'Mikopo kwa wanafunzi bado ni tete'

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
'Mikopo kwa wanafunzi bado ni tete' Monday, 13 December 2010 20:43

Hidaya Omary na Mwanaidi Abasi

UPATIKANAJI wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchinio, bado ni tete na jana wanafunzi kadhaa walivamia ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi jijini Dar es Salaam wakilalamikia kucheleweshwa kwa fedha hizo.

Habari zilisema hadi kufikia jana, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro, Chuo Kikuu cha Tumaini na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam, walikuwa bado hawajapata mikopo.

Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na gazeti hili walisema kitendo hicho kimewaathiri kisaikolojia na hata kulazimika kukopa fedha kutoka kwa watu.

Mwanafunziwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwesigwa Christian alisema kuchelewa kwa mikopo hiyo kumemfanya ashindwe kuhudhuria masomo.

"Mpaka sasa hatujapata pesa zetu, jambo linalotufanya tushindwe kuingia darasani kwa kukosa nauli na njaa," alisema Mwesigwa.

Alisema kwa jumla wanafunzi, wamechoshwa na utaratibu wa bodi hiyo katika kutoa mikopo na kuiomba serikali kuingilia kati jambo hilo.

"Kila tukija tunapangiwa tarehe na kupewa sababu zisizokuwa na msingi mara hatujajaza fomu, mara majina hayaonekani hatuelewi kwa kweli,"alisema Jonh Revocatus.
 
Back
Top Bottom