MICHO THOMAS BK
Member
- Jun 2, 2012
- 48
- 6
Kuwa makini na vitu vya bure ni hatari au kama vp zichukue usizitumie kwa sasa weka ac ya Benk nyingine ili waki kufuatilia urudishe hyo hela mara moja.
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.
Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?
Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.
NB kwenye heading ni (50,000,000)
Hii inapendeza kwelikweli.Huoni Kama Umejipatia Mkopo....toa iyo pesa Tumia kwa vitu vya Msingi...coz end of the DAy. Bank itakutafuta na MtakubalianA jinsi ya Kuzirejesha...Mkopo. Huo HAuna Riba ...
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Kwa mujibu wa sheria za kibenki,makosa yafanywayo na benki hayambani mteja. Hayo ni makosa ya benki. Hupaswi kuogopa. Toa hizo pesa na uzitumie. Utajuta kuziachaacha pesa za bure
Kuna utofauti mkuu, hii ni 2012 dunia imekuwa kama kijijiilikuwa mwaka 82 nasimuliwa eti pale kijijini kwetu kuna ndege ilidondosha gunia la hela, akaliokota mama fulan (hadi leo yupo) afu maaskar walipokuja kawapa, wakamlamba kofi afu wakamwambia utakufa maskini, true 2 the moment she z very poor...WOGA WAKO NDO UMASKINI WAKO
Nashukuru kwa maelezo yako kuu, Account yangu haijawahi kuzidi milioni nane (8,000,000)inategemeana na account yako ikoje, kama account yako ina tabia ya kupokea hela mara kwa mara kubwakubwa kama izo, unaweza kunyamaza tu na kuzitumia huku ukisikilizia, wakija wambie mimi sikujua kama nina overdraft nilijua hela yangu ya kawaida imeingia. katika sheria za bank, ukiongezwa hela hivyo huwa si kosa la customer ni la banker wenyewe na huwezi kuadibishwa. this is just a matter of fact na kila kesi huwa inaamliwa kulingana na mazingira yake. mfano: kama account yako mara nyingi huwa haifiki hata 20m, ikaonekana uliomba bank statement au yapo mazingira kuwa ulilijua salio lako kabla na baada ya kuwa over-credit, ukaonekana labda umetoa hela haraka sana ili kuzikimbiza tofauti na kawaida yako, yaani bank statement yako itaonyesha kama ulikuwa na nia ovu kuitoa hela kwasababu umejua umeongezea au la....hapo utapatikana ushahidi wa kiamzingira kuwa ulikuwa na knowledge ya kuongezea hela isiyo yako na uliitoa haraka kwa nia ovu na utashitakiwa kwa kosa la obtaining money by false pretence au hata theft. cha muhimu hapo ni namna au afya ya account yako, kama inaingiza hela na kutoa mamilioni hayo mara kwa mara unaweza ukawambia sikuwa na knowledge...ila kama ulikuwa na vilaki vyako tu, utajinasisha na utafungwa.
Ndugu tutajie akaunti namba yako tutakusaidia
Duuh, itakuwa mbaya sana.Kuna mwanasheria humu JF anaitwa ruttashobolwa akija atakupa ushauri wenye busara. Ingawa mimi ningeshachukua kwani kwa kusema tu humu wameshasoma jf na ingawa hujasema ni tawi lipi la NMB, wameshacheck mwenye salio km lako na kesho hakika hutoikuta
Nitamfahamisha meneja, mimi niko NMB ni karani.Kwani utafanyaje kwa mfano????
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.
Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?
Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.
NB kwenye heading ni (50,000,000)
Ndugu tutajie akaunti namba yako tutakusaidia