'Mimi ni Masiha Nimeletwa Kuiokoa Dunia'

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079
2557494.jpg

David Shayler hali yake ya zamani kushoto na alivyo hivi sasa kulia Monday, July 20, 2009 1:50 AM
Afisa wa zamani wa shirika la Ujasusi la Uingereza M15 ambaye aliachishwa kazi miaka 6 sita iliyopita ameamua kuwa shoga na kuvaa nguo za kike huku akijitangaza kuwa yeye ni Masiha ambaye ameletwa kuja kuiokoa dunia. Kwa miaka 10 iliyopita David Shayler (40) alikuwa ni afisa anayeheshimika sana katika shirika la ujasusi la Uingereza M15, lakini baada ya kuachishwa kazi miaka sita iliyopita Shayler ameamua kuwa shoga na hivi sasa anajiita Masiha ambaye ameletwa kuikoa dunia.

Shayler ambaye hivi sasa anaishi kwenye nyumba moja kwenye kijiji cha Abinger Hammer, Surrey pamoja na kundi la wafuasi wake, amejibadilisha mpaka jina na kujiita "Delores Kane" na huvaa vimini na wigi na hujiweka matiti ya bandia kifuani.

"Nimegundua kuwa mimi ni Kristo na nipo hapa kuiokoa dunia. Mwaka 2012 unatabiriwa kuwa ndio mwisho wa dunia".

"Kazi yangu ni kuwaonyesha watu nini cha kufanya mwisho wa dunia unapokaribia. Kama ilivyokuwa kwa Yesu mimi pia nilifungwa jela na kuadhibiwa ili niwe mwokozi wa watu" alisema Shayler.

Shyler alizusha mtafaruku baada ya kudai kuwa Yesu naye alikuwa ni shoga na ndio maana na yeye ameamua kuwa shoga.

Shyler alisisitiza kuwa yeye kwa kushirikiana na wafuasi wa kundi lake wataiokoa dunia hii ambayo inaelekea kufikia mwisho wake mwaka 2012.

Shyler anakumbukwa kwa mtafuruku mkubwa aliouzusha baada ya kujiunga na kundi la wahanga wa shambulizi la septemba 11 nchini Marekani linaloitwa 9/11 Truth Movement, na kuwaambia wafuasi wake kuwa shambulio la mwaka 2001 lilifanywa na serikali ya Marekani na kuongeza kusema kuwa ndege mbili zilizoyagonga majengo ya Twin Towers zilikuwa ni mabomu yaliyofanywa yaonekane kama ndege kwa kutumia teknolojia ya hologram.

Shyler hivi sasa amefungua tovuti yake "I am Messiah" ambayo ndani yake anaelezea imani zake na mawazo yake ya kuikoa dunia.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2557494&&Cat=2
 
Siku hizi za mwisho tutaona nakusikia mengi.Mchafu na azidi kuwa mchafu,mtakatifu na azidi kutakaswa
 
Hakika hizi ni siku za Mwisho.

Eeh Mola tunusuru sisi na vizazi vyetu pia.
 
Back
Top Bottom