Mikoa ya tanzania now..

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,842
Nasikisikia tu
kuwa kuna mikoa mipya ya Simiyu na Katavi

wakati fulani nilisikia Njombe na Geita pia ni mikoa

sasa kama kuna mtu ana ramani mpya inayoonyesha mikoa yoote mipya ya Tz
na wilaya zake naomba aweke hapa

nina uhakika wengi wetu hatujui mikoa hiyo mipya ndo ipi?

imekatwa katwa vipi kutoka ya zamani...
 
Kaka ramani ni ile ile aliyoiacha mwalimu kwenye zile atlas tulizotumia shule za misingi enzi hizo,kama kuna ramani nyingine basi hiyo ni ya kuchakachua na kwa bahati mbaya mimi tokea mikoa hiyo mipya itangazwe sijaona ramani ya Tanzania ikibadilika hata tukianzia mkoa wa Manyara ambao ulitangazwa enzi za Ben Mkapa kama sijakosea
 
Nilisikia kuna ramani mpya ta Tanzania. Ilitangazwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Kipindi kile mama Tibaijuka alipotoka kule UN kudai ongezeko la eneo la bahari.
 
Ni kweli Tanzania ina mikoa mingine mipya iliyopitishwa na Vasco da Gama asiyeangalia madhara ya kufanya hivyo kiuchumi. Amefanya hivyo kuwapa ulaji marafiki zake. Ila huko tuendako mchezo huu mchafu utaligharimu taifa. Chukulia mfano Mkapa aliunda mkoa wa Manyara kwa maslahi ya Sumaye ambaye hata hivyo Mungu kamchapa kiboko haikuwa kama alivyoona karibu na kupanga. Ningekuwa rais mpya ningebatilisha mikoa hii kwani haikutengenezwa kihalali zaidi ya siasa za maji taka za Chama Cha Mafisadi.
 
Back
Top Bottom