Shelute Mamu
Member
- Mar 17, 2009
- 37
- 1
Inasikitisha kuona kuwa mpaka leo hii kabila la Kichagga linawakandamiza wanawake katika familia zao. Wiki iliyopita nilishuhudia familia moja ikimfukuza dada yao ambaye hakubahatika kuolewa na kulazimika kuendelea kukaa kwenye mji wa wazazi wake. Lakini kaka zake kwa kushirikiana pamoja walimlazimisha kuondoka pale nyumbani pasipo kujali atakwenda kuishi wapi? na kwa nani! Si huyu tu bali wako wengine ambao wamefukuzwa nyumbani kwa kisingizio kwamba hawajaolewa na pale siyo kwao. Wanawake wasioolewa wanaitwa (WALIFU) kwa kichagga cha SIHA.
Lakini kinachosikitisha zaidi Wazee na Jamii ya SIHA inakubaliana na jambo hili. Nafikiri sasa umefika wakati kwa jamii kuondoa hii mila potofu ya unyanyasaji wa jinsi hii. Naamini ndani ya Jamii Forum kuna Waandishi, Wanasheria naomba wasaidie suala hili.