Milipuko ya gongo la mboto ni uzembe si ajali: Wanasheria mnasemaje?

mshaurimkuu

Member
Jan 23, 2011
57
30
Awali ya yote nawapa pole ndugu zetu wa Gongo la Mboto ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika na milipuko ya kizembe iliyotokea hivi karibuni. Kwa wale waliojeruhiwa, nawatakia afya njema na Mwenyezi Mungu awajalie kupona haraka ili wandelee na shughuli zao za kila siku. Kwa wale waliopoteza maisha kutokana na uzembe huu, tunawaombea wapate pumziko la amani. Tunalaani vikali uzembe huu ambapo ni takribani pungufu ya miaka miwili tu kwa staili hiyo hiyo uliathiri ndugu zetu wengine wa Mbagala; umbali usiozidi hata km. 15 kutoka ulipotokea mlipuko wa juzi.

Ndugu zangu, mimi si mwanasheria wala si mtaalamu wa lugha lakini napata tatizo sana na matumizi ya neno AJALI kama lilivyotumiwa na wanasiasa wetu katika mlipuko wa majuzi. Jamani, hebu watalaamu wetu tujuzeni, AJALI maana yake ni nini? Ni mambo haya madogo madogo ambayo katika mizania ya sheria yasipotafsiriwa vizuri na hatua mathubuti kuchukuliwa, wanasiasa wazembe huyatumia kudanganya umma na pia kuyatumia kama mlango wa kutokea.

Kama Bungeni hivi majuzi ulizuka utata na mtafaruku mkubwa hadi Bunge likakaa ili kupata tafsri sahihi ya neno "RASMI" ambalo kimsingi halikuwa na madhara yoyote kulinganisha na tukio la Gongo la Mboto; Je, si zaidi kupata tafsiri sahihi ya neno "AJALI" ambalo ndilo linalotumika kuhalalisha milipuko hiyo?

Katika kupitia pitia mitandao mbali mbali nimekutana na hukumu ifuatayo:

Ryland V. Fletcher iliyotokea mwaka 1865. Jaji Bluckburn Colin anasema kwa kimombo:

"The true RULE OF LAW is, that the person who for his own purposes brings on his lands and collects and keeps there anything likely to do mischief if it escapes, must keep it in at his peril, and, if he does not do so, is PRIMA FACIE answerable for all the damage which is the natural consequence of its escape."

Naomba nisichakachue, kwa maelezo ya kina kuhusiana na hukumu husika, bofya kiunganishi kifuatacho: Rylands v. Fletcher - Rule, Liability, Land, Strict, Defendants, and Water
 
Back
Top Bottom