Mimba ya kwanza

TODO

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
219
62
Naombeni mawazo ndugu zanguni.wife kapata mimba huu ni mwezi wa pili naombeni mnishauri namna bora ya kuitunza ili aweze kujifungua salama lakn pia ajifungue mtoto mwenye afya njema.asanten kwa ushauri
 
kula balanced diet, kufuata ushauri wa Dr, kutumia Vitamins zilizopendekezwa bila kukosa, kupata mapumziko ya kutosha, kuacha kilevi na uvutaji wa sigara. Kila la heri.
 
Hakikisha anafanya yafuatayo:
2. Anapiga ultrasound kabla mimba haijamaliza miezi mitatu. Hii inasaidia kukadiria kwa ufasaha zaidi siku mtoto anayotarajiwa kuzaliwa.
3. Anafanya jitihada zote kujikinga na malaria. Malaria wakati wa ujauzito huhatarisha sana afya ya mama na mtoto. Atumie chandarua chenye dawa, akienda clinic atapewa dawa za kukinga malaria.
4. Akianza kliniki atapimwa damu. Ikionekana damu ni chini, pamoja na njia nyingine za kula matunda nk anywe vidonge vya madini ya chuma. Damu ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mtoto, vilevile damu inahitajika kama reserve kwa sababu wakati wa kujifungua kuna uwezekano wa kupoteza damu nyingi, hivyo akiwa na damu a kutosha inapunguza uwezekano wa madhara makubwa.
5. Ahudhuria cliniki siku zote atakazopangiwa.
6. Kikitokea kitu chochote msichokielewa vizuri, afikishwe hospitali mara moja kwa ushauri na matibabu.
7. Akifikisha wiki 37 afanye tena ultrasound ambayo pamoja na mambo mengine itaonyesha jinsi mtoto alivyokaa na hivyo kunwezesha daktari kuweka mkakati wa njia ya kujifungua.
8. Aendelee na shughuli zake za kila siku kama kawaida kadri atakavyoweza kuhimili. Ujauzito siyo ugonjwa...
 
kuwa naye karibu zaidi pia matunda kwa wingi na mazoezi una uwakika hiyo mimba ni haki usije kulea mimba za watu wengine kwa sababu wanawake mmmh
 
Back
Top Bottom