Mila na Desturi na Dhulma za familia

Catrthbertl nende kwenye serikali za mitaa kule kijijini uongee nao waeleze hali halisi ninauhakika watakusaidia. kwani kwa wachagga ni lazima kwa kule kijijini uwe na boma hasa kwa mwanaume. wanaokuambia uondoke ukatafute sehemu nyingine me naona kwako itakuwa ngumu. Utaenda kunywea kisusio wapi?

Zaidi wachaga ukifa lazima ukazikwe uchagani we utazikwa porini ndugu? Aisee babaangu usikubali Pambana upate haki yako eti!
 
Ndugu yangu,
Nunua amani kwa gharama yoyote na sio kihamba kwa gharama kubwa. Mwambie mama akubali baranara ipite pale kwenye shamba lenu hata kama bado ni dogo. usipofanya hivyo vita itaendelea na hapatatosha!!
Mimi pia nimeipitia hiyo hali. Baba alipofariki mama mdogo na wanae waliturusha shamba la ekari 10. Tulisamehe na tukajitahidi kusoma na sasa tuna mashamba mara kumi ya hilo. watoto wa huyo mama ni wavuta bangi na wachovu wakubwa!!! Achana na kihamba hicho wachukue kama watatjirika!!

Mshola, asante sana kwa kunipa faraja ndugu yangu, mimi katika maisha yangu naombaga mungu anipe amani na sio utajiri au mashamba kama hivyi tunavyo gombana kwa kitu kidogo kama hicho ambacho kinatishia hadi maisha ya mzazi wangu.
 
Catrthbertl nende kwenye serikali za mitaa kule kijijini uongee nao waeleze hali halisi ninauhakika watakusaidia. kwani kwa wachagga ni lazima kwa kule kijijini uwe na boma hasa kwa mwanaume. wanaokuambia uondoke ukatafute sehemu nyingine me naona kwako itakuwa ngumu. Utaenda kunywea kisusio wapi?

Zaidi wachaga ukifa lazima ukazikwe uchagani we utazikwa porini ndugu? Aisee babaangu usikubali Pambana upate haki yako eti!

REOLASTON, wewe ndie umenilewa 100% kusudio langu la kutaka haki yangu, kwa mshanga yoyote yule ni lazima uwe na boma lako pale hata kama utakuwa unatembelea huko christmas kwa christmas, swala la kuzikwa huko huo ni mtizamo wa mtu binafsi me hata ukinizika porini ni sawa tu,ilimradu mungi ajinijalia kupata watoto,wototo wangu wajue sehemu baba yao alipotokea n'k.
 
Shukran ndugu yangu, kuhusu kichwa cha posting yangu naona ni sahihi kabisa maana sisi wachaga tumekuwa ni watu wa dhuluma sana hasa kuhusu maswala ya ardhi kiasi kwamba watu wanafukia atua ya kutoana roho.

Na shukuru kwa ushauri wako.

Ndugu yangu, pamoja na kwamba unapinga kubadili heading ya post yako kwa sababu tu ya kudai wachaga ni watu wanaodhulumu sana ardhi, utakubaliana na pia wachaga hao hao ndio wasionyimana njia(mbenge)za kuelekea majumbani mwao pamoja na udogo wa ardhi zao? Ulishawahi kusikia wapi mtu wa maeneo kama hayo ya kwenu kamnyima mwingine sehemu ya kupita ili afike kwake. Kule mashamba hayakupimwa ili kuacha nafasi ya walio nyuma ya nyumba za wengine waweze kupita. Swala hapa ni mama yako kunyanyaswa au ni kutoa njia kwa nduguyo?
 
Nakuunga mkono Kanda2 ..nilipoona kichwa cha habari nilidharau hata kusoma maudhui maana nilijua ni yale yale ya ukabila.
Mtoa mada ushauri wa bure ni kuwa siku nyingine ukitaka usaidiwe tena kwa haraka usiweke vichwa vya habari vyenye kugawa watu... nenda moja kwa moja kwenye kiini.Ukweli ni kuwa una hoja nzito au una ishu inayohitaji msaada ila umekosea kuiweka.Unapaswa kuzingatia yafuatayo katika kutafuta haki yako:
1. Ni bahati mbaya sana sasa nyie mnalipa kwa makosa aliyoyafanya baba yenu - kutelekeza shamba lake kijijini na kuzamia mjini.Kama unavyojua- asiyekuwepo mara nyingi husahaulika na lake linakuwa halipo.Hata kisheria ukitelekeza ardhi kwa kipindi fulani unapoteza haki kwenye ardhi hiyo.( kwa wale wenye ardhi zilizokaa bure - mnaohodhi mnatakiwa kuweka ushihadi kuwa mpo au mtarudi)
2.Hilo la kunyanyaswa na huyo baba yenu mkubwa pengine ( sina uhakika) alipokuwa kifungoni,nduguye ambaye ni babako naye hakuijali familia aliyoiacha nyuma, au wala hakujali kwenda kumtembelea gerezani.Na kwa binadamu wengi, muosha huoshwa! Anawafanyizia hayo yote kama kisasi.
3. Bila kuingia kwa undani sana,naungana na Mzalendohalisi kuwa maisha yapo popote na si lazima mkae hapo Machame Nkuu... kwanza wewe sasa ni kijana wa umri wa kutosha..toka katafute maisha pengine utafanikiwa na hata utawasaidia ndugu na mamako.

WomenofSubsatanc. Ya kutelekeza yanatoka wapi? Hawa si walipewa kasehemu kadogo kama adhabu ya mzazi wao kutotembelea nyumbani? Sasa adhabu gani hiyo isiyoisha? Aliyetelekeza si ameishaondoka? Mke wake na watoto wake wana kosa gani? Mbona mnataka kuendekeza udhulumati?

Hawa jamaa waende ardhi wakapimishe eneo lao. Wajenge uzio kuzunguka eneo lao. Kama ndugu zao wanataka sehemu basi waongee nao kibiashara.

Kwa sasa hivi waende kwenye sheria. Wakatoe ripoti polisi kuhusu vitisho na unyanyasaji. Hatuwezi kuruhusu vitendo kama hivi kwa namna yeyote. Waachane na hao wazee wa ukoo. Mambo yote kwa kaizari.

Amandla...........
 
Jamani mtoa mada yuko sahihi - ingawaje SIO WACHAGA WOTE ila mchaga KIHAMBA anaona kama ndio Mungu kwake - Nina ushahidi - nilinunua eneo na linapakana na mama wa Kichaga - yaani nilimwomba atoe sehemu kidogo tutengeneze barabara - mimi kidogo na yeye kidogo - LO alikataa kabisa - nikamwomba nimlipe basi hata hela kidogo ALIKATAA - mwisho niliuza eneo - nilishangaa sana - sasa MCHAGA MTOA MADA AMETUAMBIA WAKO HIVYO - SIJUI LABDA KWELI - Hata hivyo namshauri hicho kihampa kidogo alichopata ajenge hivyo hivyo - barabara atoe pia - kwani mwisho wa yote - TUTAVIACHA HAPA HAPA DUNIANI - BORA AMANI KULIKO UGOMVI
 
Ndugu yangu, pamoja na kwamba unapinga kubadili heading ya post yako kwa sababu tu ya kudai wachaga ni watu wanaodhulumu sana ardhi, utakubaliana na pia wachaga hao hao ndio wasionyimana njia(mbenge)za kuelekea majumbani mwao pamoja na udogo wa ardhi zao? Ulishawahi kusikia wapi mtu wa maeneo kama hayo ya kwenu kamnyima mwingine sehemu ya kupita ili afike kwake. Kule mashamba hayakupimwa ili kuacha nafasi ya walio nyuma ya nyumba za wengine waweze kupita. Swala hapa ni mama yako kunyanyaswa au ni kutoa njia kwa nduguyo?

Tatizo sio kunyimana barabara ndugu yangu,tatizo ni kwamba wao walikuwa na sehemu yao ya kwenda kwenye hicho kiwanja chao lakini wakajenga kwa mbele na kuzungushia ukuta,sasa wanakuja kwetu wanataka barabara ya kupitia iliwajenge huko,wakati wao wameziba njia wenyewe na sasa wanalazimisha wapewe barabara.hii ni haki kweli?
 
WomenofSubsatanc. Ya kutelekeza yanatoka wapi? Hawa si walipewa kasehemu kadogo kama adhabu ya mzazi wao kutotembelea nyumbani? Sasa adhabu gani hiyo isiyoisha? Aliyetelekeza si ameishaondoka? Mke wake na watoto wake wana kosa gani? Mbona mnataka kuendekeza udhulumati?

Hawa jamaa waende ardhi wakapimishe eneo lao. Wajenge uzio kuzunguka eneo lao. Kama ndugu zao wanataka sehemu basi waongee nao kibiashara.

Kwa sasa hivi waende kwenye sheria. Wakatoe ripoti polisi kuhusu vitisho na unyanyasaji. Hatuwezi kuruhusu vitendo kama hivi kwa namna yeyote. Waachane na hao wazee wa ukoo. Mambo yote kwa kaizari.

Amandla...........

Ahsante kwa kunielewa na kuniunga mkono.
 
Jamani mtoa mada yuko sahihi - ingawaje SIO WACHAGA WOTE ila mchaga KIHAMBA anaona kama ndio Mungu kwake - Nina ushahidi - nilinunua eneo na linapakana na mama wa Kichaga - yaani nilimwomba atoe sehemu kidogo tutengeneze barabara - mimi kidogo na yeye kidogo - LO alikataa kabisa - nikamwomba nimlipe basi hata hela kidogo ALIKATAA - mwisho niliuza eneo - nilishangaa sana - sasa MCHAGA MTOA MADA AMETUAMBIA WAKO HIVYO - SIJUI LABDA KWELI - Hata hivyo namshauri hicho kihampa kidogo alichopata ajenge hivyo hivyo - barabara atoe pia - kwani mwisho wa yote - TUTAVIACHA HAPA HAPA DUNIANI - BORA AMANI KULIKO UGOMVI

BORA wewe umejionea mwenyewe kupitia huyo jirani yako,
ni napo sema kuwa wachagga ni wa dhulumati wengi wao swala la ardhi wako radhi undugu ufe au mku mtoa mtu roho kabisa me ndio nime kulia kule na nimeshuudia vitendo hivi kwa watu wengine na sasa ndio vipo kwangu.
 
Tatizo sio kunyimana barabara ndugu yangu,tatizo ni kwamba wao walikuwa na sehemu yao ya kwenda kwenye hicho kiwanja chao lakini wakajenga kwa mbele na kuzungushia ukuta,sasa wanakuja kwetu wanataka barabara ya kupitia iliwajenge huko,wakati wao wameziba njia wenyewe na sasa wanalazimisha wapewe barabara.hii ni haki kweli?

Hivi wanachotaka ni njia au barabara!
 
Carthbert,

I like your spirit not only in defending what you believe is rightly yours, but thinking about the future. to me it seems Kihamba is not only a space to live, you believe is an identity and passage to generation.

Ningekuwa najua kesi yako kwa undani, na kusikia maelezo ya upande wa pili ningekwambia what legal procedures you should follow. Since i don't know your case my advise is limited. However, there are few places you could go: Baraza la ardhi la wilaya, ambapo unapaswa kupeleka kesi kwenye serikali ya kijiji kwanza.Serikali ya kijiji ikifikia maamuzi ambayo hujaridhishwa nayo unakwenda baraza la ardhi la kata!

Pia unaweza kuwasiliana na Shirika la HakiArdhi, wakakupa mwongozo, unawezaje kusukuma kesi yako kupitia vyombo vya sheria.

Lakini kabla hujafika mbali ni vyema uhakikishe kwamba unawasiliana na familia yako, na mkuu wenu wa familia anaridhia kwamba mmeshidwa kuyamaliza katika ngazi ya familia.
 
sasa sii kama hapatoshi sii mhamie sehem zingine za jamhuri? Morogoro, Tanga kuna mapori tu!!

Kwa nini mnataka kubanana hapo?

Swala sio kuhama tu, mbona tulipigani uhuru ili kuweza kumiliki ardhi yetu? Kwahiyo, mataifa ya kigeni ya kija na kutuambia wanataka tanzania yetu, tutahamia kenya kwa sababu wanamapori mengi? Nadhani utasema hapana, na kama ndivyo, mwache kijana aumize kichwa na mapenzi ya ardhi yake. Kwani Kuitunza nchi lazima ujue kuionea uchungu, kama usipoonea uchungu ardhi yako, utalindaje nchi yako?
 
Carthbert,

I like your spirit not only in defending what you believe is rightly yours, but thinking about the future. to me it seems Kihamba is not only a space to live, you believe is an identity and passage to generation.

Ningekuwa najua kesi yako kwa undani, na kusikia maelezo ya upande wa pili ningekwambia what legal procedures you should follow. Since i don't know your case my advise is limited. However, there are few places you could go: Baraza la ardhi la wilaya, ambapo unapaswa kupeleka kesi kwenye serikali ya kijiji kwanza.Serikali ya kijiji ikifikia maamuzi ambayo hujaridhishwa nayo unakwenda baraza la ardhi la kata!

Pia unaweza kuwasiliana na Shirika la HakiArdhi, wakakupa mwongozo, unawezaje kusukuma kesi yako kupitia vyombo vya sheria.

Lakini kabla hujafika mbali ni vyema uhakikishe kwamba unawasiliana na familia yako, na mkuu wenu wa familia anaridhia kwamba mmeshidwa kuyamaliza katika ngazi ya familia.

Ahsante sana ndugu kwa ushauri wako,nime zungumza na watu wameniambia kuwa Serikali kwa sasa wanatoa hati miliki za kimila,kwa vijiji vyote tanzania hivyo wameni shauri niende kwanza kwenye office za wilaya nika shughulikie swala hilo.
 
Swala sio kuhama tu, mbona tulipigani uhuru ili kuweza kumiliki ardhi yetu? Kwahiyo, mataifa ya kigeni ya kija na kutuambia wanataka tanzania yetu, tutahamia kenya kwa sababu wanamapori mengi? Nadhani utasema hapana, na kama ndivyo, mwache kijana aumize kichwa na mapenzi ya ardhi yake. Kwani Kuitunza nchi lazima ujue kuionea uchungu, kama usipoonea uchungu ardhi yako, utalindaje nchi yako?

Petu Hapa,

Land pressure ndugu! Kama ni eneo la heka 1 na ana watoto wadogo wakiume watatu..sasa baadaye na hao watoto watagawiwa nini?

Haina haja kubanana banana wakati Jamhuri ina maeneo mengi tu na makubwa!
 
Ndugu Carthbertl pole sana na yaliyokusibu, mnalipa dhambi aliyofanya Baba yenu kutokumhudumia Babu yenu. Kuna ushauri hapa unatolewa kuwa ni vizuri kuhama, lakini kuhama sio kitu rahisi hata kama Tanzania ni kubwa, kwenda kuanza maisha sehemu nyingine ni ngumu sana na unapokuwa hauna mtaji. Pia kama ulivyozungumza, kwa mchaga kukosa eneo uchagani ni kudhalilika kwa hali ya juu.

Sasa kwa ushauri wangu, hivyo vitisho Mama yako anavyopewa lazima viwepo kwa kumbukumbu. Sio lazima kwenda kuripoti polisi kwanza, lakini jaribuni kuripoti katika Serikali ya kijij, mtaitwa kusuluhishwa, na hiyo ndio kumbukumbu. Wakizidi ni vizuri mkaripoti polisi, manake hayo manyanyaso ina maana wanawaona sio ndugu tena. Kama mtu Baba yako mkubwa aliwahi kumfukuza Mama yako kwa Panga, na Mama yako mkubwa anamtukana Mama yako na kumtishia maisha hapo hakuna usalama. Ni bora kushitaki wajue kuwa kuna watu wanajua vitisho vyao ili hata waogope kufanya jambo baya zaidi.

Kuhusu ardhi, bado unatakiwa kuitumia Serikali ya kijiji, sijui kama nao wataegemea wapi?, lakini kama utawaeleza yote uliyoeleza, na ikawa kweli mnaonewa. Sidhani kama hao ndugu zenu wataruhusiwa kujenga barabara eneo lenu dogo, wakati eneo lao ambalo wangepitisha barabara pia wamejenga. Huwezi kukubali kudhulumiwa kiasi hicho, jaribuni kushitaki ili liwe linaongelewa, kiasi fulani wataogopa kuliko kukaa kimya.

Nikutakie kila jema katika kupigania HAKI.
 
Ahsante sana Bw.Mfumwa.
 
Petu Hapa,

Land pressure ndugu! Kama ni eneo la heka 1 na ana watoto wadogo wakiume watatu..sasa baadaye na hao watoto watagawiwa nini?

Haina haja kubanana banana wakati Jamhuri ina maeneo mengi tu na makubwa!

Mzalendo halisi,

kama anawatoto watatu wa kiume. watakapo kuja kukua, ardhi anaachiwa kaka wa kwanza ama mdogo mtu wa mwisho kutokana na mila ya kabila au familia iliyopo.

Kijana anavyongangania ardhi, si swala la nafasi ya kujenga nyumba tu, ila ni utambulisho wa koo yake. Na vitukuu vyake vitatambua baba alitokea wapi, na mwenyezi mungu akiwajalia hata kichagaa watajua kuongea.

Swala ya ardhi, sio swala ni kubwa kiasi gani, mbona mjini tunabana kwenye robo heka, na watoto saba. Watoto wakikua wanaenda kutafuata kilichochao, inapofika, miradhi inagaiwa ikishindikana wanapiga bei nyumba.
 
POle sana ndugu yangu.Nadhani tatizo ulilonalo tunalo Watanzania wengi sana,familianyingi zinakumbwa na matatizo haya.Nadhani ni vizuri ukafuata ushauri wa Bwana Petu Hapa kama alivyotoa.jitahidi kupata usuluhisho ndani ya familia,kwani pamoja na kuwa ni tatizo la kisheria ulilonalo lakini kwa jamii zetu za kitanzania na kiafrika kwa ujumla tunaanzia kutafuta usuluhisho katika familia.ikishindikana basi fuata ngazi zinazofuata,nenda serikali ya kijiji na jaribu kuwasiliana na mashirika ya ushauri wa kisheria hasa sheria ya ardhi kwani ni tatizo kubwa sana kwa jamii yetu.
Ningependa pia kuongelea swala jingine hapa,najua kuwa jamii zetu zinaishi kwa kufuata mila na utamaduni kufuatana na makabila tofauti.lakini kwa ulimwengu wa leo inabidi kujenga utamaduni mpya pia, hasa katika swala la urithi.inabidi wazazi kujifunza kuandika wosia kabla ya kufariki,najua wengine wanasema ni uchuro,lakini si swala la uchuro.ni swala la kuhakikisha kuwa unaacha familia yako kwa amani pale wewe utakapokuwa haupo tena duniani.pia inabidi sheria zetu za nchi zinazohusu mirathi zipitiwe tena ili tuweze kufafanua hasa what part does the traditional laws play katika sheria za nchi.najua hili ni swala ambalo linahitaji mjadala mkubwa sana labda hapa si mahala pake.
kwa kumalizia, pamoja na kutoa pole kwako ndugu yangu ningependa kusema kuwa tulioelimika kidogo tujaribu kuelimisha wanafamilia wetu ili migongano kama hii isiweze kutokea.Kikubwa kwa kweli inabidi tujifunze kuandika wosia ili kulinda familia zetu....
 
Ndugu zangu wanaJamii.

Napenda kutoa shukrani zangu kwenu kwa jinsi mlivyo jitolea mda wenu na kutembelea thread hii, nimefarijika sana kwa ushauri wenu ambao kila mtu amenishauri kwa jinsi ambayo ameguswa na maelezo yangu, na ushauri wenu nimeupokea na tayari nime ufanyia kazi.

Ndugu zangu wanajamii, kutokana na ushauri wenu na mtizamo wangu nimeonelea hili jambo lisiniumize kichwa sana, hivyo nimeongea na mama na kumwambia kuwa swala la yeye kutishiwa maisha na kutukanwa a-ripoti kwa mwenye kiti wa kijiji, maana nikisema tu ripoti polisi itakuwa nime jenga chuki ya milele na hawa ndugu zangu, kama wata endelea na vitisho vyao ndio itatulazimu kupeleka swala hili polisi.

Ahsanteni sana ndugu zanguni na mbarikiwe sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom