Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,778
- 59,133
"Hivi mwanaume kakataa mimba we umelea ya nini? Haki ya nani mi mwanaume hajaniachia mimba nikalea, labda aniachie mtoto hapo angalau!"
Hayo ni maneno ya dada mmoja kwenda kwa mwingine ambae ni mama mtarajiwa. Alikua anamwambia kauli yake ikisuggest kwamba mwanaume anapokimbia/kataa mimba basi kiumbe cha watu kinakosa haki ya kuishi hivyo kitolewe. Hii kitu imenifanya nijiulize. . .
1.Hivi mimba ni ya nani? Ya mwanaume hivyo asipokua tayari kushiriki katika malezi yake basi iondolewe na kutupiliwa mbali?
2.Mimba ni ugonjwa usiozuilika hata watu wasijali wakati wa kupata ila wawe tayari kutumia gharama kuziondoa?
3.Baadhi ya wanawake wa akili za aina gani hata wajiweke katika position za kupata mimba na mwanaume asiyeeleweka huku wakijua fika 'BILA KUWEZESHWA HAWAWEZI'??"
Nasikitika kuona kwamba wanawake wengine wana fikra zilizokaa kinyume nyume na bila huruma wako tayari kuadhibu viumbe ambavyo havikishiriki kwenye mambo na starehe zao binafsi.