Kiama chaja: Mikutano ya Vyama vya Siasa kuundiwa Kanuni ya Makatazo!

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Wana JF kutokana na CHADEMA kufanya Mikutano yenye Mvuto kwa Wananchi, Serikali kupitia Mamlaka za Juu za (CCM) uongozi zimemuamuru Msaliji(kada wa CCM) wa vyama vya siasa kutengeneza Kanuni itakayokataza vyama vyote vya siasa kufanya mikutano kwa Uhuru(mlengwa ni M4C).

Inadaiwa mikutano hiyo imekuwa ikihatarisha Amani ya Nchi na kuzoa wanachama wa vyama vingine.

Kwa mujibu wa mtoa Nyeti hizi, Msajili atawaita Makatibu Wakuu wote na kuwapa kitabu cha Kanuni ya Mikutano ambayo haitamruhusu mtu asiye wa Mkoa fulani kuvuka mkoa na kuhutubia Hadhara bila kibali maalum cha Msajili.

Haya ni maagizo toka juu.

Nawasilisha
 
wataiona mbombo magamba hata watumie njia yoyote wanayoona inafaa they must knw that the end of their domination in tz is soon to be end up and m4c wil take the position for better lives and management of tanzanians.
 
Kwa katiba ipi ya nchi au sheria ya mtanzania kwenda popote kwenye nchi hii ili mradi havunji sheria imesha kufa,Kwa hiyo serikali inakubaliana na sera ya majimbo je itakuwa hivyo na kwa mwenyekiti wa CCM yaani huu utawala hauna tofauti na ule wa makaburu una nyonga sana haki za wananchi
 
Hii serikali ni ombaomba, na moja ya masharti inayopewa itembezapo bakuli lake, ni kuheshimu utawala bora. Wakileta hii nasi tusisite kuwashitaki kwa hao bwana zao (wafadhili) kwamba wanakiuka haki za binadamu na kutoheshimu utawala bora.
 
Hilo nimeliona leo nilipopita Morogoro.

FFU kutoka Dar wametanda kila kona ya Manispaa kuzuia Mikutano ya CDM.

TAFAKARI: Police wa kulinda mikutano ya vyama hakuna kama alivyodai RPC Moro, lakini wa kuzuia mikutano ya vyama kinzani wapo wa kutosha na nimeshuhudia leo!!!
 
Hiyo haipo wala haiwezekani.Ina maana mwenyekiti au katibu wa chama haruhusiwi kutembelea matawi ya chama?

Huyu msajili akicheza watu watazaa nae.
 
Raisi nae itabidi awe na pass ya kuvuka mkoa.!! ccm wamefilisika ubunifu hadi busara,wanajiona wanahati miliki na nchi hii.
 
Hii ni hatari sana kwa umoja wa kitaifa, nadhani mtakumbuka kauli ya Joshua Nasari pale Arusha hadi akalazimika kuifuta na kuomba msamaha.

Wakileta hili hata watumishi wa umma na viongozi kama wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurungenzi wa halmashauri nk watalazimika kuwa wazaliwa katika mikoa husika.

Tulianza na sumu ya udini, naomba sana hii ya ukabila tuiache kwani hakuna atakayesalimika.
 
Back
Top Bottom