Milioni Hamsini (50,000,000) zimeingia kimakosa kwenye Account yangu

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,673
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.

Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?

Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.

NB kwenye heading ni (50,000,000)
 
Mpaka kesho saa tatu hazitakuepo.
Ukizikuta zidraw zote uame mkoa, m-50 zinakutoa kabisa kama wewe ni mjanja kama we ni **** usithubutu.
 
mkuu sijui nikushauri nini ila ngoja nikupe mfano kidogo. Kuna rafiki yangu aliwahi kukuta mil 12 kwenye account yake. Naye bila kuchelewa akaitoa na kuitumia then akaachana na hiyo akaunti.
Kumbe ile ela iliingia kwake kimakosa baadae akawa hunted na kukamatwa kwa kosa la cyber crime. Japo mwisho alikuja kuachiwa lakini alikuwa kawekwa ndani kwa week mbili na aliachiwa kwa kurudisha nusu ya ile ela na kuhonga honga sana.
So akili kumkichwa linaweza kuwa ni zali au inawezekana ni shari pia.
 
Zipo toka Ijumaa, leo Alfajir saa 11 na dk 5 nilikwenda kucheki nimeikuta.
 
mkuu sijui nikushauri nini ila ngoja nikupe mfano kidogo. Kuna rafiki yangu aliwahi kukuta mil 12 kwenye account yake. Naye bila kuchelewa akaitoa na kuitumia then akaachana na hiyo akaunti.
Kumbe ile ela iliingia kwake kimakosa baadae akawa hunted na kukamatwa kwa kosa la cyber crime. Japo mwisho alikuja kuachiwa lakini alikuwa kawekwa ndani kwa week mbili na aliachiwa kwa kurudisha nusu ya ile ela na kuhonga honga sana.
So akili kumkichwa linaweza kuwa ni zali au inawezekana ni shari pia.
Hii Comment yako mpaka natetemeka.
 
Unaweza kuzichukua na kuzifanyia shughuli yako. Baada ya uchunguzi polisi watakufungulia kesi ya wizi kwa njia ya mtandao, lakini ukienda mahakaman, utesema mie nimekuta pesa nikatumia. Sijamwibia mtu yeyote. Hivyo itabadilika na kuwa kesi ya madai. Kwa hiyo utalazimika kuzilipa kwa mfumo mtakao kuwa mmekubaliana.

Kisheria huruhusiwi kutumia kitu kisicho mali yako, kufanya hivyo ni wizi. Unatakiwa ufanye utafiti kweli labda kuna ndugu yako kakukumbuka. Fungua jalada(toa taarifa polisi) ili hata siku ukitaka kuzitumia uwe na kinga
 
Kwa mujibu wa sheria za kibenki,makosa yafanywayo na benki hayambani mteja. Hayo ni makosa ya benki. Hupaswi kuogopa. Toa hizo pesa na uzitumie. Utajuta kuziachaacha pesa za bure
 
Unaweza kuzichukua na kuzifanyia shughuli yako. Baada ya uchunguzi polisi watakufungulia kesi ya wizi kwa njia ya mtandao, lakini ukienda mahakaman, utesema mie nimekuta pesa nikatumia. Sijamwibia mtu yeyote. Hivyo itabadilika na kuwa kesi ya madai. Kwa hiyo utalazimika kuzilipa kwa mfumo mtakao kuwa mmekubaliana.

Kisheria huruhusiwi kutumia kitu kisicho mali yako, kufanya hivyo ni wizi. Unatakiwa ufanye utafiti kweli labda kuna ndugu yako kakukumbuka. Fungua jalada(toa taarifa polisi) ili hata siku ukitaka kuzitumia uwe na kinga
Nina uhakika hakuna ndugu yangu wa hivyo, yaani namaanisha
hakuna kabisa.
 
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.

Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?

Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.

NB kwenye heading ni (50,000,000)

kamuulize manager wa benki hapo utapata kila aina ya ushauri.
 
Toka ijumaa chief!! Kuna raia mna upepo wa pesa lkn ndio hivyo tena.
Acha kuogopa uoga wewe unafikiri ukiwatunzia watakupa hata kumi. Anyway changanya na za kwako sasa..
Unaweza kukuta ni upepo wa gerezani.
 
Huwa inatokea.....mara nyingi ni vijana wa IT bank wamepanga dili.............subiria watakupigia simu kukueleza kwamba kuna mchongo umeingia kwako kwa hiyo mpange dili ya kuutoa (infact usitegemee kupata chochote ni wajanja sana) Nina experience 2 za watu ninaowafahamu juu ya hilo
 
Back
Top Bottom