Millioni Zabebwa Dar!!!!

Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,631
4,225
Milioni Dar zabebwa mchana​

2008-09-05 16:06:10
Na Sharon Sauwa, Ilala

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa majambazi, wamevamia mchana kweupe katika ofisi za duka moja la vifaa vya ujenzi na kusomba simu za bei mbaya na mapesa kabla ya kutimkia kusikojulikana.

Taarifa za kipolisi zinaeleza kuwa tukio hilo limejiri jana, mishale ya saa 5:00 asubuhi pale Tabata Relini Jijini wakati watu hao, huku wakiwa wameshikilia silaha nzitonzito ikiwa ni pamoja na bunduki, walipovamia katika ofisi za kampuni moja ya ujenzi na kupora dola 1,150 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh. Milioni 1.2) na pia Shilingi Milioni Moja za Kitanzania.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Aibula Tanda, amesema watu hao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa katika magari madogo mawili aina ya Toyota Saloon lenye namba za usajili T 478 AVZ na jingine lenye namba T 365 AVK.

Akasema watu hao walipofika, walijifanya ni wateja wanaotaka kununua baadhi ya vifaa vinavyouzwa mahala hapo.

Akasema Kaimu Kamanda Tanda kuwa walipofika mapokezi, watu hao wakawaweka chini ya ulinzi watu watatu waliokuwa katika ofisi za duka hilo, kisha wakapora simu na fedha hizo.

Hata hivyo, akasema majambazi hayo hayakufyatua risasi na yakampora Mkurugenzi wa ofisi hiyo Bw. Lurjs Marjinuos, 29, simu yenye thamani ya shilingi 600,000.

Pia watu hao wakampora mteja aitwaye Bw. Alotiary Patrick al-maarufu kama Mosha, simu ya mkononi aina ya G81 yenye thamani ya shilingi 400,000 na dola 1,150 za kimarekani pamoja na shilingi milioni moja.

Akasema baada ya tukio hilo, watu hao wakakimbilia kusikojulikana na kwamba hadi sasa, Polisi wanaendelea kuwasaka.

Wakati huo huo, watu wengine watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemteka na kumpora gari dereva teksi Albatazar Msele kabla ya kumtupa katika msitu wa Jeshi wa Buza Sigara.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi, amesema tukio hilo limetokea jana saa 2:45 usiku wakati watu hao walipomkodi dereva wa teksi hiyo yenye namba za usajili T118 AQL.

Akasema watu hao walikodisha teksi katika eneo la Jet Lumo na kutaka wapelekwe Buza Sigara, lakini walipofika katika msitu huo walimkaba dereva kabla ya kumpiga na kumtupia nje.

Akasema Polisi wanaendelea na upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

SOURCE: Alasiri

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/...05/122013.html
 
Hizi ni salaam muafaka kwa Kamanda Kova.

Operesheni yake imeishia wapi? Au ndio anafukuzana na hao machangudoa na wapiga debe tu!
 
Back
Top Bottom