Mimi na nyumba yangu TUMEAMUA CHADEMA mpaka Kieleweke

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Tangu kuanza kwa harakati hizi za vyma vingi nilijisemea moyoni lazima niongeze uzazi ambao utasaidia mageuzi ya haraka hapa Tanzania, baada ya kuona mafisadi wanapandikiza watoto wao kwenye siasa, nikajisemea haikubaliki, Ngoja mimi na familia yangu tuanze kupeana darasa la Uraia na Utaifa , katika hili mageuzi hayatashindikana, kama maandiko yasemavyo huwezi kuimba nyimbo za Bwana Ukiwa Ugenini, hivyo nimeamua kuwafundisha itikadi sahihi watoto wangu , kwafaida ya kuikomboa nchi toka kwa wakoloni weusi.
CHADEMA NI KWAVIZAZI VYOTE
.

404502_2940387143602_1078884546_3217501_168364347_n.jpg
 
kweli umeamua, ulichelewa wapi chadema ni kama airtel. Hawa watoto mbona wako peke yao bila mama au mama ni CUF mwanadada wa CCM?
 
Wakikua ndani ya mavazi hayo tu, nguvu tosha 2020. Mbona mmewabagua skafu ya chama?
 
Duh huyo dogo wa tatu kulia kafanana na mwanasheria mkuu wa serekali.

404502_2940387143602_1078884546_3217501_168364347_n.jpg
 
Ata slaa ni fisadi pia,
Alimfisadi mshikaji fulani akampola mke mchana kweupe.
Lipumba yuko juu.
 
Hakika watakuhukumu vijana hao wakipata akili zao kwakuwaamulia itikadi ambayo huenda hawapendi, huyu wa mwisho analia akiashiria hapendi hata hizo nguo.

Jamboi la pili nikushauri ndugu yangu kuzaa watoto wengi ambayo baadaye utashindwa kuwapeleka shule wakakosa ajira wakapokea kofia na t-shirt za kampeni ya chama usichopenda wakatoa na kura hoko utajiua kwa sumu. Tafakari chukua hatua ya kuwasomesha kwanza. mwisho waulize wapemba kama walifanikiwa katika mikakakti hiyo ya kuzaa sana wakaishia serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Ata slaa ni fisadi pia,
Alimfisadi mshikaji fulani akampola mke mchana kweupe.
Lipumba yuko juu.

HAPANA Hakumpora; Bali jamaa alishindwa kuhudumia hivyo alikuwa anamsaidia kulea mke. Tehe tehe tehe...............


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
hivi hawa wameshafikisha umri wa kupiga kura kweli hawa?

hawajafikisha, tunawaandaa kwa 2020. kama wanamiaka 7 na 8, watakuwa na umri wa miaka 18, inayotosha kupiga kura.

nampongeza mzazi kwa mwono wake wa mbele
 
yaani wew na Nyumba yako mmefanya CHAGUO LA BUSARA SANA!!!!

HEKO!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
yaani wew na Nyumba yako mmefanya CHAGUO LA BUSARA SANA!!!!

HEKO!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Mizambwa kumbe hata wewe una damu ya ufisadi:teh teh teh,ngoja niwasiliane na wanajamii ili wasikupe nafasi ya kugombea kwenye baraza na wana jf.
Umenikatisha tamaa!
 
lazima katika kuelekea ukombozi kamili tuanze kuingiza itikadi za mabadiliko kwa kizazi kipya, tuwekeze kwa vijana wasafi, tuwaache mafisadi wawekeze kwenye majumba na anasa zingine maana kipindi kifupi kijacho tutarudisha mali zetu, tutarudisha raslimali zinazoibwa pale HAZINA KUU ya serikali, tutawafunga na kuwanyonga wezi wote wa mali za umma, si mbali ni kafibu, amka Tanzania , wakati ni sasa.
 
Nimeipenda sana hii. kazana kulea familia iwe na afya tele

asante sana. nashukuru kwakweli, tunaendeleza mapambano kutokea ndani ya mioyo yetu, kisha kwa watoto wetu, halafu kwa majirani zetu , kisha taifa zima.
 
Ni kweli ni wewe na nyumba yako mmeamua kutumikia CDM kwa sababu zenu binafsi ata Mimi na ukoo wangu tumeamua kuitumikia CCM kwa sababu ambazo tunaamini ni za msingi kama vile ni chama cha watanzania wote yeyote yule mwenye sifa anaweza pata nafasi ya uongozi si chama cha udini au ukabila au ukanda,Ni chama chenye sera zinazotekelezeka na wala si za kufikirika kama za mfalme juha,Ni chama ambacho kina mfumo mzuri wa upatikanaji wa mgombea jimboni ata mimi naweza gombea nafasi yoyote ile kuwakilisha chama changu kwenye uchaguzi mkuu kama vile Uraisi,ubunge,udiwani,uenyekiti wa mtaa au wa kijiji kupitia mfumo wa kura za maoni nanachaguliwa na wananchi wote ambao ni wana CCM jimboni lakini kwa vyama vingime majina yanaletwa toka makao makuu alafu wanadai kamati kuu imeamua wakati humo kwenye kamati kuu wako ndugu, jamaa na marafiki yani baba,baba mkwe,mama,dada,kaka, wachumba na wake zao wako humohumo kama hujulikani makao makuu imekula kwako,Ni chama ambacho viongozi wake wako karibu na wananchi na ni wasikivu kwa yale yanayosemwa na kuitajika na wananchi kwa manufaa ya taifa mfano Raisi Jakaya Kikwete hii imethibitishwa na kambi ya upinzani bungeni hizo ni bahadhi ya sababu nikisema niandike zote humu nitakesha kila kukicha,CCM Oyeeeeee,Idumu CCM daima!
 
Back
Top Bottom