Mi nadhani bado kuna tatizo la watu kufahamu uislam na ugaidi. Inawezekana magaidi wakawa ni waislam lakini uislam si ugaidi. Dunia ya magharibi imewafanya watu waamini kwamba uislam ni ugaidi wakati si kweli hii ni njama walioamua kuieneza ili waweze kunyonya mafuta ya waarabu kwa urahisi. Asili hasa ya dunia ya kiarabu kupinga wenzetu wa magharibi ni huu utaratibu wa nchi za kimagharibi kuhakikisha kwamba resources zote za hapa ulimwenguni zinakuwa zao na kunufaisha kwao na kuziacha nchi husika zikiwa masikini kabisa. Haya mambo hayafanyiki kwa bahati mbaya hata kidogo, ni mipango kabambe ambayo kwanza wanahakikisha wanatengeneza watu wao wanawaahidi maisha saafi ulaya then wanaanza kula maliasili zetu taratibu.
Mkinyanyuka na kudai haki zenu ndo majina km magaidi, waasi nk hutokea lakini gaidi wa kwanza hapa duniani ni kundi la utawala la nchi za magharibi ambao ugaidi wanaoufanya kwa nchi za Asia na Africa ni afadhali ya Osama na kundi la Haram la Nigeria. Ni hizi nchi za magharibi zinazotufanya mpaka leo watanzania tukawa masikini hivi wakishirikiana na watawala wetu walioahidiwa maisha mazuri ulaya hususani Belgium (centre for African and Asian politics). Ukiangalia viongozi wetu woote wa africa na Asia wanamiliki majumba ya kifahari Ulaya. Sababu ni kwamba siku mkiamka na kudai vyenu wanakimbilia ulaya walipojiwekea maisha yao na ya watoto wao.
Kama kuna mtu anataka kuona haya aanzishe tu mfano wa upingaji wa kinachoendelea hapa nchini mara moja watamuita gaidi km ni muislam na ukiwa mkristo watakuita muasi. ikiwa na maana kwamba hutakiwi kupinga wanayofanya ma bwana wakubwa kwani wao ndo wamepewa dhamana na mungu kula mali zetu.
Nadhani ifike kipindi sasa watu wajue nini uislam na nini ni ugaidi bila hivyo tutajikuta tukichukiana bila sababu.
Hawa wenzetu asili hasa ya kupigania nchi zao zindeshwe ki islaam ni kwamba wanaamini ktk uislam muongozo thabiti ndipo utakapopatikana kwa sababu kuu zifuatazo:
1. Ni sheria za kiislam ambazo hazina matundu ya kutokea wala ubabaishaji, km mtu kaiba hukumu yake ni kukata mkono basi hakuna la kujadili.
2. Viongozi wasiokuwa na dini si viongozi ni mashetani, hawezi kuwa na huruma kwa jamii wanayoingoza na ndio maana unaona huyu mpagani bwana kingunge anapinga hata vitu vya msingi (waraka wa wakotoliki) bila hata kueleza mapungufu yake inakuwa shida.
Nawaomba ndugu zangu watanzania tuwe makini na hii dunia ya kimagharibi ambayo lengo lake kubwa ni kuvuna mali zetu wakishirikiana na ndugu zetu tuliowapa jukumu ya kuzilinda bila ya huruma kwa masikini wa nchi hii amabao hawajui mkate wao wa kesho ni nini.
kwa suala la sharia kuwa kali ni sawa, lakini China mbona haina sharia na mambo yanakwenda vizuri? mbona wahalifu wananyongwa kila siku bila kujali cheo wala mali zao?? hapa TZ na nchi nyingine za afrika kinacho kosekana ni nia thabiti ya kutekeleza sheria zilizopo na hiyo ni weakness ya watawala walioko madarakani.
Huwezi kusema wanaoiba mali ya nchi na kuweka nchi nyingine kama chenge nia yao ni baadaye waende kuishi huko, hilo siyo kweli kwa sababu hata mwizi wa kawaida huweza kuficha mali alizoiba sehemu nyingine ili kufisha ushahidi pindi akikamatwa. Kinacho takiwa ni serikali zinazokuwa madarakani kutaifisha mali iliyofichwa nje ya nchi, lakini tunarudi pale pale kuwa wezi ni hao hao viongozi.
Napinga hoja yako eti tukiwa ni nchi ya kiislamu basi tutaweza kudhibiti u-magharibi, mbona u-magharibi ni mzuri tu!! kinacho hitajika ni kuwa wa kweli na kudumisha demokrasia ya kweli. Wewe hujatembea nchi za kiislamu ukaona mateso wanayopata wananchi, hasa wanawake.
swali langu ambalo waislamu hawajawahi kuliji ni "kwa nini magaidi watumie dini ya kiislamu kufanya mauaji na hamuwakani kuwa siyo wenzenu?? Je, waislamu mtajitengaje na magaidi ili hali mmeshindwa kuwakana hadharani??"
kwa kumalizia, chonde chonde, mmwambie kabisa shehe ponda kwamba TZ hatutaki boko haram, hata boko isiyo haram hatutaki!!
hakuna maisha na utamaduni ulio wa huru na haki kama wa ki-magharibi, ndo maana wenzetu magharibi wana maendeleo!!