Mikutano ya CDM kufunga kampeni Tengeru na USA

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Updates:
Mkutano umekwisha wakuu, kilichotokea ni historia katika Arumeru watu walikuwa ni wengi haijawahi kutokea na kitu kilikuwa kimeratibiwa vizuri.

Ni wazi ushindi ni kwa Nassari bila chenga.

Nassari anatoa kituko hapa, katika kujibu hoja ya kuwa na mke.

Anasema kwa kuwa Halima Mdee hajaolewa basi wakimuudhi anaweza kumuoa Mdee kisha Aremeru ikawa ina wabunge wawili!!!!!!

Mbowe anasema wanampango wa kupeleka hoja binafsi marais wastaafu ambao wanafanya kazi za chama wasilipwe pension na serikali bali chama.
Slaa atoa tuhuma nzito kuwa leo katika hotel Snow Cret kulikuwa na mkutano kati ya tume na CCM ili kuona jinsi ya kuokoa jahazi.

Vicent Nyerere anasema Wameru wanatatizo moja tu, tatizo lao ni pale wanaponyang'anywa haki haki yao. Anasema haki yao ni Nasari.

WanaJF nitakuwa live kuwaletea bila chenga yatayojiri katika mikutano ya kufunga kampeni ya jimbo la Arumeru. Hivi sasa mambo yanaendelea kwa kuwapika mawakala eneo la USA.
Vitendea kazi vipo vya kutosha kwa ajili ya picha na videos.

Stay tuned,
 
WanaJF nitakuwa live kuwaletea bila chenga yatayojiri katika mikutano ya kufunga kampeni ya jimbo la Arumeru. Hivi mambo yanaendelea kwa kuwapika mawakala eneo la USA.
Vitendea kazi vipo vya kutosha kwa ajili ya picha na videos.

Stay tuned,

Mbona leo ma-reporter wa CDM wamekuwa wapole sana.
 
WanaJF nitakuwa live kuwaletea bila chenga yatayojiri katika mikutano ya kufunga kampeni ya jimbo la Arumeru. Hivi sasa mambo yanaendelea kwa kuwapika mawakala eneo la USA.
Vitendea kazi vipo vya kutosha kwa ajili ya picha na videos.

Stay tuned,
Kila la kheri. Hakika saa ya ukombozi ni sasa.
 
Mkuu hongereni sana bwana, tunasubili kwa hamu picha hizo!
 
Tunashukuru saaana Mkuu,
usisahau ku post na picha ili tuweze kujionea hali halisi eneo la tukio. All the best makamanda wote wa CDM mnaotuwakilisha huko
 
Mbona leo ma-reporter wa CDM wamekuwa wapole sana.

mkuu wala usiwe na wasiwasi na ushindi ...ripoti utaletewa na matokeo kesho saa 3 usiku tayari tutakuwa tushachukua arumeru hilo halina ubishi nawahakikishia wanachadema wote na wale wasio wapenzi ushindi ni wetu wala msiwe na hofu magamba huku hayana chao kabisaaa na mimi naongea nikitokea uwanja wa mapambano arumeru sio hao wanaotaka kujinyonga wakiwa dar hata hali halisi haijui
 
Back
Top Bottom