Mimba za wanafunzi sheria inasemaje?

Watunduru

Senior Member
Dec 29, 2011
170
39
Imekuwa ni jambo la kawaida mzazi kukamatwa,kutozwa faini au hata kifungo kwa sababu tu eti mtoto wake wa kike {mwanafunzi}kapewa mimba,au mtoto wa kiume katia mimba.tusiojua sheria tunashindwa kuelewa kigezo kinachotumika kumtia hatiani mzazi kwa kosa ambalo kimsingi hakulifanya yeye binafsi na pengine hata wakati kitendo kinafanyika hakuwa na habari na au asingependezwa nacho.hebu wana sheria nisaidieni ktk hili.
 
Wazazi wanatozwa faini kupitia sheria ya UPE, kwa kushindwa kusimamia mtoto aende shule, hasa wengine
hawajali kama mtoto amefika shule au la, hata akiitwa shuleni haendi, au akienda hali ya utoro wa mtoto
haibadiliki, ni halali aadhibiwe maana anashiriki kutujengea taifa la wajinga. Kuhusu mimba ni sahihi waadhibiwe
kwani wazazi wengi hushiriki kupokea mahari ili binti aolewe, kama ni mvulana basi mzazi humsifu kuwa amekuwa kidume
kwa kutia watoto wa watu mimba. (mambo hayo yapo zaidi ukanda wa pwani).
Lakini binti kama hajafikisha 18yrs aliyemtia mimba anastahili kushitakiwa kwa kosa la kubaka, japo panatakiwa ushahidi wa
kitaalamu kama vile DNA kuthibitisha kuwa mnayemtuhumu ndiye haswa aliyempa mimba binti, kwani tukio hujulikana baada ya siku nyingi kupita hivyo ni rahisi kujenga mashaka na mtuhumiwa akaachiwa huru.
 
Back
Top Bottom