Mimba za watoto shuleni; Nani alaumiwe?

Isimilo

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
217
6
Kumekuwa na ongezeko kubwa kuhusu mimba za watoto(wanafunzi wa kike mashuleni kwa kasi ya aina yake.
Serikali kwa mtizamo wangu imekuwa na upeo finyu sana wa kuelekeza uwajibikaji kwa wale wanaowapachika wanafunzi mimba.

Pili kwa jinsi ambavyo utakuta serikali inajadili hili jambo mtuhumiwa huwa ni mtu mzima against mwanafunzi. hapa kuna loophole kubwa sana inaachwa ambapo wanafunzi kwa wanafunzi( ME/KE) hawatajwi kama wanahusika katika sakata hili.
angalau litajwe hata kisiasa tu kwenye majukwaa: hapana kiongozi ambaye amewahi kujaribu kukosoa watoto wa kike/kiume kuwapa wenzao mimba.

Je, hili siyo lililotuchelewesha kwenye mapambano ya ukimwi pale ambopo tulikuwa tunashindwa kuweka suala la kondom wazi wazi mapema?

Anatajwa mwanafunzi wa kike kama muonewaji na raia (mtu mzima kama mkosaji) lakini hivi sasa kwa kutumia ushahidi wa kimazingira(sentensi za kibunge) naona kabisa wanafunzi wa kiume (matured) about 90% wana mahusiono ya kimapenzi na wanafunzi wenzao tena si mmoja bali (in bundles).

Serikali haina mkakati wowote wa kisheria unaoonyesha (uwajibishaji wa hawa wanafunzi hasa pale wanapokuwa wamepeana mimba wenyewe kwa wenyewe.

Pia kumekuwa na mwanya wa kuwapa wasichana uhuru usiokuwa na kikomo kwa sababu wao hawana sehemu yoyote kisheria inayowaogopesha kutenda kosa hilo.

Ina maana kweli dhana iliyowekwa kwamba walidanganywa kwa 100% inwaondolea kuwajibishwa kabisaa.

Jambo lingine la kuongeza hapa ni kuhusu usafiri. Jambo hili linatia huruma na simamzi sana kwa kuona jinsi wanafunzi wanavyoteseka sana kwa ajili ya usafiri.

Ila kuna kitu huwa nakutana nacho mara kwa mara labda mnaweza kunisaidia hapa; mara nyingi mida ya kuanzia saa nne usiku na kuendelea unakutana na mwanafunzi ana uniform zake anatoka shule na in most case if not all the time of the occasion utakuta mwanafunzi huyu ni wa kike, je hoja ya usafiri hapa bado ina hold? Tena utakuta companion ni boys ambao wako katika mavazi ya kawaida.

Nauliza hivi kweli is it fair not to make these ladies guilty and ANSWERABLE when they come accross pregnancy.
 
Hili ni swala la maadili ya jamii yote na sii tu swala kuwafunga wanaume wahusika! Maana watoto wa siku hizi hupevuka mapemma na hujifunza haya mambo mapema!

Elimu ya kujamiiana iimarihswe mashuleni na pia athari za ukimwi! Pia wazazi waongee wazi2 bila kificho na watoto wao!
 
Nani alaumie? - Jumuiya ya wazazi na Wizara ya elimu!!!

Pamoja na ukosefu wa maadili katika jamii yetu, kama Mzalendohalisi alivyofafanua, tatizo jingine linalosababisha hivyo vibendi kwa wingi ni ukosefu wa effective 'After-school-Programs.'

Watoto wakitoka shule ile saa 8, huwa hawana shughuli nyingine yeyote ya maana zaidi ya kusarandiana huko mitaani tu. Kuna umuhimu wa jumuiya wa wazazi na wizara ya elimu kushirikiana kuanzisha after school programs (zaidi ya vijituisheni mshenzi) ambazo sio tu zitawa keep watoto bize, bali pia kuipa changamoto IQ zao.....hence kuondoka na "Wafrica Ndivyo Tulivyo (NN style)" epidermic.
 
Back
Top Bottom