Mimi nalilia Nchi yangu Tanzania

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
522
240
Ndugu zangu Watanzania, sina maneno ya kuweza kutumia ili muelewe mpaka sasa nchi yetu siyo ile tuliyo kuwa nayo wakati wa mwalimu Nyerere! Sasa hivi hii nchi si yetu tena. Nchi hii imechukuliwa na mafisadi tena siyo wa hapa ndani tu bali hata watu wa nje wamekuja kututawala.
Ndugu zangu, naomba nianze na suala la uchaguzi la mheshimiwa spika. Spika wetu inasemekana amewekwa na kikundi fulani cha watu. Anna Makinda hakuwa na nia ya kuchukua fomu ya kugombea uspika. Baada ya mafisadi kuona mwiba wao mheshimiwa Samwel Sitta anachukua fomu ya kugombea uspika, walimtuma fisadi mwenzao akimbie haraka kwenda Njombe kumshawishi Makinda kuchukua fomu ili waweze kumpitisha awe spika kwa kuwa yeye hana uwezo wa kugundua mambo haya yanavyokwenda. Yeye bila kujua amechukua hiyo fomu. Mafisadi walijua hata baada ya Makinda kuchukua fomu asingepitishwa na wabunge kwa kuwa wabunge wenge walikuwa wanamhitaji Sitta. Waliamua kuja na mpya ya mwaka eti sasa ni zamu ya mwanamke kushika mhimili wa tatu-BUNGE! Kwa kuwa Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha wanazungukwa nao wanaendelea kushangilia eti wamepata spika mwanamke. SHAURI YENU! Mnauza nchi.
Kwa nini mafisadi hawamtaki Sitta? Kila Mtanzania ni shahidi wa kazi aliyoifanya mheshimiwa Sitta katika Bunge la tisa. Kwa kuwa alikuwa ni tishio kwao kwa kuruhusu mijadala iliyokuwa inawachimba mafisadi.
Watanzania ambao wana nia nzuri na nchi yao hawawezi kugomea mambo haya kwa sababu hawajui haya. Kama mambo haya siyo kweli naomba niambiwe mazingira yaliyotumika kumchagua spika je, ni ya mtindo gani hayo?
Kikubwa kinachofanyika katika nchi yetu ni kuiachia kwa mafisadi polepole. Mafisadi wana nguvu ya fedha na kimkakati. Wanataka kuhakikisha nchi hii sasa si ya Watanzania bali ya watu wachache wenye pesa.
Leo hii Watanzania, ajabu hata waandishi wa habari wanawalaumu wabunge wa CHADEMA kususia kuapishwa kwa waziri mkuu. HHawajui mantiki yake. Watu wote wanaoelewa mambo haya hawapo tayari kwenda sehemu ya maapisho ambayo mnajua kabisa Watanzania wanazungukwa. Hii ni sasa kwa Mtanzania yeyote ambaye ana uzalendo wa nchi yake Tanzania.
Viongozi wengi wanataka siasa nyepesi ambazo hazina mkakati mahsusi wa kutatua matatizo yaliyo kwenye nchi yetu. Mfano, hivi ndugu zangu ni nini umhimu wa kuwa na wabunge wengi kiasi hiki kutoka Zanzibar? Gharama za kuendesha mambo haya zinatoka wapi? Jamani Watanzania na viongozi wetu tukae chini tuone nchi hii ytunaipeleka wapi!
Mambo haya yote yanatisha! Kwa sasa mambo yanayoendelea hayana tija kwa Mtanzania!
CHADEMA ni chama ambacho kimeyaona haya yote, uonevu unaoendelea na ndio maana unaona wanakuwa na msimamo thabiti wa kuwatetea wananchi. Spika wetu anadiriki kuwaita viongozi wa upinzani bungeni na kuwaambia kutoitambua serikali ya JK itasababisha wasipewe nafasi kwenye kamati za bunge! Hii inamaanisha kuwa wabunge hawa badala ya kuangalia maslahi ya taifa waangalie maslahi yao binafsi. TANZANIA YETU BWANA!!!
Kwani kwa nini CCM sasa imejawa na watu fulani na wanashughulika sana kuhakikisha watu fulani tu ndo wanashika nafasi za juu katika nchi hii. JAMANI HAKUNA AMANI BILA HAKI!!
Hivi ni nani asiyejua utendaji kazi wa mheshimiwa Makinda. Je, kuna maslahi gani ya kumpigia upatu awe spika wa bunge letu? TUAMKE NDUGU ZANGUNI! UNYONGE WETU usitumalize kiasi hiki. Tufike wakati ambapo maamuzi ya wananchi ndo yawe msingi wa kupata viongozi wa nchi yetu. Kama huu utaratibu wa kuchakachua kura utakuwa ndo mtindo wenyewe, hakuna siku tutapata viongozi sahihi wa kutetea nchi hii. Hao viongozi wetu wanaopewa vyeo na kuvishqangilia hawajui hata yale yanayoendelea. Wenyewe kikubwa ni hivyo vyeo wanacyopata. Hawajui kuzazi cha baadaye kutarithi nini.
Watanzania, hivi kweli kuna sababu yoyote ya makampuni yanayochimba madini hapa kwetu kusafirisha mchanga mpaka huko ughaibuni! Kweli ndugu zanguni tuweke ubinadamu mbele na siyo ubinafsi.
 
Back
Top Bottom