Twilumba
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 11,539
- 12,395
We zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana
Nyange so descouraging!!!!
We zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana
we zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. Ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana
hivi kwa joto la dar, ng'ombe wa maziwa ni biashara inalipa au ni ile kujisikia tu kuwa nimefuga ng'ombe wa maziwa? maana ngombe wa maziwa kwa ukweli wanastawi sana maeneo ya baridi.
Biashara ya duka la Dawa Baridi inalipa sana kama utapata mtalaam wa kukushauri, ingawa kwa sasa naona sheria zimekuwa ngumu but unaweza ukaanza kujua procedures lakini naona inalipa ..... ntawailiana na jamaa yangu mmoja ni mfamasia wa mkoa fulani anipe vigezo then ntakuwasilisha hapa jamvini lakini hii ni hadi kesho!!
nashkuru sana baba ubaya kwa ushirikiano wako.nasubir ayo majibu io kesho.thanx again
yeah uku mbuzi katoliki ni wengi kilo ni 3500 tu.i think ata hii ni biashara nzur ila inahitaji space ya kutosha.Mkuu ng'ombe wa maziwa wanalipa sana hapa dar kuliko unavyodhania. can u belive wahindi wanafuga ng'ombe wa maziwa posta na kariakoo tena magorofani?.
Mama derek kwa songea sina uzoefu nako sana ila nasikia pande hizo mbuzi katoliki wanalipa, mafuso yanakuja huko kusomba kwa wingi,
pia boda boda zinalipa sana mikoani sijui hesabu yenu huko ni ngapi
Mama D Kuna P3 kwenye biashara yeyote tarajiwa ili ufanikiwe!
P1 Product;
Bidhaa gani unataka kuuza! mf huwezi ukaanzisha biashara ya kuuza kiti moto kati ya jamii ya kiislamu au biashara ya kuuza magari kati ya maskini...
P2 Place
chagua eneo muafaka kwa biashara husika usihamehame wala kubadilibadili aina ya biashara, pia uwepo kwenye biashara siku na wakati wote ili wateja wawe na uhakika wa kupata huduma....
P3 Publicity
Matangazo kwamba una bidhaa gani na iko wapi ni muhimu sana sana. Weka bango wafahamishe jamii wewe binafsi au kwa njia yeyote Unauza nini
NB Jumla ya pesa ya mauzo uelewe kwamba sio FAIDA Uelewe ukifuga ng'ombe aidha upate maziwa ukose nyama au upate nyama ukose maziwa huwezi ukapata nyama wakati huo maziwa!
Haiwezekani!
yeah uku mbuzi katoliki ni wengi kilo ni 3500 tu.i think ata hii ni biashara nzur ila inahitaji space ya kutosha.
Kwa bodaboda hesabu yao ni 7000 kwa cku ila inabd kupata mtu mwaminifu sn,weng wao huwa hawalet hela cku zote,sbb kibao kila cku
Mama Derick..... Swali lako linakuwa gumu in so far watu hatujui market ya hapo ulipo....., kuna mtu kasema duka la madawa (je hapo ulipo yapo mangapi, je suppliers watakuwa wapi, je competition ni kubwa au watu wanapendelea miti shamba kuliko hizo dawa?) hapo meaning yangu ni kwamba inategemea na soko...., mfano biashara ya kiti moto huenda ikawa nzuri Dar na isilipe Dubai..., au huwezi ukafanya biashara ya kuuza Ice kwa eskimos...,
Kwahiyo kila biashara inalipa kama kuna soko, unasource ya product nzuri, na unaweza ukauza sawa au chini ya competition na bado ukapata faida, kwahiyo cha maana angalia kitu ambacho hakipo hapo... (if there is a need, then there is an opportunity)..., kuna mtu kasema matunda na mboga mboga, kama hapo hazipo angalia kama unaweza ukazipata nje ya mkoa na kuzileta hapo ulipo ili uuze. Je kuna biashara yoyote hapo ambayo mtu anafanya lakini wewe unaweza kuifanya bora...., (mfano saloon ya kusuka au kinyozi, unaweza ukawa unaleta products chache kutoka dar, ukipata msusi mzuri watu watakuja), au unaweza ukawa mfugaji..,
Je una skills zozote, mfano mapishi (unaweza ukapika keki) na kuzisambaza kwenye maduka na kuuzia watu. In short hapa utaona biashara yoyote unaweza ukafanya, na kufanikiwa kwako sio kwa sababu fulani na yeye amefanikiwa ni management yako, anything you do can work better or worse kutokana na commitment sio sababu biashara fulani ni nzuri na nyingine ni mbaya.
Kwahiyo Information is the key..... Unajua ni wapi unaweza ukapata products kwa bei rahisi ambazo zina soko hapo kwako
Au una skills zozote mfano kusuka au kupika? au unaweza kupata msusi au kinyozi mzuri ukamuajiri kwenye saloon
Au je una good people skills na marafiki ambao unaweza ukawauzia bidhaa (mfano nguo na urembo) ambavyo unaweza kuagiza kutoka dar
Au ukizunguka mjini biashara gani unayoiona unadhani unaweza ukaifanya bora zaidi kuliko inavyofanywa sasa hivi
Je sehemu ulipo kuna shida ya bidhaa gani au watu huwa wanasumbuka sana kutafuta bidhaa gani
The list is endless..
By the way kuna jamaa yangu ni Wakala wa MPESA ni biashara yenye faida ndogo sana lakini its all about volume..., je kuna mawakala wa hii kitu huko, na je kuna customers wengi wa kutosha, nadhani alianza na mtaji wa 3 m na yeye am not sure lakini faida ni ndogo but he seems happy with it
mama derick... je songea juices za concentrates kama zinazokua packed kwenye cups kama za METL zinapatikana.... kuna machine ndogo (semi automatic sealing machine) yaku seal juice kwenye cups kama hizo za METL ....zinapatikana china kwa bei ndogo sana...halafu utanunua juice concentrates with different flavour from anywhere pamoja na cups and seal film zitatoka china... ukapack na ku seal na kuuza katika mji mzima wa songea... ukaipa brand name ya derick juices.... budget yako ni nzuri kwa mradi huu... ni PM nikutumie more details pamoja na photos na machine particulars uamue kusuka au kunyoa bure kabisa
View attachment 21901
something like this
Mama Derik, kule Njombe maeneo ya Chaugingi kuna kiwanda kimoja cha kanisa karibu na ofisi za halmashauri ya mji wa Njombe. Wanatengeneza chupa za plastic na wanauza maji swafi ya kunywa kwenye chupa za plastic.
Ushauri wangu kama mdau alivyodokeza hapo juu nunu kifaa cha kufungia chupa za plastic na kisha wasiliana na wakala wa juice uwe unajaza kwenye chupa za plasic na kuweka brand name ya biashara yako. Usisahau kupitia kwa idara ya afya wa mji ili wahakiki ubora wa bidfhaa yako.
Mwanzo mgumu lakini subira yavuta kheri, kwa mtai wako ukiwa mstahimilivu utafika mbali. Njombe na Songea si mbali.
Kumbuka biashara si kuiga ya fulani, hapa wadau wametoa mapendekezo mazuri, buni yako ili uwe na soko zuri, na wengine watakapofunguka akili kuiga we utakuwa umeshafika mbali na kuteka soko tayari.
Ishaallah
Nyange we vipi? Mama Derick baadhi ya watu watakukatisha tamaa lakini usitishike kwani inawezekana, muhimu ni kuweka nia , kisha ni kuangalia kuna opportunity gani kama alivyokushauri Prime Dynamics, msingi wako kweli ni mdogo kwa hivo ni muhimu katika chochote kile utakachofanya inabidi uwajibike wewe mwenyewe (Front line)We zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana
We zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana