Mikopo ndani ya Ndoa

Mwanamke kamili hawezi kuwa na dosari hizo, go on Our contract still exists na ni matumaini yangu Tutakapokuwa wote Valentines day utanipa feedback ya ukweli.

Afadhali maana nilidhani umenipotezea muda bure. . .
 
Inasikitisha sana kuona kuwa wanawake wengi huwa na tabia za hivyo. Zamani nilijua ni uswahili but now imefikia hadi kwa wanaojiita wasomi. Pengine inachangiwa na tabia ya baadhi ya kina baba kutokuwajibika sasa mama anaamua kumfanyizia au nini sijui.

Ila wapo pia kina baba wanaokopa kwa wake zao (mimi nachukia mwanandoa anapokwambia niazime kiasi flani nitakurudishia ilhali anakwenda fanyia kitu cha familia).
 
Tunakurupuka kuoa kwa kucheki bodi tu. Tabia, tabia hasa toka pande za waliotumwa hela. Binti anaulizwa mchumba wako ana duka au kazi gani. Ndoa sio hela ila ni kijisehem cha kuendeshea maisha.ndoa ni wawili wapendano kwa dhati.mtindio wa wazi ndo unatuambia mke awe na digrii kumbe hata gemu bila2
 
Mimi sioni tatizo, kwa mfano mwanamke hana kazi mumewe ndio anaenda kazini, huku nyuma sukari imeisha anaweza mama kununua sukari kutoka kwenye akiba yake binafsi mumewe akirudi anamwambia nilitoa 2000 ya sukari mume anamrudishia au nilitoa 30,000 ya mshahara Hg anarudishiwa.
 
Tusijadili hii ishu kwa wepesi sana.
Ndani ya ndoa kuna mgawanyo wa majukumu na kila mwanandoa huwajibika.
Ikitokea mke/mume anataka pesa za kutimiza yale majukumu yake au anataka pesa kwa kitu fulani, kuna namna mbalimbali za kupata uwezesho kutoka kwa mwenziwe.Mimi kwa mfano, nikihitaji pesa kiasi fulani na kumwahidi mwenzangu kuwa nitamrejeshea, basi nachukulia huo ni mkopo na huwa narudisha.Hata na yeye hivyp hivyo.Ila pale ninapomuomba anipe kiasi fulani bila kuahidi kurudisha basi hiyo ni grant haihitaji kurejesha.Na yeye ni hivyo hivyo.Tusichanganye mambo jamani.
Kwenye ndoa ipo mikopo, ruzuku na grants.
Ikiwa maneno ya rejareja yanatokea, basi hiyo ni tabia mbaya tu ya huyo msema hobyo.Mwanaume ujilaumu kuoa mwanamke mwenye maneno ya ovyo.
 
mbona Ndoa hizi ndo nyingi? Watu wanakopeshana humo balaa...ikitokea ugomvi kidogo utasikia "kwanza nirudishie pesa yangu ya KARO.. We si ndo umenioa???

Akiniambia hayo maeneno, naandika talaka tatu.
 
Tusijadili hii ishu kwa wepesi sana.
Ndani ya ndoa kuna mgawanyo wa majukumu na kila mwanandoa huwajibika.
Ikitokea mke/mume anataka pesa za kutimiza yale majukumu yake au anataka pesa kwa kitu fulani, kuna namna mbalimbali za kupata uwezesho kutoka kwa mwenziwe.Mimi kwa mfano, nikihitaji pesa kiasi fulani na kumwahidi mwenzangu kuwa nitamrejeshea, basi nachukulia huo ni mkopo na huwa narudisha.Hata na yeye hivyp hivyo.Ila pale ninapomuomba anipe kiasi fulani bila kuahidi kurudisha basi hiyo ni grant haihitaji kurejesha.Na yeye ni hivyo hivyo.Tusichanganye mambo jamani.
Kwenye ndoa ipo mikopo, ruzuku na grants.
Ikiwa maneno ya rejareja yanatokea, basi hiyo ni tabia mbaya tu ya huyo msema hobyo.Mwanaume ujilaumu kuoa mwanamke mwenye maneno ya ovyo.

Perfect women.Nafikiri ungeleta thread yenye mada kama hiyo...uwasaidie wadada wenzio
 
Mie naamini vile mtakavoujenga msingi wa ndoa yenu kulingana na vipato vyenu ndivo utakavokuwa,
Kwa mfano nimekulia kwa wazazi wenye ndoa na waajiriwa sijawahi kusia haya mambo ya kukopeshana,kinachotokea walipangiana majukumu kila mmoja alikuwa akitimiza majuku yake ikitokea amepungukiwa mwingine anamalizia na hakuna cha kudai,

Mambo ya shule yote tulikuwa tunadeal na baba ili kurahisisha mama anakusanya mahitaji yetu anapeleka kwa baba yeye anatoa mshiko au mnaongozana kwenda kununua,mambo ya msosi na mambo yote yanayohusu matumizi ya hm tulikua tunadeal na mama saa ingine baba anatoka anauliza km kuna kitu hamna akiambiwa anarudi nacho na halipwi wala kudai,

Siamini ktk kukopeshana ndani ya ndoa kwani tutakuwa ni mwili mmoja na kila kitakachokuwepo na kupatikana ni chetu wote cha msingi kupeana majukumu kulingana na vipato vyetu,vile mme atakavomzoesha mkewe tangu awali ndio itakavokuwa siku zote.
 
i see kuna wanawake wa hivyo

hiyo nyumba si yake na mumewe? Anamkopesha mumewe kwenye matumizi ya nyumba? Mfano anaponunua sukari, mume akirudi anamdai hela ya sukari? Kama ni hivyo huyo mwanamke hajajitambua au hajajua kama yupo kwenye ndoa.

Unless kama mume umemwambiz mkeo akukopeshe kiasi kadhaa utamrudishia, hiyo akikudai umlipe kwa kweli

wanawake wa hivyo wapo, wao chako ni chetu, changu ni changu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom