Mikopo ya Benki; Wanaomba sana rushwa

Ulipewa risiti ya hiyo shs 50000/-?kama ukupewa umeliwa
icon10.gif
fomu ni bure CRDB,wizi mtupu! wanatulipisha shs 30000/- kama legal fee kwa mwanasheria wao wenyewe ambaye wanadili naye,kama una mwanasheria wa kwako wa bure ruksa.Katika organisation yangu wengi wanamlalamikia kwa yule loan officer ambaye yupo responsible na sisi anapenda rushwa sana, ni pale H/House.
Kwani wengine si wamo humu, waambiwe ili waache hako kamchezo ka rushwa.

Renegade,

Loan Officer wa Holland House CRDB anayekwamisha mikopo ya wateja kwa kudai Rushwa..hivi Kimei unalijua hili??

Jina la huyu Loan Officer CRDB ni nani?

Tumshikie basi bango!!!!
 
Siyo hivyo tu wakuu, lakini hata watumiaji wengi wa benki hawaulizi vya kutosha kuzijua benki wanazowekeza fedha zao zina mifumo gani ya kibiashara. Watu wanaamua kuweka pesa zao kwasababu sisizo za kibiashara na kwakulazimishwa either nawaajili wao au na interest za ndugu zao, bilakujua pesa ni "comodity".kama kama komodity zingine ambazo huwezwa mahali zinapotakiwa kupata faida, mfano ukiweka 10,000TSH katika benki fulani, (jina ninalo) baadaya mwaka unakuta balance ni 0TSh unajiuliza nimeweka ile kwangu au wote tupate kitu. Nafikiri yatupasa kubadili mitizamo ya ukuzaji mitaji yetu kwani hatakama ni kamshahara kako wanaweza kukafirisi kote hata kabla hujaaccumulate hivyo bado usipige hatua.
Ni vyema kabla kufungua account waulize products zao, makato yao nafaida utazopata kwakuweka pesa yako kwao na ziainishwe kwenye mkataba unaoutumia kufungulia account.Ni wajanja maranyingi kwenye mikataba haonyeshi maeneo hayo, lakini maranyingi huonyesha kwenye promoseni na matangazo ya kibiashara ambayo huna ground the kisheria kudai. au wanakuonyesha wakati umeshafungua account na wameshaanza kuzitumikisha pesa zako na ndo unashituka, NDO UMELIWA HIVYO!
Vinginevyo tutalia we na mikopo hatupati lakini benki zinazidikufunguliwa." meaning that it is the bsness of profit of which our share as customers is eaten out of businessmind.

Open your eyes and see!
 
Naona kuna tabia inaanza kujengeka kwamba kila lisemwalo baya linashabikiwa, inawezekana nikawa nimekosea, naomba nikusolewe. Kitaaluma ni mwalimu, nataka lifahamike hili kwanza, ili niweze kutoa hoja yangu. Watu wengi nimekutana nao nje ya nchi na hata ndani na hasa vijijini anatafuta huduma fulani kama mkopo. Jambo la kwanza atauliza unamfahamu nani katika taasisi fulani, nahitaji mkopo, eti bila kumfahamu mtu hupati. Ni kwa minajili hii watu hawa hufika benki kuomba mikopo; bila hata ya kujua taratibu na hujifanya wanyonge kiasi wanaonekana wepesi kutoa chochtoe. Wafanyakazi walafi huwaonea hawa sana. Tena kwa bahati mbaya wanaodai rushwa sio wenye kuhusika na uamuzi ila ni watu baki kabisa.

Hoja yangu ni walaji(customers) wanajua kidogo mno kuhusu haki zao na taratibu za huduma wanazohitaji. Mimi nadhani mada ingekuwa jinsi gani mabenki yanavyoweza kushugulikia elimu hii ya haki ya mteja. Kwa uzoefu wangu mabenki ya sasa hatuwezi tukayalalamikia yana wadai rushwa kuliko mahakama. Kule kila kitu ni giza huwezi kujua barua umpe nani, dhamana inatolewa vipi, hujui karani na taarishi ni yupi, hakimu na maofisa wasajili wa mahakama ni wapi, na ukiulilza unajibiwa vibaya. Na kwa kuwa kuna jua kali, uchovu, hasira kwa kuwa ndugu yako yuko rumande, hakuna msaada unaoupata pale, na wote polisi na wafanyakazi wa mahakama hawana aibu kuomba chochote, basi ni rahisi kweli kutoa rushwa pale, hata kama ungekuwa na dhamira kali dhidi yake. Benki hapana.

Na kwako Obseva, kwa nini usitamke tu Benki Ya Biashara (NBC) ni ukweli usiopingika, ukiacha pesa yako muda katika account, huyeyuka na wana maelekezo tosha kabisa.

Naomba kutoa hoja
 
Ndugu zangu yote haya yanatokea kwa sababu vyombo vyetu ambavyo vilitakiwa kufanya kazi yake wamekaa tu ili wapelekewe taarifa mezani. TAKUKURU na N.S. wanafanya nini? Maana ndio taasisi za kuhakikisha ukengeufu huu wanadeal nao sambamba. Kama ni sheria haipo ya kushughulikia rushwa katika taasisi za watu binafsi wapush through demand ya sheria mpya ili iwape nguvu ya kiutendaji. Maana tusisahau haohao wala rushwa kama vyombo vyetu havina taarifa zao sahihi au kuwaimplicate na tuhuma za rushwa ndio kesho wna keshokutwa wataingia kwenye taasisi za umma na kuzitafuna kama mchwa. Mara nyingine ndio watakuwa wabunge wako na bila uadilifu tusitegemee jipya.

Bahati mbaya tuna selikari ya kishkaji hivyo wote wanatenda kazi zao kishjaji
 
Na kwako Obseva, kwa nini usitamke tu Benki Ya Biashara (NBC) ni ukweli usiopingika, ukiacha pesa yako muda katika account, huyeyuka na wana maelekezo tosha kabisa.

Naomba kutoa hoja
Reply With Quote
 
....tuwe more practical na tuache kulalamika sana,ukiombwa rushwa make sure stop ya kwanza ni kwa manager then report TAKURURU,sio lazima uwe na ushahidi wewe ukihisi tuu jamaa anataka rushwa report kwa wakuu wake wa kazi hayo ya evidence watajua wenyewe mbele kwa mbele na uhakika waki report wawili au watatu tuu lazima akomeshwe mtu na rushwa zitapungua,lakini mkibaki kucheka cheka tuu na kuishia kuzitoa mnajiumiza wenyewe!
 
Mikopo nchi hii ni vurugu tupu. Mimi rafiki yangu alihitaji millioni 15 mwaka jana NMB tawi fulani na ilibidi aachie 300 thousand ili mkopo uwe approved pamoja na kutimiza vigezo vyote. Ilimchukua siku tano tu kupata mkopo. Sasa wewe ukijaribu kupitia njia ya haki nakuambia haki ya nani, hutapata kitu hata kama vigezo vyoooooote unavyo.
Huoni wenzio wafanyakazi wamenona tena wanaendesha magari ya wakurugenzi?
Shauri yenu:)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom