Mikakati ya kulinda mitandao na watumiaji vipi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Marekani pamoja na mabavu yake yote inayoionyesha kwa nchi mbali mbali
duniani haswa ambazo hazipendi maslahi yake , iliamua kutangaza wazi
nia yake ya kufanya mitandao yao ya mawasiliano kuwa kitu muhimu sana
kwa taifa lao kwa ajili ya maslahi yao ya sasa na huko mbeleni


Raisi wa nchi hiyo ameunda jopo maalumu katika ikulu yake itakayo
simamia masuala ya Mitandao na mawasiliano mengine yanayohusiana na
mitandao ,


Kwa sasa kila nchi na jamii inaweka mikakati shirikishi na endelevu
kwa ajili ya ukuaji wa mitandao au au njia za mawasiliano ,
kuziboresha zaidi na kuzifanya ziwe salama zaidi kwa ajili ya maslahi
ya nchi hiyo au jamii hizo


…………………………………………………………………………….


Ukitembelea nchi kama Nigeria yenye wananchi zaidi ya milioni 130
wengi wao ni vijana walioenda shule kidogo , serikali ya nchi hiyo
pamoja na wananchi kwa ujumla wamechukuwa jukumu moja nalo ni kujenga
naigeria mpya ya wakati ujao mwaka huu walikuwa na mkutano ulipachikwa
jina la REBRAND NIGERIA wanasafisha nchi yao kutokana na yale mabaya
yote ambayo wananchi ya nchi hiyo walikuwa wakifanya nje ya nchi
pamoja na ndani ya nchi yao .


Kwa kuanza na hatua hiyo Kulikuwa na Hiyo REBRAND NIGERIA na wiki
chache zilizopita Raisi wa Nchi hiyo ameingia katika vita kubwa ya
kuhakikisha mitandao ya nchi hiyo iko salama , wananchi wa nchi hiyo
wanadhibitiwa dhidi ya vitendo vingi vya kihalifu wanavyovifanya dhidi
ya nchi zingine au ndani ya nchi yao ya Nigeria .


Mfano kuna banki kadhaa ambazo zimeajiri watu maalumu kwa ajili ya
kufuatilia matendo na taarifa za baadhi ya wateja wao haswa katika
masuala ya pesa wanapochukuwa , kuingiza , au kuingizia wengine
pamoja na mawasiliano yao mengine ambayo yataweza kuwasaidia katika
kufanikisha kudhibiti uhalifu


Kuna baadhi ya maeneo nchi humo ambapo mashine za ATM za kutolea pesa
mfano zimepigwa marufuku kabisa kufungwa baadhi ya maeneo pia
hawaruhusu hata biashara za benki kuwepo kutokana na kukithiri kwa
vitendo vya uhalifu kwa njia ya mitandao .


……………………………………..


Nchini Malaysia napo nchi hiyo imewekeza sana katika kuhakikisha
mitandao yake inakuwa salama kama nchi zingine katika idara mbali
mbali za kipolisi wanavitengo vyao maalumu ambavyo kazi yake ni
kufuatilia mawasiliano ya mitandao toka Malaysia kwenda kwingine na
yanapoingia pamoja na kufuatilia habari zingine zinazohusu mambo yao
ya ndani .


Ukitembelea vitengo hivi vya kipolisi utaweza kuonyeshwa maoneo hatari
ambayo wanayafuatilia kwa ukaribu tukio kama la kusambaa virus kwa
njia ya mtandao likianza basi katika computer zao ubaoni utaona kabisa
jinsi wanavyosambaa na jinsi wanavyoweza kuwapa taarifa watu na
vitengo mbali mbali vya nchi hiyo .
…………………………………………………………


Siku chache zilizopita kumezuka wimbi kubwa la watu kutoka nje ya nchi
kuingia nchini mwetu kuuza bidhaa zinazohusiana na mawasiliano au
programu za aina mbali mbali .


Bahati mbaya kuna watu kutoka benki kadhaa wamedhubutu kununua bidhaa
hizi wengine wa idara nyeti za serikali ambazo zinatakiwa zihudumiwe
bidhaa hizo au vitu hivyo na watu wao wanaohusiana na ICT na sio mtu
wowote tu .


Sijasema kama ni ubaya kununua kitu , lakini tuangalie sisi kama nchi
sasa tuko katika hatua gani na usalama wetu ukoje , kuna watu
waliniandikia ujumbe kuniambia kwamba hao ni wajirani zako waache
tupanue biashara katika jumuiya ya afrika ya mashariki .


Hata hivyo walishindwa kujua mfano sisi na Kenya ni washindani wa
kibiashara katika eneo hili la afrika ya mashariki , kama hiyo ni sawa
basi wao watakuwa na interest zaidi na Tanzania katika kuhakikisha
wanapata taarifa zaidi kwetu au kutoka kwa watu wetu ili iwe rahisi
wao kuzitumia katka ushindani na kwa shuguli zingine ambazo zitakuwa
na faida kwa nchi yao .


Hapa nchini kwetu pia tumeona vikao na makongamano mengi yakifanyika
kuhusu masuala haya haya ya usalama wa mitandao na vitu vingine vya
mawasiliano toka mwaka jana mikutano na midahalo hii imekuwa mingi
sana .


Mwaka huu pia Bwana Ali Mafuruki kwa kutumia kampuni yake pamoja na
washirika wake alifanya mkutano na waandishi wa habari kushirikiana na
Jeshi la polisi walitoa msaada wa Mil karibu 10 kwa jeshi la polisi
kwa ajili ya mafunzo ya kulinda mitandao hii


Kwahiyo hayo mafunzo wanayoyapata wakirudi watumie vifaa gani ?
inawezekana ni bwana Ali mafuruki pamoja na hao washirika wake ndio
watauza vifaa hivyo na mitambo hiyo ya mawasiliano kwa jeshi la polisi
ili kuweza kupambana na uhalifu huu


Sipingi hatua hiyo lakini kitu alichofanya mafuruki ni kwa maslahi
yake ya kibiashara na watu wake huu ni utongozaji wa dhahiri kabisa
ili wapate tenda hiyo ya kuuzia jeshi letu vifaa hivyo na mitambo hiyo
kwa dhamani ambayo itakuwa ni faida kwao ukilinganisha na msaada huo
walioutoa kwa mafunzo


Jambo jingine ni kwamba kwa sasa nchini kwetu mchakato wa kuwa na
sheria za mitandao ndio uko mbioni kwahiyo sheria hizo zikiwepo ndio
serikali inaweza kutangaza tenda ya watu au kampuni zinazoweza kuleta
vifaa vinavyoweza kutumika katika kupambana na uhalifu mbali mbali wa
mitandao kama sheria hakuna hata hiyo misaada haina maana sana hata
hayo mafunzo .


Pia kuna kampuni iliwahi kuliuzia jeshi la polisi aina ya Antivirus
ambazo zilishindwa kuwa activated licence zake inaonyesha
zilishatumika , sasa sijui kama kampuni hiyo inahusika na uuzaji wa
antivirus hizo ambazo zilishindwa kuactivate na kufanya kazi
inayotakiwa kufanyika .


Hayo ni machache tu wadau tuna mengi na mazito kabisa ya kujadili na
kuandika na sio kukaa katika vikao morogoro , mwanza na nje ya nchi
bila kuwa na mikakati endelevu ya kuhakikisha Taifa hili linaweza
kujilinda na kuwalinda raia wake dhidi ya mitandao na uhalifu mwingine
unaohusiana na mitandao hii


Katika mikutano hii ni watu wachache wanakutana wenyewe huko mara
nyingi haitangazwi ili kila mdau aweze kushiriki na kutoa mada au
kuuliza maswali yake , naamini nchini mwetu kuna vijana wengi sana
wenye kuelewa masuala haya waliosoma hapa hapa nchini na wengine nje
ya nchi lakini wanafanya kazi nchini ambao kwa namna moja au nyingine
wanaweza kushiriki katika kupeleka suala hili mbele zaidi .


Ni wakati sasa umefika kwa mikutano hii , midahalo hii na mikakati hii
inayohusu masuala ya mawasiliano au kuwasiliana iwekwe wazi ili kila
mtu aweze kushiriki aweze kuleta mapinduzi katika jamii yake , kila
mtu aweza kuja na njia na mbinu za kuboresha kitu hichi sasa na huko
mbeleni .


………………………………………………………………………..


Kuna changamoto Fulani napenda kutoa zinazohusiana na mawasiliano haya
haya .


1- pamoja na Tanzania kuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa simu za
mikononi watu wanashindwa kuwa na vyama ambavyo vinaweza kutumika
dhidi ya watoa huduma hizi za simu mfano upandishaji wa gharama za
simu uliofanyika hivi sasa hakuna mtu aliyetolea tamko suala hili kila
mtu kimya
2- ukija kwenye masuala ya benki sasa hivi kuna wizi wa ATM hakuna
vyama vinavyohusiana na benki hizi au wadau wa benki kutolea tamko
suala hili hata benki zenyewe zinafanya hii ni siri yao wenyewe wakati
wanaoumia ni wananchi wanaoweka pesa zao mule .
3- hili suala la watu kuchafuana kwenye mitandao na sehemu zingine nao
hakuna vyama vinavyoweza kukaa pamoja na wamiliki wa mitandao hii au
wamiliki hawana vyama vinavyoweza kuwakutanisha kutoa matamko na
kutafuta suluhu kati yao .


NAKUTAKIA JUMAPILI NJEMA
 
Back
Top Bottom