Mikoa mitatu mipya kuanzishwa

Kama kuna mtu anajua mgawanyo ulivyo especially kwa wilaya ya Geita ambayo imekuwa mkoa atujuze kwenye Jamvi!..kuna tetesi nilisikia wanataka kama na geita ziwe kama mkoa mmoja! sasa wakifanya hivyo sijui shinyanga itakuwaje mana ndo walikuwa wanaitegemea wilaya ya Kahama kwa mapato
 
Kigezo kikubwa walicho tumia eti kusogeza maendeleo kwa wananchi kwa haraka vimkoa vidogo vyenyewe wameshindwa kuvipelekea maendeleo ya haraka mpaka kesho vinashika mkia kimaendeleo wananchi wenyewe wanaishi kwa matumaini huduma za muhimu kama maji,shule, dispensary ni za kubabaisha tu nenda huko Lindi na Mtwara kisha safiri Kigoma yaani watawala wetu wanachekesha naona nyuma ya pazia ni kujiongezea ulaji kwa watu frani frani.
 
kati ya mambo yote ya ajabu sielewi kwanini Pwani haigawanywi ili kuongeza eneo la mkoa wa Dar!!! it makes absolutely NO SENSE!!!!!

Mwanakijiji Mkoa wa Iringa ni Mkubwa sana na hata geographical location zake kati ya Wilaya na Wilaya imekaa vibaya sana.I have been kwenye hizi wilaya zote zilizotajwa hapa Makete,Ludewa na Njombe mi kwa kweli naunga mkono suala hili.Ni bora wilaya hizi zipewe hadhi ya kuwa mkoa ili kupeleka kasi maendeleo ya maeneo haya.
 
Mwanakijiji Mkoa wa Iringa ni Mkubwa sana na hata geographical location zake kati ya Wilaya na Wilaya imekaa vibaya sana.I have been kwenye hizi wilaya zote zilizotajwa hapa Makete,Ludewa na Njombe mi kwa kweli naunga mkono suala hili.Ni bora wilaya hizi zipewe hadhi ya kuwa mkoa ili kupeleka kasi maendeleo ya maeneo haya.
Mkuu Gender Sensitive naomba unieleweshe unaongezaje maendeleo kwa kufanya say Njoluma kuwa mkoa, to me naona kulikuwa na watendaji kama kawaida kama wakuu wa wilaya, watendaji wa wilaya n.k ambao tunategemea watafanya kazi na kustir development. Kwa sasa utakuwa na mkuu wa mkoa pale Njombe na bado utakuwa na mkuu wa wilaya katika wilaya zinazounda mkoa, ulichofanya ni kuongeza ofisi ya mkuu wa mkoa ambayo itaongeza zaidi matumizi na kutupa return ndogo sana. Please nieleweshe, maendeleo yanakuja vipi hapo.
 
Haya majina hata hayapendezi, kwa mara ya kwanza tunakuwa na jina/majina ya mikoa abbreviated! walishindwa kukubaliana jina moja zuri (relative term though) lenye maana kama ilivyo manyara? huenda hata majina ya wilaya ni vifupi vya kata zinazounda.

Mkuu, ulitaka ama unapendekeza yapewe majina gani ili yapendeze? Lakini angalia kwenye fikra zako isije kukawa na kasumba kuwa majina yenye asili ya ulaya, marekani, uarabuni, bara Hindi na uchina ndiyo bora kuliko yenye asili ya lugha na lahaja zetu!

Kuhusu majina ya wilaya hizo kutokana na kata,nikitumia tafsida, nitasema si kweli. Nikikujibu kavu kavu ni takwambia ni mwongo. Majina hayo yana historia ndefu sana. Nalipenda jina SIMIU zuri kulitamka tamu kulifikiri, jina la lenye vtamkawa vya kibantu haswa.

Ilifikiriwa mwanzoni kuitwa mkoa wa Njombe, kwa kuwa wilaya za Ludewa na Makete zilitoka ndani ya Njombe district ya mjerumani na muingereza. Tetesi zinasema wakaona ni kama kurudia kuvitukuza vya mkoloni.

Wakapandekeza NJOLUMA ikiwa ni jina lilioanza wakati wa uanzishaji wa vyama ushirika. Wakati huo ushirika wao uliitwa Njombe-Ludewa-Makete Co-opereative Union (NJOLUMACU.). Toka hapo hata kwenye vikao vya kimkoa vya kiserikali na kimichezo wilaya hizo zilitajwa kama wilya za NJOLUMA.
 
Kigezo kikubwa walicho tumia eti kusogeza maendeleo kwa wananchi kwa haraka vimkoa vidogo vyenyewe wameshindwa kuvipelekea maendeleo ya haraka mpaka kesho vinashika mkia kimaendeleo wananchi wenyewe wanaishi kwa matumaini huduma za muhimu kama maji,shule, dispensary ni za kubabaisha tu nenda huko Lindi na Mtwara kisha safiri Kigoma yaani watawala wetu wanachekesha naona nyuma ya pazia ni kujiongezea ulaji kwa watu frani frani.

Mkuu Fidel80, nakwambia Tanzania si kubwa kama tunavyofikiri ukiimarisha miundombinu ya barabara, reli, usafiri wa maji na anga vikiwa Katika ubora unaokubalika. vikichagizwa na mawasiliano ya kiteknohama.

Nakumbuka miaka ya themanini gari likitoka Tukuyu kwenda asubuhi hurudi jioni. Tripu moja kwa siku. palikuwa na gari moja linaitwa KARANJA, gari hili lilikuwa linapiga tripu mbili, TUKUYU-MBEYA, lilisifiwa na kuonekana linakimbia mno. Leo gari hufanya hata tripu sita na barabara ni lami safi mno.

Nimekumbuka tena..... sijui kama unazikumbuka zile zama za simu za kunyonga....baada kuomba kumpigia mtu kwa ridhaa ya operator wa Shirika la Posta na Simu Tanzania.
Lol kuna mengi!!!!!!
 
Wilaya mpya zilizoanzishwa mpaka leo zingine hazieleweki kama ni wilaya sasa sijui hiyo mikoa itakuwaje, mie nadhani ni bora mikoa iliyopo iboreshwe kwanza na si baraka ya kuongeza mikoa tu wakati hata hiyo iliyopo mingine bado ni duni.sijui wa JF mnalionaje hilo swala.
 
Mwanakijiji Mkoa wa Iringa ni Mkubwa sana na hata geographical location zake kati ya Wilaya na Wilaya imekaa vibaya sana.I have been kwenye hizi wilaya zote zilizotajwa hapa Makete,Ludewa na Njombe mi kwa kweli naunga mkono suala hili.Ni bora wilaya hizi zipewe hadhi ya kuwa mkoa ili kupeleka kasi maendeleo ya maeneo haya.

GS, haya yote ni sawa. Mimi najiuliza hizi gharama za kuendesha hii serikali nani atabeba? Juzi tu hapa tumepata data kuwa serikali inakusanya kodi toka kwa wastani wa watu milioni mbili. Bajeti 2010/2011 ndo tumeisikia hivyo, hakuna creativity ya kupanua wigo wa kodi. In real sense serikali inajiongezea expenses wakati mapato yako constant!!

Ukisoma data za Dr. Slaa kwenye hotuba yake kuchangia bajeti, utangundua zile figure walizoleta kwenye bajeti hii zimepaishwa na mfumuko wa bei tu, lakini hakuna ongezeko lolote kwenye mapato!!!

Halafu leo tunasema maendeleo yatawafikia watu wetu kwa kuongeza mikoa!!! Kweli?
Hawa watawala sijui vichwa vyao kama viko sawa!!
 
Kwa mujibu wa wanasiasa wetu kuanzisha mkoa ni kama bilioni 10 hivi (nisahihisheni kama nimeoverlook) na bad kila mwaka itahitaji bajeni wa ajili ya uendeshaji. Mi nadhani ni kuongeza mzigo kwa serikali. Hii hii miko iliyopo iboreshwe, hebu cukulia mfano wa Manyara, ni ,maka 8 sasa tangu uanzishwe lakini bado mambo mengi hayajakamilika, kisa ukosefu wa fedha,sikubaliani a hili wazo kabisa
 
Wakuu, me naona kama tatizo ni la kiutawala hilo lipo kulingana na population iliyopo na sio area coverage. Na kama ni hivyo bora wakubali wazo la CHADEMA la sera ya majimbo litafaa!
 
• Shinyanga, Mwanza zamegwa vipande

na Martin Malera, Dodoma


amka2.gif
RAIS JAKAYA Kikwete amegawa mikoa mipya, wilaya na tarafa kwa maelezo kuwa ni mbinu ya kurahisisha shughuli za kiutawala na kuleta maendeleo.

Hatua hiyo ambayo ni dhahiri itaongeza ukubwa wa serikali, ilitangazwa jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Kuu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Njeruma uliomeguka kutoka mkoa wa Iringa, ambao unaundwa na wilaya za Njombe na Ludewa.
Kwa mujibu wa Pinda, mkoa mwingine mpya ni Geita uliomeguka kutoka mkoani Mwanza huku mkoa wa tatu ni Simiyu, uliomegwa kutoka mkoani Shinyanga.
Mkoa mwingine mpya ambao bado uko kwenye mchakato wa mwisho kabla ya kutangazwa ni Mpanda.
Kwa maana hiyo, sasa Tanzania itakuwa na mikoa 30, kutoka ya zamani 26.
Mbali ya mikoa hiyo, Waziri Mkuu Pinda alizitaja wilaya mpya kuwa ni Mulele na majina ya mikoa kwenye mabano kuwa ni (Rukwa), Gairo (Morogoro), Kalambo na Kwela (Rukwa).
Wilaya nyingine mpya ni Nyasa (Ruvuma), Kaliuwa (Tabora), Chemba, Ikungi (Singida), Wanging’ombe (Mbeya), Mbongwe, Uvinza (Kigoma), Nyang’wale (Mwanza), Kakonko, Mkalama, Buhingwe na Ushetu.
Mbali ya tarafa, serikali pia imepandisha hadhi baadhi ya wilaya kufikia kiwango cha Halmashauri. Wilaya hizo ni Handeni, Lindi, Masasi na Ilemela.
Baadhi ya tarafa mpya zilizotajwa jana ni pamoja Tunduma, Izenje, Kifura, Ruaha, Ngoheranga, Mpwayungu na Bukombe.
Akijibu hoja za wabunge mbalimbali, Waziri Mkuu ambaye bajeti ya ofisi yake ilipitishwa jana, alisema Serikali ya Awamu ya Nne imefanya kazi kubwa kwa kuhakikisha inatimiza Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005.
Kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi, alisema kuwa serikali imewafikisha watuhumiwa 13 waliotuhumiwa kukwapua sh bilioni 133, kutoka Akaunti ya Fedha za Nje, mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na bado inaendelea na uchunguzi ili wote waliohusika wafikishwe mahakamani.
Kama ilivyokuwa kwenye hotuba yake ya bajeti, Waziri Pinda alisisitiza kuwa serikali imepania kudhibiti matumizi mabaya ambapo kuanzia sasa safari za ndani na nje ya nchi, zitahitaji kibali chake hasa kwa safari muhimu tu. “Wakuu wa mikoa na wilaya, acheni woga kuhoji matumizi ya Halmashauri, hakuna sababu ya kuogopa. Mnamwogopa nani?” alihoji.


SOURCE :TANZANIA DAIMA
 
Hivi Mkoloni (watu wachache) waliweza vipi kuongoza mikoa 16 na wakapeleka maendeleo mikoani kuliko serikali chini ya Mtawala mweusi?..
Je, kwa tamko la Ras na waziri mkuu, haionyeshi uwezo mdogo wa mtu mweusi kuongoza eneo kubwa pasipo kuongeza ukubwa wa serikali!
 
Naomba kuuliza, fedha za kuongeza mikoa zinatoka wapi?

Naomba kuuliza, tunapodai mikoa ni mikubwa sana kiutawala je ina maana hatuna watu wenye uwezo wa kuongoza na kuleta ufanisi mpaka tuanze kupunguza ukubwa? Kama ni hivyo kwa nini tusipunguze basi ukubwa wa nchi kwa kuwa imetushinda kutawala?
 
Naomba kuuliza, fedha za kuongeza mikoa zinatoka wapi?

Naomba kuuliza, tunapodai mikoa ni mikubwa sana kiutawala je ina maana hatuna watu wenye uwezo wa kuongoza na kuleta ufanisi mpaka tuanze kupunguza ukubwa? Kama ni hivyo kwa nini tusipunguze basi ukubwa wa nchi kwa kuwa imetushinda kutawala?

Rev. Kishoka hakuna anayefanya kazi Tanzania watu wote wamegoma viongozi hawataki kuelewa ndio maana wanaona nchi kubwa. Wasomi sasa hivi ni wengi kwenye kila fani, mioundombinu iko bora magari ya kifahari, ndege kila mkoa, simu sio za kukoroga, mobile mpaka kijijini. wakuu wana laptop, palmtop, fingertop, desktop whatever, amabazo hazitumii anayway, lakini hawafanyi kazi.

Hakuna morale ya kazi, na mtu aliamka asubuhi anaenda kazini msimamishe muulize anaenda kufanya nini wtaokukujibu sahihi kati ya kumi ni watatu tu.

Mkuu wa mkoa anafunga ofisi tatu za ardhi Mkoa wa Dar Es Salaam kwa ajili ya Rushwa wakati watu wana time table zao, fikiria mtu anataka mkopo kwa ajili ya MKUKUTA au muwekazaji amepanda ndege kuja Dar kufuatia mkutano wa diaspora ( whatever it means) anafika dar anambiwa ofisi Zote za ardhi zimefungwa for two weeks . Kisa Rushwa sounds funny. Hicho ( Rushwa) kimekuwa kilio cha watu wote miaka nenda rudi no one acts, uchaguzi umekaribia kila mtu anajifanya yuko karibu na wapiga kura. Wanakumbuka shuka asubuhi.
 
Katika hotuba ya Desemba 30 Bungeni Dodoma (nakala ya Kiingereza: SPEECH BY THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, ON INAUGURATING THE FOURTH PHASE PARLIAMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, PARLIAMENT BUILDINGS, DODOMA, 30 DECEMBER 2005), JK hakutangaza kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka.

Toka hapo bajeti ya kila mwaka haikutangazwa kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka!

Sasa haya yametoka wapi?


 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom