Mikakati urais CCM 2015 yashika kasi

Kama CCM watamteua Lowassa agombee urais 2015 na wananchi wakamchagua kuwa rais, ni bora Mungu ashushe ghalika kuiangamiza Tanzania.
 
Hakuna anayesubiri 2015 hii mifisadi ya CCM lazima iondoke mapema kabla ya 2015. JK anasema haijui Dowans lakini anasema walipwe kwa njia yoyote ile huu ni umburu kenge.
 
OMG...PLEASE DON'T MOVE IT IS NOT APRIL FOOL JOKE;





*Mwenyekiti Wazazi asukiwa mkakati kuondolewa, Msekwa aongea
*Kikao cha sekretarieti chakaa Sinza kupanga mikakati wake
*Mawaziri tisa kwenye mbio za urais wasahau majukumu yao


Makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa


MAKUNDI ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yanayojiandaa na urais wa 2015, yameanza kuzivuruga jumuiya za chama hicho kwa kupanga mikakati ya kuwang’oa viongozi wanaohisiwa kuwa nje ya mitandao yao, Rai limebaini.

Rai pia imebaini kuwa jumla ya mawaziri tisa, wamekuwa wakizunguka katika ziara nchi nzima, kupanga mbinu za kupata wapambe zaidi ndani ya chama hicho, watakaowatumia katika harakati kuwania nafasi hiyo wakati utakapowadia.
Jumuiya za CCM ambazo zinaonekana kuathirika zaidi na makundi hayo, ni ya Wazazi na Umoja wa Vijana (UVCCM). Rai limefahamishwa kwamba upo mkakati wa dhahiri wa kumng’oa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Balozi Athuman Mhina, huku UVCCM ambayo imepwaya baada ya mzozo wa ndani kwa ndani ulioanza mwanzoni mwa mwaka jana, nayo ikiwaniwa na wasaka urais hao.

Balozi Mhina amekiri kuufahamu mkakati huo katika mazungumzo na Rai Jumanne wiki hii, lakini akashindwa kuingia kwa undani kuelezea mpango huo na sababu zake, kutokana na kile alichosema mahali alipokuwa wakati akizungumza na Rai hapampi fursa ya kulizungumzia jambo hilo.

“Natambua kufanyika kwa kikao hicho cha kuning’oa mimi kilichofanyika Sinza, lakini hapa nilipo kuna watu wengi siwezi kukueleza hali halisi ya ukweli ulivyo, nikipata nafasi nzuri nitakupigia,” alisema Balozi Mhina juzi Jumanne kwa njia ya simu, akisema wakati huo alikuwa Goba, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari hizo, lipo kundi moja la wanamtandao wa kuelekea 2015, ambao wanaona kuwapo kwa Mhina ndani ya Wazazi kunaweza kukawa kikwazo kwa kundi hilo katika harakati zake za kuusaka urais mwaka 2015.

Uongozi wa juu wa Jumuiya ya Wazazi, umegawanywa na makundi hayo kwa makatibu wakuu kuwa upande tofauti na wenyeviti wao. Hali hiyo, inaufanya uongozi katika jumuiya hizo uwe wa kuviziana na kuwindana, kila mmoja akiwa haziamini harakati za mwenzake.

Habari ambazo zimelifikia Rai wiki hii zinasema mwanzoni mwa mwezi huu, Katibu Mkuu wa Wazazi, Khamis Suleiman Dadi, aliitisha kikao cha watu wake wa karibu, kikao ambacho kinadaiwa kujichimbia maeneo ya Mugabe, Sinza, nyumbani kwa Naibu Katibu Mkuu Wazazi (Bara), Edward Ndonde.

Kikao hicho kilichopewa hadhi ya kikao cha Sekretarieti, kinadaiwa kuhudhuriwa na wakuu wa idara za jumuiya hiyo pasipo kumshirikisha wala kumtaarifu Mwenyekiti, Balozi Mhina wala mjumbe yeyote wa Kamati ya Utekelezaji.

Kwa mujibu wa habari hizo, wengine wanaodaiwa kuhudhuria kikao hicho na idara zao katika mabano, ni pamoja na Ndonde mwenyewe, Zacharia Katale (Utumishi), Bernad Lusale (Uchumi), Lengenie Kamnde (Mhasibu Mkuu) na Ali Timamu (Oganaizesheni).

Habari za awali zilisema kikao hicho kilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti (Bara), Pius Msekwa, na Abdallah Bulembo ambaye aligombea na Balozi Mhina katika uchaguzi uliopita wa Wazazi na kushindwa.

Hata hivyo, Msekwa alikanusha vikali kuhudhuria kikao hicho, akisema hatambui chochote bali kama kweli wanataka ushauri basi wamfuate ofisini kwake atawapa ushauri wa kikatiba.

“Kwanza suala la kuwapo mgawanyiko ndani ya Jumuiya ya Wazazi, hilo silifahamu ndiyo kwanza nalisikia kwako. Pili, sijaitwa wala sikuhudhuria kabisa kikao hicho cha Sinza kwa lengo la kutoa ushauri. Lakini kama wanataka kupata ushauri wangu wa jinsi ya kufanikisha kumng’oa Mwenyekiti wao waje tu ofisini nitawapa ushauri wa kikatiba,” alisema Msekwa juzi Jumanne kupitia simu yake ya mkononi.
Juhudi za kumpata Bulembo na wakuu wengine hao wa idara hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitambuni juzi Jumanne. Lakini wadadisi wa mambo ndani ya jumuiya hiyo, wanahoji ni kwanini kikao cha kazi cha wajumbe sita kifanyike nyumbani kwa mtu wakati vikao kama hivyo huwa mara zote vinafanyika makao makuu ya jumuiya.
Habari zinasema katika mkakati wa kundi hilo la Wazazi linaloongozwa na Katibu Mkuu, baada ya kujadiliana katika kikao hicho cha siri na kubaini kwamba hawana uwezo wa kumng’oa Mwenyekiti wao, waliamua kuondoka na mkakati wa kutafuta uwezekano wa kuifuta Kamati ya Utekelezaji.

Rai lilizungumza na mjumbe mmoja wa Kamati ya Utekelezaji, Stella Manyanya, ili kupata undani wa mvurugano huo ndani ya Jumuiya hiyo, ambaye alisema Sekretarieti ya Wazazi haina uwezo wa kuifuta Kamati ya Utekelezaji wala kumng’oa Mwenyekiti wao.

Akizungumza juzi Jumanne kupitia simu yake ya mkononi, Manyanya alisema Wazazi kama moja ya Jumuiya muhimu za CCM, kamwe hawatakubali jumuiya yao iwekwe mfukoni mwa mtu mmoja kwa maslahi yake.

Alisema anachojua yeye Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi, siku zote imekuwa ikitenda mambo kwa maslahi ya chama, na kwamba wajumbe na viongozi wao ni wamoja katika kuhakikisha kwamba CCM inaendelea kutawala nchi hii hata baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Aidha, alisema hadi sasa Kamati ya Utekelezaji imeweza, kwa kutumia juhudi zake, kufanikisha ukusanyaji wa fedha za kugharamia mkutano wa Baraza Kuu unaotarajiwa kufanyika baada ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ambavyo vinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya Wazazi, ndani ya UVCCM kunadaiwa kuwapo udhaifu wa kiutendaji wa jumuiya uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na mizozo ya ndani kwa ndani iliyojitokeza baada ya kung’olewa kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yusuf Masauni kwa madai ya kudanganya umri wake.

Mizozo hiyo ndiyo iliyosababisha jumuiya hiyo kuishiwa nguvu na kusababisha ishindwe kutekeleza wajibu wake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana wa kuwatetea wagombea wa chama hicho mbele ya wapigakura vijana.
Ombwe la kukosekana kwa UVCCM kwenye uchaguzi huo, lilionekana wazi baada ya kuanzishwa kwa kundi lililokuwa likijiita ‘Vijana Zaidi’ lililokuwa chini ya Miraji Kikwete, mmoja wa watoto wa Rais Jakaya Kikwete.

Miraji aliwahi kukaririwa na jarida la Bang, akisema kazi kubwa ya kundi hilo ni kuunganisha matarajio ya vijana kwa Serikali pamoja na kuwashawishi vijana wengi kwa kdri iwezekanavyo kuwapigia kura wagombea wa CCM.
Kutokana na kukosekana kwa nguvu ndani ya UVCCM, makundi ya mitandao ya urais wa 2015 ndani ya chama hicho, yamekuwa yakipenyeza kucha zao ndani yake na kusababisha jumuiya iyumbe kisera na kiutendaji.

Lakini kubwa zaidi katika harakati hizo ni kwa baadhi ya mawaziri wanaofanya ziara za kiserikali katika mikoa mbalimbali, hasa Tanzania bara, kutumia fursa hiyo kuitisha vikao vya wana CCM usiku kupanga safu za kampeni za 2015, badala ya kutuliza akili zao kwa ajili ya kukabiliana na changamoto nzito zinazoikabili Serikali.
Rai imebaini jumla ya mawaziri tisa ambao wamekuwa wakizunguka mikoani kwa ziara za kiserikali, lakini wakati huo huo, wakiitisha vikao vya usiku na viongozi pamona na wanachama maarufu wa CCM mikoani, kupanga safu za kujiandaa na uchaguzi wa 2015 ndani ya chama hicho.

Bado haijaweza kujulikana mara moja iwapo suala hilo la kampeni za 2015 litajadiliwa kama moja ya tatizo ndani ya chama na vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) vinavyotarajiwa kuketi wakati wowote mwezi huu kutathmini hali ya kisiasa ndani ya chama.
Hadi sasa haijafahamika ni lini hasa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu vitafanyika, baada ya Msekwa kuliambia Rai wiki hii kwamba hadi sasa ratiba haijatolewa na kwa hiyo hata yeye hajui ni lini hasa vikao hivyo vitaanza.
 
baadhi ya watu wameanza kampeni na kusahau kujishughulisha na shughuli za kiuchumi, that's why hatuendelei maana tumekalia porojo na maneno tu.
 
Back
Top Bottom