Mil. 90 Zinahitajika kuokoa Uhai wa Dr. Ulimboka

MAELEKEZO RASMI YA KAMATI KUHUSU UCHANGIAJI WA FEDHA ZA MATIBABU YA DR.STEVEN ULIMBOKA.

Baada ya majadiliano kati ya familia ya Steven Ulimboka,kamati ya jumuiya ya madaktari na MAT.Zifuatazo ni namba za mawakala zitakazotumika kuchangia.
MPESA 31915
TIGOPESA 05416.
CHITAGE.

asakuta same, tuthibitishie kuwa zitafika kunakotakiwa bila mawaa plse.
 
Last edited by a moderator:
Mi nadhani wakati watanzania wanachangia, Madaktari waendelee kuwahudumia wagonjwa wanaoweza kutibiwa hapa hapa nchini haitakuwa kitu cha msingi watanzania wakahangaika na mtu mmoja wakati Mamia ya Wagonjwa wanakufa mahospitalini.

Halafu ni kweli Madaktari wanalamika dawa hakuna hospitali au ni pendekezo lao la kulipwa Mshahara wa Milioni 3.5 kwa mwezi, katika hili nawaelaza Madaktari wafanye analysis waje na data kama inawezekana ila
Prof analipwa 2.5M ambaye anamfundisha Daktari.

Mbunge 2.5M. Nakushauri kaombe Salar slip ya Mbunge wako wa Jimbo atakupa
Hlafu 60% ya Madai yametekelezwa hata lile mlilotaka kukopeshwa Magari, Posho kuongezwa yametekelezwa, na Mashine mliyokuwa mnahitaji Itengenezwe Wataalam wanakuja kutoka kule mashine ilikokuwa imetengenezwa, Mlikuwa hammtaki waziri ametotolewa ten pamoja na Katibu Mkuu ndugu Blandin Nyoni waelezeni watanzania Ukweli wa Madai yenu kupitia vyombo vya Habari kwa sababu watanzania ndio waajiri wenu Mnalipwa mishahara kodi za Watanzania.

umechangia ngapi mkuu?manake unaonekana kama kibosile wa magamba.
 
Nimesikia bungeni madiwani wapandishiwa posho zao. Je wametoka kiasi gani na kufikia kiasi gani. Na je wako wangapi tanzania?
 
"Serikali kwa unafiki wao walijipendekeza eti wapo tayari kugharimia matibabu ya Dr. Ulimboka, madaktari wamegoma kuwa hawawezi kupokea fedha kutoka kwa Yuda Eskarioti"

wasijempa Polonium bure hao madhalimu!
 
Serikali si ilisema ita gharamia matibabu yake? Au wame badilisha mawazo?

We weweee hatutaki kabisa hizo hela za mafirauni MAGAIDI zitamfanya asipone buree..wakammaliza nazo kbsaaa tutachanga wenyew km Mungu kamlinda na ataeendelea mlinda..waache hao mashetani CCM wajipatie laana na pesa zetu za kodi..
 
Hali ya Dr. Ulimboka kwa sasa sio private issue na wala sio issue ya wanataaluma wenzake ni jambo la watanzania wote, Bunge limeshindwa kujadiri, Wizara yake ya Afya imeshindwa hata kutoa tamko, Ofisi ya waziri Mkuu inayoshughurikia madai ya Madaktari ya kuboresha mazingira ya kazi pamoja na kuboresha huduma za afya kwa ajili ya watanzania. Walio baki ni Raia wa Tanzania, Tunaomba tushirikishwe ipasavyo, Naona ushirikishaji wa wananchi kutoka kwa madaktari sio mzuri sana. Madaktari semeni, kuweni wazi mnataka msaada gani kutoka kwa RAIA, tupo tayari kufanya lile tunaloweza kama halitawezekana tutawaambia hilo tumeshindwa. Tunaomba mpango wa namna michango inavyoweza kukusanywa mara moja kuweza kumsaidia Dr. Ulimboka kutibiwa India.

kweli kabisa. Wananchi ndio tegemeo kubwa kwa uli.
 
Hivi watanzania wameifanya India kuwa ni tenderer wa kuwatibu! Hakuna matibabu sehemu nyingine duniani isipokuwa India tu? Je, ni wakazi wa dunia nzima wanatibiwa India au ni watanzania tu?

mheshimiwa nzowa kule uhindini gharama zake ni nafuu sana thats why sirkali imepitisha wabongo twende huko. ila watu km kina mamvi and chenge wao wanaenda jerumani na sehemu nyinginezo expensive excluding uhindini. haya ndo maisha ya bongo sasa.
 
Kuna nyuzi nyingine wameandika million sitini na nane (68,000,000) hapa tisini (90,000,000). Bongo Bingo.
Hicho ndicho kiwango kilichosomwa na ITV kwatika taarifa yao ya saa 2 Usiku, Tsh.Mil.90
 
Mi nadhani wakati watanzania wanachangia, Madaktari waendelee kuwahudumia wagonjwa wanaoweza kutibiwa hapa hapa nchini haitakuwa kitu cha msingi watanzania wakahangaika na mtu mmoja wakati Mamia ya Wagonjwa wanakufa mahospitalini.

Halafu ni kweli Madaktari wanalamika dawa hakuna hospitali au ni pendekezo lao la kulipwa Mshahara wa Milioni 3.5 kwa mwezi, katika hili nawaelaza Madaktari wafanye analysis waje na data kama inawezekana ila
Prof analipwa 2.5M ambaye anamfundisha Daktari.

Mbunge 2.5M. Nakushauri kaombe Salar slip ya Mbunge wako wa Jimbo atakupa
Hlafu 60% ya Madai yametekelezwa hata lile mlilotaka kukopeshwa Magari, Posho kuongezwa yametekelezwa, na Mashine mliyokuwa mnahitaji Itengenezwe Wataalam wanakuja kutoka kule mashine ilikokuwa imetengenezwa, Mlikuwa hammtaki waziri ametotolewa ten pamoja na Katibu Mkuu ndugu Blandin Nyoni waelezeni watanzania Ukweli wa Madai yenu kupitia vyombo vya Habari kwa sababu watanzania ndio waajiri wenu Mnalipwa mishahara kodi za Watanzania.

Jimy,
Hata kama una chuki binafsi na madaktari au una jazba kutokana na uamuzi wao wa kugoma basi uwe mkweli kwa taarifa unazozitoa. Inawezekana kuwa mbunge mshahara wake ni hizo fedha ulizoonyesha lakini mbunge ana posho nyingi sana kiasi kwamba kile anachopeleka nyumbani ni kasma ya nguvu inayokadiriwa kufika milioni 10.
Kwa upande wa maprofesa hizo data ulizotoa labda ni za miaka kumi iliyopita. Sasa hivi maprofesa mshahara wao ni kuanzia ni TZS 4,016,300/= kwa profesa mshiriki (au wenyewe wanaita Associate professor) na Profesa kamili ananyaka 4,203,300/= au 4,390,300/=. Kwa upande wa shahada ya kwanza tutorial assistant anachukua kati ya TZS 1,188,100/= na 1,372,600/=. Kwa utaratibu wa zamani (sijui kama sasa bado unaendelea) waliosomea MD walikuwa wanaanza kama Wahadhiri wasaidizi na kwa sasa hao mishahara yao ni kati ya 1,482,800/= na 2,078,100/=. Kwa hiyo kama serikali ingetumia busara kidogo tu na kuwaajiri hawa sawa na wanataaluma kutokana na unyeti wa kazi zao kwa uhai wa Watanzania wangeweza kabisa kuwapa mshahara wa TZS 3,500,000/=. Hata kama ingekuwa pungufu ya hapo lakini sio laki tisa. Ina maana kuwa class mate wako aliyebaki MUHAS akaajiriwa kama mhadhiri msaidizi na wewe unayeajiriwa kuwa Daktari kule Ikwiriri tayari mnapishana zaidi ya laki tano. Ikiwa tuna madaktari (MD) wasiozidi 2,500 malipo yao yanawezekana kabisa. Kwani unadhani zinahitajika fedha kiasi gani? Mbona serikali haisemi? Kwa taarifa yako kama kwa wastani kila daktari angelipwa 7,000,000/= (mara mbili ya madai yao maana kuna masinia) basi kwa mwezi serikali ingetumia TZS bilioni 17.5 sawa bilioni 210 kwa mwaka ambayo ni sehemu ndogo sana ya posho za vikao serikali, kwenye mashirika ya umma na serikali za mitaa. Nina uhakika kuwa malipo halisi yatakuwa pungufu ya haya na yanawezekana. Hii ingeonyesha jinsi serikali ilivyo makini na inavyojali uhai wa Watanzania lakini sasa imeonyesha kinyume chake ndio maana haijali kuona mtu ameuwawa, uhai kwa serikali hii si kitu cha thamani hata kidogo. Je, ni mambo mangapi ya kipuuzi yanayofanywa kwa kutumia fedha nyingi za taifa zaidi ya hizi? Yana umuhimu gani kwetu kama Watanzania?
Ni kuwa tu serikali haitaki na kunapokuwa na watu kama wewe ambaye unaiunga mkono wanafarijika sana maana wajinga ndio waliwao. Hivi kweli ukiwa mgonjwa ukatibiwa na daktari ambaye hajaridhika unadhani utapata huduma inayotakiwa? Walazimisheni, wafukuzeni na muwajengee chuki matunda yake sote tutafaidi. "Mungu hadhihakiwi, kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna"; na kwa nchi au utawala ni hivyo hivyo.
 
Nashauri uwepo uratibu mzuri wa kuchangisha michango. Watanzania tuko tayari kumsaidia Mtanzania mwenzetu atibiwe na kurejea kusaidia maendeleo ya nchi yetu. Mie binafsi niko tayari kutoa 100,000. I just need assurance kuwa fedha ninazochangaa zitamsaidia mtanzania huyu
 
Tutachanga, lakini sasa kwa nini serikali isimplipie kama raia wa Tanzania (siyo kama Dr Ulimboka) wakati wao wamekuwa kila siku wanakimbilia huko India?
 
Wahusika mkumbuke kuweka utaratibu mzuri kwa wale tulio nje ya nchi katika kuchangia tafadhali
 
toka ameanzisha huu mgomo watanzania wangapi wamepoteza maìsha? Asulubiwe
 
Wa Tz wote wanao penda haki hima tuchangie Dr uli akatibiwe tusikubali serikali dhalimu ya ccm iweke mkono wake hapo.
 
Back
Top Bottom