishtushwa na taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo na kumhusisha Bw. Ridhiwani na ufisadi wa BoT.

Akifafanua jambo hilo,Bw. Masha alisema wakati akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya DGF inayousishwa na ufisadi huo, walikuwa na utaratibu wa kuchukua wanafunzi wa mazoezi katika fani ya sheria kila mwaka.

"Wanafunzi walioonekana wanafanya vizuri katika mazoezi kampuni ilikuwa ikiwaajiri watano kila mwaka, ambapo Bw. Ridhiwani ni miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri na kuajiriwa na kampuni hiyo,"alisema Bw. Masha.

Alisema kuajiriwa kwa Bw. Ridhiwani kulifanyika wakati Baba yake ( Rais Kikwete) hajawa Rais na wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Bw. Masha aliongeza kuwa wakati Bw. Ridhiwani anajiriwa katika kampuni hiyo, Baba yake alikuwa hajaonesha dalili zozote za kutaka kuchukua fomu za kugombea urais.

Alisema kinachoonekana sasa ni kwamba huenda baadhi ya watu hawataki mtoto huyo aendelee kuwepo kwenye nafasi hiyo kwa dhana kwamba kuwepo kwake hapo,'kuna mkono' wa baba yake.

"Inashangaza sana watu wanataka tumfukuze Ridhiwani kwa sababu baba yake amekuwa Rais, kwa mantiki hiyo mtoto wa Rais aajiriwe katika ofisi zipi ? "alihoji Bw. Masha.

Akizungumzia mtoto wa Rais wa Zanzibar, Bi. Fatuma Karume ambaye naye anafanyakazi kwenye ofisi hiyo, alisema kuwepo kwake katika ofisi hiyo kulitokana na uwezo mkubwa wa utendaji alionao.

Bw. Masha alisema awali, Bi. Fatuma alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni yake na walikuwa wakisaidiana mambo madogo madogo na baadaye kampuni hiyo iliamua kumchukua baada ya kuafikiana.

Alisema kutokana na taarifa zilizotolewa na gazeti hilo kampuni hiyo inaangalia hatua gani itachukua dhidi ya tuhuma hizo na kwamba yeye hawezi kuzungumzia sasa kwa sababu hahusiki kwa kuwa kuna uongozi mwingine. Akizungumzia kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Masha alisema watu wengi wamekuwa wakihoji kupewa wadhifa huo mzito katika umri mdogo.

Aliwataka watu hao kutambua kuwa yeye alianza kuongoza kampuni kubwa nchini tangu mwaka 1991 .Alisema utendaji wake mzuri wa kazi ndio ulimfanya aonekane anafaa kuongoza nchi katika umri wake wa sasa wa miaka 38.

"Leo hii ukiniuliza ni kwa nini nimeteuliwa kuwa waziri sina jibu,sikujiteua mimi na jibu hilo lipo katika ngazi ya uteuzi, wakaulizwe walioniteua,"alisema Bw. Masha. Wakati huo huo watu tisa wanaotuhumiwa kutaka kufanya ugaidi wakati wa ziara ya Rais George Bush wa Marekani nchini mwezi uliopita, wameachiwa huru.

Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Masha alisema watuhumiwa hao wa ugaidi waliachiwa huru Februari 18 mwaka huu baada kufanyiwa uchunguzi wa awali.

Alisema pamoja na kuachiwa huru, bado taratibu za uchunguzi zinaendelea na itakapobainika kuwa walitaka kujihusisha na vitendo hivyo vya kigaidi hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa.

Bw. Masha alisema waraka aliotumiwa na Waislamu kuhusiana na watuhumiwa hao,ataujibu na kufafanua kwamba awali hakuwza kuujibu kutokana na waraka huo kusambazwa kwenye vyombo vya habari.

"Hawa watu walionitumia barua kutaka msaada wangu, walikuwa hawahitaji msaada wenyewe, ila walikuwa wananifikishia taarifa,"alisema Bw. Masha.

Alisema kuwa hata hivyoanajiandaa kuijibu barua hiyo kwa sababu inamhusu na inahitaji majibu.


Hoja ni kuwa hapo Masha kaongea kama waziri au binafsi? bado ana hisa kwenye hiyo kampuni? ule'utaratibu wetu' wa kutenganisha biashara na siasa haujaanza kutumika?
 
Hii hapa habari yenyewe waungwana:



Hoja ni kuwa hapo Masha kaongea kama waziri au binafsi? bado ana hisa kwenye hiyo kampuni? ule'utaratibu wetu' wa kutenganisha biashara na siasa haujaanza kutumika?

Mkuu,
Ume highlight kitu muhimu sana. Inaelekea Masha bado anajihusisha na biashara huku akiendelea kuwa waziri. Hili sio jambo zuri kabisa.

Kulikuwa hakuna haja ya yeye kuitisha press conference kuongelea scandal
ambayo inaihusu kampuni ambayo yeye sasa sio mkurugenzi tena.

Angeweza ku comment kama angeulizwa kama mengineyo na waandishi wa habari.

Mpaka sasa naona Masha hajafanya vibaya sana, badala ya kuwapiga madongo, inabidi kuwa support watu kama hawa, japo ni vizuri pia kukosoa makosa yao ili wajirekebishe.

Kwa Tanzania, ukiwa kwenye system ni ngumu mno usikumbwe na matope ya wahusika wengine. Unless kuna ushahidi wa kutosha, naona tumpe benefit of the doubt.

Huwezi kujua mpaka uingie kwenye siasa au biashara za Tanzania, system yote ni mbovu mno kuanzia chini mpaka juu na ndio inawafanya hata watu makini
washindwe kuwa waangalifu na hivyo kujikuta uchafu wa wengine unawarukia hata wao.
 
Nilisoma Resume ya Hon. Masha na nikasema what a smart guy, good experience, academia.. Lakini leo nimekuwa proved wrong, one time Sen.John Edward alisema kama big resume ni qualification ya utendaji bora then VP wa US angekuwa mtendaji bora.

This guy doesn't have sense. sorry i said, sababu kwanza yeye ni nani kuja kumdefend Ridhiwani kwenye media? Jee yeye ni msemaji wa State house? Muda anaopoteza hapo nani anafanya kazi yake? Jamani i wanna take kazi ya uandishi wa habari, swali ni mmoja tuu " Jee wewe unakuja kumtetea Ridhiwani kama nani'? Jibu, nilikuwa muajiriwa wake. Jee wewe ni muajiriwa wake sasa? Then tukikwambia kwamba unajikomba kwa muheshimiwa utasemaje?

Kweli some time kusoma kwenye vyuo vyetu huku ng'amba ambavyo ni kama uchochoro kunasaidia. Maana kabla ujaamua unawaza. How can you call the press meeting to discuss something which doesnt affiliate with you what ever?
 
Mkuu,
Ume highlight kitu muhimu sana. Inaelekea Masha bado anajihusisha na biashara huku akiendelea kuwa waziri. Hili sio jambo zuri kabisa.

Kulikuwa hakuna haja ya yeye kuitisha press conference kuongelea scandal
ambayo inaihusu kampuni ambayo yeye sasa sio mkurugenzi tena
.

Angeweza ku comment kama angeulizwa kama mengineyo na waandishi wa habari.

Mpaka sasa naona Masha hajafanya vibaya, badala ya kuwapiga maodongo, inabidi kuwa support watu kama hawa, japo ni vizuri pia kukosoa makosa yao ili wajirekebishe.

Kwa Tanzania, ukiwa kwenye system ni ngumu mno usikumbwe na matope ya wahusika wengine. Unless kuna ushahidi wa kutosha, naona tumpe benefit of the doubt.

Huwezi kujua mpaka uingie kwenye siasa au biashara za Tanzania, system yote ni mbovu mno kuanzia chini mpaka juu na ndio inawafanya hata watu makini
washindwe kuwa waangalifu na hivyo kujikuta uchafu wa wengine unawarukia hata wao.


exactly mkuu...hapo sasa ndo amespill the beans...watua ambao walikuwa hawajasoma mwanahalisi sasa watajua kuna ishu kama hiyo na ndo kwanza amefungua mjadala kumhusu yeye na Ridhiwani pia.
 
  1. Kaajiriwa Ridhiwan (kwa uchapa kazi wake!)
  2. Kaajiriwa Fatma (kwa uchapa kazi wake!)
  3. Kateuliwa Masha kuwa waziri (kwa umahiri wake!)
  4. Kwateuliwa Mujuluzi ( mkurugenzi mwingine wa IMMA) kuwa jaji (kwa utendaji mahiri!)
  5. Ishengoma mkurugenzi wa Deep Gold (kwa umahiri wake labda?)
Ni coincidence tu Watanzania, aminini tu! Msihoji!
 
JF nina waamini kwa kusimamia issue hata kama unakuta inamgusa Baba yako lakini JF is for that .Naomba kujua nyie leo mnasema Masha ni Msafi ni sawa na kuimba JK ni msafi ila Serikal yake chafu . How comes bwana .JK aunde Serikali iwe butu then yeye awe sharp ? How do you distinguish Meremeta na Mkapa ? Kiwira na Mkapa, Yona ? Mwananchi Gold na Warioba ? BOT na gavana na hatimaye CCM na Serikali nzima? Hebu tuwekane sawa .
 
  1. Kaajiriwa Ridhiwan (kwa uchapa kazi wake!)
  2. Kaajiriwa Fatma (kwa uchapa kazi wake!)
  3. Kateuliwa Masha kuwa waziri (kwa umahiri wake!)
  4. Kwateuliwa Mujuluzi ( mkurugenzi mwingine wa IMMA) kuwa jaji (kwa utendaji mahiri!)
  5. Ishengoma mkurugenzi wa Deep Gold (kwa umahiri wake labda?)
Ni coincidence tu Watanzania, aminini tu! Msihoji!

Then why Hon. Masha came into public and defended Ridiwani if it is just coincidence? What does he try to protect? I smell fishy, it seems they are cooking the kitchen.

Kwa nini anatishia kulikomesha gazeti lilochapisha habari? There is something he is trying to hide. We will find it sooner or later. Does it have anything to do with his jop position? Is he worrying about something that public doesn't know about it?
Is he seeing something that majority of us cant see?

What is it? Maswali bila majibu, why why why????
 
Then why Hon. Masha came into public and defended Ridiwani if it is just coincidence? What does he try to protect? I smell fishy, it seems they are cooking the kitchen.

Kwa nini anatishia kulikomesha gazeti lilochapisha habari? There is something he is trying to hide. We will find it sooner or later. Does it have anything to do with his jop position? Is he worrying about something that public doesn't know about it?
Is he seeing something that majority of us cant see?

What is it? Maswali bila majibu, why why why????

Issue za TZ huwa zinaanza kwa kuitwa Udaku na sasa zinakuwa msumari zinaanza kuchoma tena msumari wa moto . Sasa mlo sema the guy smart ndiyo hivi alivyo kurupuka ?Hivi Ridhiwan yuko Tanzania ama nje mbali ambako hata hawezi kusoma magazeti na kwenda maelezo ? Kwa nini atishie kwenda Mahakamani badala ya kwenda kuwaita tu Mahakamani ?Yeye ni waziri wa mambo ya usalama sasa. Kubenea anaanza kutishwa .Je ni connection ? Hakutakuwa na ocnflict of interest mwisho wa siku na Kubenea atauawa kweli na polisi hawatafanya lolote ?
 
This is just a confused government. Sasa waziri wa mambo ya ndani kwenda kutetea shirika la wakili binafsi ndio utamwita huyo mtu ni smart? Sasa ikitokea hiyo kampuni kesho inafungua kesi mahakamani dhidi ya gazeti, what are the chances kwa haki kutendeka? These are matters of common sense. Well, hata mimi nilikuwa na matumaini makubwa sana na huyu Masha, lakini sasa demeanor yake in the recent years imekuwa inanikatisha tamaa sana. He's increasingly becoming as hopeless as CCM itself!
 
Minister belittles link with JK's son
By Rose Athumani
THE CITIZEN

Home Affairs minister Lawrence Masha yesterday rejected accusations that he owes his position to association with the son of the Head of State.

Defending his position as a politician and a lawyer, the minister said accusations hat his appointment is linked to his association with Ridhwani Kikwete, a law intern who later joined the minister's advocates' firm, were malicious and baseless.

Mr Masha was reacting to the media reports that linked his appointment with the president�s son, making it clear that he took 'Sabbatical' leave from 2005, in order to be fully engaged in politics.

�I am a director of IMMA advocates together with my partners but I have been on Sabbatical leave since 2005,� he affirmed.

�If there�s anything that was done by IMMA, then it should not be personalized or directly linked to me or my appointment as cabinet minister,� he urged.

He said the president�s son worked as an intern at IMMA law firm as a final year student of the University of Dar es Salaam mid 2004 to 2005, noting that his political career wasn't shaped by this young student's internship.

�We receive interns every year as a reputable law firm�the important thing to us is a student's ability to work and deliver not prominence or personality,� he told a packed news conference yesterday.

He was explaining how the president's son got employment at IMMA, saying that the law firm has a tradition of accepting law student interns and Ridhwani Kikwete was among those interns for that year.

�After the internship period we normally evaluate the interns and those we find had performed quite highly, we give them employment. And that�s what happened with Ridhwani,� he stated.

Mr Masha, visibly disturbed as he narrated those accusations, described the charges as "cheap politics" aimed at tarnishing his image and career.

�Politics in this country is beginning to be a bit difficult. It not actual politics but the politics of tarnishing each other's names," he said.

Local newspapers ran a story linking the president's son with the corruption and embezzlement saga on the Bank of Tanzania (BoT) where IMMA as a law firm was employed to prepare papers for Deep Green Finance Ltd, a company linked to the BoT scandal.

He also defended the entrance to the law firm of Ms Fatma Karume, the daughter of Isles President Abeid Amani Karume saying her entrance had nothing to do with her father being president.

He said that as the law firm started, Ms Karume was approached as a potential partner but at the time she had her own law firm. She later deciding to join IMMA "and at this point in time this should not be seen as political agenda," the minister intoned.

He described Ms Karume as a highly qualified advocate who has been named among this year's nominees for top arbitrator awards in Africa, according to the Chambers and Partners Global Report for 2008.

According to Chambers and Global Partners, a leading UK law firm, the rankings are based on legal ability, professional conduct, client service, commercial awareness, diligence and commitment to the client.

Ms Karume joined IMMA in the capacity of a partner and not an employee.

A weekly scandal hunting tabloid picked up her trail this week as well as Ridhwani as part of IMMA, the leading law firm in the registration of Deep Green Finance Ltd.

Citing the relationship between IMMA and the defunct DGFL of South Africa, Mr. Masha said his firm provided legal services and was paid for that.

�IMMA provides legal services to various clients both local and international�it is unfair to link our firm with any wrongdoing or misconduct on the part of some of our clients,� he emphasised.

Deep Green Finance Ltd was among 22 companies receiving payments from the BoT saga, cited in an audit report on the BoT External Payment Arrears (EPA) account, receiving Sh8 billion.

The paper similarly said company records at Brela, the registration agency, listed advocate Protase Ishengoma and Stella Ndikimi as DGFL directors, with Mr Ishengoma being one of the partners at IMMA
 
Alisema kutokana na taarifa zilizotolewa na gazeti hilo kampuni hiyo inaangalia hatua gani itachukua dhidi ya tuhuma hizo na kwamba yeye hawezi kuzungumzia sasa kwa sababu hahusiki kwa kuwa kuna uongozi mwingine. Akizungumzia kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Masha alisema watu wengi wamekuwa wakihoji kupewa wadhifa huo mzito katika umri mdogo.

Kwa kauli hii Masha amejichanganya, anazungumza kwa niaba ya IMMA at the same time anakanusha hawezi kuzungumza mambo ya IMMA kwa kuwa yeye sio mkurugenzi tena huko!

Masha.jpg


Mkuu vipi tena mbona unatuangusha vijana!
 
Suala la ufisadi ni pana, tusiwe na tabia ya kuangalia matokeo tu, tuangalie na chanzo pia. baba H unaweza kuwa sawa au la kwa kile unachosema. Mimi nitaangalia suala la kuajiriwa na hapa simwangalii Ridhiwan kama mtoto wa Kikwete bali kama mtafuta kazi(najua keshapata. Ninawajua magraduates wengi tu ambao tena walifanya vizuri lakini kupata kazi imekuwa ni ngumu sana. Ninafikiri hapa kuna suala la unamjua nani, na wala si unajua nini.

Masha ni kijana na msomi mzuri na ni bora akasimama katika misingi imara ya kutupa ukweli na si kufanya siasa katika kazi
 
Its so wrong for anyone to think kuwa kamati ya Dr. Mwakyembe ilimu uncover kila fisadi aliyehusika kwenye deal la Richmond, there must be some people ambao 'wamenusurika' kutokana na mazingira magumu ya upatikanaji wa ushahidi kama ilivyoainishwa kwenye ripoti. Na kama kawaida kuna wengine walienda kupiga kambi kwa wataalamu Bwagamoyo kuhakikisha kwamba vitumbua vyao haviingii mchanga!!It doesnt mean kama hukutajwa na Mwakyembe- you are clean! Naamini wote waliopona kwenye kamati, nguvu ya wananchi wanyonge kwa pamoja itawafunua na watajulikana, huu ni mwanzo tu..... 1. R. Kikwete 2. Masha 3.........,etc. Naamini hii list itaendelea, its just a matter of time.
 
I've had a feeling kwamba this guys is shaddy. Uhusiano wake na Ridhwani is nothing professional but all political and if he can spend even a minute trying to deny that he'll just be fooling himself. Wajanja wote wa mjini wanafahamu hilo so he should try givign another explanation.
 
am fired up, i have another question. Jee Hon. Masha atakubali kuanika vigezo alivyotumia kumuajiri Ridhiwani? We want some proof of what he said? Since he decided to play fair, then how can you prove that Ridhiwani was qualified candidate. That is all we asking.

I know Ridhiwani gatta brain, but our job in JamboForum is to keep them Honest, so Mr Masha plz show us the credentials.
 
Katika historia yangu kwenye JF Es huwa hatetei kitu bila ya maslahi.Nampenda Es maana akiwa na maslahi yuko tayari kukusafisha hata kama anapoteza heshima yake . Nimefuatilia hili la Masha kuanzia kwa Ridhwan ES you are firm .Wakati wengine wanakata issue hii lazima wengine waingie tena pembeni kujua , kitu gani unacho simamia namna hii kwa nguvu zako zote .Maana uko kama wazungu wanakupa msaada wakijua wanataka nini.Nakupenda kwa hil lakini najiuliza pia kwa hili .

1. Mkuu Mugi, karibu tena baada ya kupotea sana na hili jina.

2. Masha, ni my brother in blood, uwaziri wake haumfanyi awe less of a human being, nimeishi naye New York, in the 90s, na nime-share naye apartment kabla ya mimi kuoa, familia yake ni yangu, yangu ni yake, kule Sengerema kwao mimi ni mwenyeji sana, kwa kwenye hili sio kwamba ninaongelea mpita njia, sasa siwezi kumkimbia kwa sababu ni waziri au nimchukie kwa sababu yeye sasa ni waziri na mimi sio, hapana kwenye maisha hivyo, rafiki ni rafiki.

3. Masha, kuzungumzia IMMA, akiwa waziri hilo ameteleza period, angewaachia IMMA wenyewe wajibu, kwenye hilo nimezungumza naye jana ni off the line, lakini haimfanyi awe fisadi au un-qualified kuwa waziri, lakini ni makosa.

4. Mimi sio fisadi na wala sina urafiki na mafisadi, lakini siko hapa kuwahukumu tu viongozi bila ukweli, Masha sio fisadi, amekuwa amekuwa director Oxygen akiwa na miaka 28, ambapo angeweza kufanya mambo mengi ya ajabu kama kweli ni fisadi, Masha sio mmiliki wa IMMA, the matter of fact yeye ni mmoja wa wale waliokuwa chini kwa kipato pale IMMA, kulinganisha na wenziwe, lakini kama kuna wenye ukweli wauweke hapa uchambuliwe, lakini so far sijaona convincing dataz, lakini walionazo waziweke hapa.

Ahsante Mkuu.
 
Lazima niendeelee kusimamia msimamo wangu!!

Hivi ni vijana wangapi wanafanya vizuri kwenye vyuo na kwenye internship zao, lakini hawapewi kazi hapo IMMA hata wakienda kufanya intern hapo?.

Pili kwanini huyu Waziri aende kufanya press conference ya kumtetea Ridhiwni, wakati kubeana anatafutwa kutolewa roho lakini hajafanya press conference ya kumlinda?.
watu wanatishiwa maisha waziri hazungumzi, leo Ridhiwani kasemwa tu na gazeti, waziri kaja juu na anataka kulifikisha gazeti mahakamani!!!!
Bado mnasema the Guy is Smart, usimate kwa kukutea wachache wenye sifa na uwezo, nani atatutetea wanyonye sisi, wana JF, kubeana, na wengineo huo kinyamkela kijijini???

Hapa kubali usikubali, swala ni kulindana na kupeana shavu kwa kujuana jamani, hii ndo Tanzania na wengi wanalijua hilo.

Baba H punguza hasira. Wadau hatuna fact za credebility za Ridhiwani mpaka kuajiriwa. Tunachokijua mpaka sasa ni kwa nini Mh. Masha kaja kumtetea Ridhiwani kwenye press media?

Jee tangia achukue wizara yake ni mangapi ameshakuja kwenye media kuyazungumza? Sababu nimesoma news nyingine naona anadai Tanzania kuna dirty politics inaongozwa na media. Kwanza naomba niseme kwamba media bado haijafanya movement za kutosha kuwa brief wananchi.

Sasa BabaH naomba tusaidie swala mmoja, Jee unafahamu credentials za huyu kijana alipokuwa pale UDSM school of Law? Was he in top 5% in the class of the year 2004-2005? Sababu nimeona Hon.Masha amesema kwamba wanachukua cream student, then i want know if Ridhiwani was all the time in the Dean's list?.

BabaH, plz defend your point. Why do you think Ridhiwani doesn't qualify for that position?
 
Mimi nasema kama ndio Masha anasema kuwa anaanza kazi inabidi aangalie sana manake amejichanganya sana,sidhani kama waziri anayetegemewa na taifa zima anaweza akatetea kampuni moja ambayo pia anasema hahusiki nayo...inamix kidogo...
 
...this guy(Masha)is a joke. According to my knowledge and understanding ya siasa za Bongo, kuchaguliwa kuwa minister si kwamba he has something extra to offer, Karamagi,Mapuri,Meghji etc are the living examples of useless public servants!!

Tanzania oxygen aliyoiongoza ilikufa kifo kibaya sana!!

In conclusion ni kuwa, his position in the government is indeed imekuwa boosted na uhusiano wake na wakuu behind the scene!!Kuendelea kwake kukataa ni kututhibitishia kuwa kuwa ana akili timamu!! Wo would admit this kind of a thing in a million yrs!!
 
Back
Top Bottom