Mikoa inayoongoza kwa umaskini Tz !

Mikoa yote ina umaskini. Maendeleo yako mijini tu. Ukienda ndani vijiji vyote, mikoa yote kuna umaskini wa kutupwa!! Ni aibu kwa Tanzania nchi ambayo imesherehekea miaka hamsini lakini bado maskini sana.
 
Bahati nzuri nimetembelea na kuishi takribani mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani na wilaya zake isipokuwa mafia kisiwani ukerewe,nkasi na ngorongoro Namshukuru Mungu sio Tanzania tu afrika ya mashariki na eneo kubwa la maziwa makuu nalijuwa vizuri. Naweza kuwa naijuwa Tanzania kuliko hata JK ,Prof. Lipumba na Dr. Slaa Orodha yangu ya Top 5 utajiri maendeleo na miundo mbinu
1. MWANZA(samaki,Dhahabu,Almasi,Pamba na Mifugo)
2.ARUSHA(Utalii,Tanzanite,Kikombe nitamalizia
 
Bahati nzuri nimetembelea na kuishi takribani mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani na wilaya zake isipokuwa mafia kisiwani ukerewe,nkasi na ngorongoro Namshukuru Mungu sio Tanzania tu afrika ya mashariki na eneo kubwa la maziwa makuu nalijuwa vizuri. Naweza kuwa naijuwa Tanzania kuliko hata JK ,Prof. Lipumba na Dr. Slaa Orodha yangu ya Top 5 utajiri maendeleo na miundo mbinu
1. MWANZA(samaki,Dhahabu,Almasi,Pamba na Mifugo)
2.ARUSHA(Utalii,Tanzanite,Kikombe nitamalizia
Nakusubiri...
 
Mbona jazba zinatufanya tupoteze logic ya mjadala

kuna mikoa ina umaskini sana,mfano Singida,sehemu kubwa ni tambarare na ni kame kitu kinachofanya watu wawe maskini wa kipato na njaa isiyoisha,na umaskini wa njaa ni umaskini mbaya sana na madhara yake ni makubwa,magonjwa,elimu duni, kuombaomba,vifo n.k

aliyesema Kagera ni miongoni,siyo kweli na kama ni rank basi kagera iko kwenye 10 bora,kwa nini?watu wengi wanaweza kusoma/kuandika,ardhi kubwa ni arable na inatumika,barabara kubwa mpaka wilayani zote zina lami sodata,umeme umesambaa sana mpaka vijijini,mazao ya biashara ama ndizi,kahawa,samaki ama miwa,n.k.kwa hili kidogo tuwe wakweli
 
Hivi ni nani anawaambia mtwara ni maskini??yaani mawazo yenu ya 70's bado mnayo hadi leo??hembu tembeleeni huko South halafu mje hapa jamvini mfute kauli zenu!! Huu ndio mkoa ambao hata usikie Tanzania nzima ipo gizani/sijui mgao wa umeme,huu utakuwa pekeyake unashine kwa umeme,Na Gesi ikiianza kuchimbwa kule ndio non-stop!!

Itachimbwa lini? Tembelea Mangaka, mikangaula, lukuledi, chikundi,chiungutwa! Mimi nilitoka huko miaka ya 1994 kabla Mkapa hajawa rais ila niliyoyaona huko Mtwara nilishtuka, nafikiri watu wa huko wakienda jehanam hawatapata sana shida maana wana uzoefu tayari. Nilitambua hakika binadamu hatuko sawa, sijui walioko huko sasa hivi je kuna mabadiliko? Sikutamani hata kurudi. Pia mikoa waliokaa sana waarabu ina umaskini wa kutisha mf. Kigoma, Tabora,na mikoa ya Pwani. Uswahili mwingi na uvivu
 
Vipimo vya umasikini vimo kwenye MKUKUTA - Mkakati wa Kuongeza Uchumi na Kuondoa Umasikini Tanzania. Vile vile kuna ripoti zinaitwa Human Development Reports ambazo huwa zinatolewa kila baada ya kipindi fulani na Taasisi ya REPOA (Research on Poverty Alleviation). Ndani ya ripoti hizo kuna vigezo vingi ambavyo hutumika kupima viwango vya umasikini kwa mikoa kwa kutumia nadharia ya MKUKUTA.

kwa hivyo nendeni kwenye hizo ripoti ili muweze kupima hasa ni wilaya gani ambazo ndiyo masikini kabisa.
 
Mara ya mwisho umefika lini Dodoma? Dodoma hadi Iringa ni mwendo wa saa mbili hadi tatu na ni lami tupu. Barabara ya Dodoma hadi Arusha kupitia Kondoa inakaribia kumalizika. Karibu Dodoma Makao Makuu ya Nchi
Dodoma inaongoza!hakuna barabara nzuri zaidi ya Morogoro road na Singida road,zote zilizobaki si za kuunganisha Mitaa,Kata,Wilaya wala Mikoa jirani zinazopitika kwa urahisi hata kipindi cha KIANGAZI!
 
Taarifa ya maendeleo ya watu ya mwaka 2015/2016 iliyosomwa bungeni june mwaka jana ilionyesha mikoa 5 maskini zaidi Tanzania Kigoma, Kagera,Geita, Singida na Mwanza.
 
Back
Top Bottom