Mikael P Aweda aanza kuivuruga CHADEMA

Naona mzee wassira amekupa msemo, wacha niwe kama gazeti la mwananchi!!!


teh teh teh! haya bwana, nimekopa maneno ya tyson, lakini huoni kweli gazeti la mwananchi walikuwa wamemchonganisha na wananchi kuwa anasinzia kumbe alikuwa anatafakari neno.
 
teh teh teh! haya bwana, nimekopa maneno ya tyson, lakini huoni kweli gazeti la mwananchi walikuwa wamemchonganisha na wananchi kuwa anasinzia kumbe alikuwa anatafakari neno.

Kama wabunge wote wangetafakari kwa style wa wassira hilo bunge lingefanyaje kazi zake?
 
Taarifa za uhakika kabisa toka chanzo cha kuaminika ndani ya uongozi wa chadema jimbo la ukonga zinasema kwamba Bw. Mikael P. Aweda ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa chadema jimbo la ubungo, amechukua fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti jimbo la ukonga.

Kwa mujibu wa katiba ya chadema bw Aweda atashikilia nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chadema jimbo la ubungo hadi mwaka 2014 hapo utakapofanyika tena uchaguzi mkuu ndani ya chama.

Katika hali ya kushangaza mwenyekiti huyu amechukua fomu za kuwania uenyekiti wa chadema jimbo la ukonga. Jimbo la ukonga linatarajia kufanya uchaguzi wake mnamo tarehe 31/07/2011 kufuatia kugawanywa na NEC(tume ya taifa ya uchaguzi) kwa jimbo hilo kulikofanyika mwaka jana na kuzaliwa kwa jimbo la segerea.

Bw Aweda alianza kuonekana akipita pita katika matawi mbalimbali ya jimbo la ukonga pasipo hata kumfahamisha aliyekuwa mwenyekiti wa jimbo la ukonga mzee Binagi, na alienda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kushiriki na kusimamia baadhi ya chaguzi za matawi ya chadema ndani ya jimbo la ukonga.

Kutokana na hali hiyo ya bw Aweda kujitosa kuwania uenyekiti wa jimbo la ukonga, amesababisha mtafaruku miongoni mwa viongozi na wanachama wa ukonga wakihoji kulikoni akimbie kutoka ubungo kuja ukonga?? Na kitu cha kushangaza amechukua fomu kugombea ukonga huku akiwa hajajiuzulu nafasi yake ya uenyekiti jimboni ubungo.

Hii ni dalili mbaya kwa kiongozi mkubwa kama yeye anayepaswa kuheshimu katiba ya chama pamoja na imani kubwa aliyopewa na wanachadema wa ubungo. Kama ameamua kuwasaliti wanaubungo basi hata wanaukonga hawatomuamini, kwakuwa ameonyesha dalili zote za kutoaminika na usaliti wa demokrasia.

Ushauri wangu kwa uongozi wa juu wa chadema, kuanzia uongozi wa mkoa wa dsm hadi uongozi wa taifa ni kumuangalia kwa makini mtu huyu asijekuwa ana agenda za siri dhidi ya chadema kwani wakati huu ambapo uongozi wa jimbo la ukonga wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda chaguzi zote zijazo, wamekuwa wakifungua matawi maeneo mbalimbali kuanzia kitunda, kivule, ukonga, pugu na chanika lakini sasa bw Aweda anaonekana kuwakatisha tamaa na kuleta mvurugano hadi kusababisha mzee binagi kutorejesha fomu za kugombea uenyekiti wa jimbo.

Kwa kuwa bw. Aweda ni mdau hapa JF namuomba ajitokeze hadharani kukanusha habari hii kama sio ya kweli, ama vinginevyo athibitishe kama anagombea nafasi hiyo na atoe ushahidi kwamba amejiuzulu nafasi yake ubungo ili asionekane ni mtu mwenye tamaa na ubinafsi.

Naomba kuwasilisha.
Wewe ni fitna mkubwa
 
Nimesikia, Mikael P Aweda alikuwa m/kiti wa Chadema Ubungo akiwa anaishi Ubungo Kisiwani, manisipaa ya kinondoni. Sasa amehamia manisipaa ya ILALA na nimesikia anajenga kitunda . Sasa kama anaishi ilala aendele kuwa kiongozi kinondoni? Binafsi sioni tatizo kwa kuwa ninamfahamu sana nitampigia simu nijue undani wa suala hili.

You are very correct.
 
Japo kuwa haya maelezo nimeyaweka kwenye thread nyingine naomba niyaweke tena hapa. Mods msiyafute haya maelezo yangu wakati thread ingalipo ili kubalance the story.

Mimi nimekuwa mwenyekiti wa Chadema ubungo na mkiti wa kwanza wa kikatiba Ubungo nikiwa mkazi wa Ubungo- Ubungo kisiwani. Ni mwanachama ni nayetumia muda na pesa zangu nyingi kuijenga Chadema kwa uwezo wangu wote.

Nilipoingia Ubungo baadhi ya viogozi waliokuwepo walikuwa wanakaimu nafasi zao ktk baadhi ya ngzi, nikamilisha chaguzi zote kutoka kata ya Manzese hadi Kibamba. Shahidi wa Yote haya Mbunge mwenyewe. Nilifanya naye kazi kwa karibu sana.
Kabla sijaja ubungo, ubungo kulikuwa na vurugu nyingi sana. Nilipochaguliwa kuwa Mkiti na baada ya waleta vurugu kutimuliwa na makao makuu. Ubungo tumekuwa moja hadi tukashinda chaguzi zote hizo za madiwani na ubunge chini ya Uongozi wangu.

MCHAKATO WA KUNG'ATUKA.
Nimewashirikisha wazee wa ubungo na secretariet ya jimbo chini ya Katibu wa Jimbo la Ubungo.
Baadaye nikakaa na viongozi wa kata zote. Wote wamenielewa.

Kuhusu kujiuzulu ubungo.
Mimi nimejiuzulu uenyekiti wa Ubungo 1/7/2011. Nakala nimempa katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na Katibu mkuu Taifa. Barua nilimwandikia katibu wa Jimbo la Ubungo.

Kwanini nimjizulu?
A) Nimehama kimakazi kutoka Ubungo, mtaa wa Kisiwani manisipaa ya Kinondoni hadi Manisipaa ya Ilala. Makazi yangu ya kudumu yatakuwa Kitunda. Sidhani kama ni busara nichome mafuta kutoka Ilala kwenda ubungo. It is a waste of Time and Money unnecessarily.
On the other hand, katiba ya Chadema inaniruhusu mimi kupima mwenyewe baada ya kuhama kimakazi-haisemi lazima nijiuzulu au lazima nibaki. Kwa hiyo, mimi nikaongea na wazee wa Jimbo la ubungo, wakanielewa.

B) Ubungo ni Imara kimtandao na kiungozi. Jimbo la ubungo lina Mbunge Mnyika na Madiwani wa kutosha (7) bila kutaja wabunge wawili ambao nao ni madiwani. Kamati ya utendaji Ubungo ina wajumbe kama Dr Kitila, Mbunge na Suzana Lymo. Si Busara kuacha jimbo la Ukonga ambako ndiko ninakotumia muda wangu mwingi na kuendelea kuja ubungo ambayo ni imara. Nimezunguka kata zote, za ukonga na nimegundua inahitajika uimarishaji. Baadhi ya viongozi waliopo (wakiwepo viongozi wa jimbo) wanakaimu nafasi zao. Busara ni mimi kuongeza nguvu ktk jimbo kama hilo.

C) Ubungo ina ruzuku ya zaidi ya Sh mil moja kwa Mwezi ( Ruzuku ya Chama na mchango wa Mbunge). Ukonga wana ruzuku ndogo sana – around laki mbili na kidogo. Kwa hiyo, Uongozi uliopo unaweza kujenga chama Ubungo wakishirikiana na madiwani na Mbunge bila mimi. Busara yangu ni kwamba sasa niende nikatumie uzoefu wangu wa kuongoza ubungo muda mrefu bila ruzuku ( kabla ya uchaguzi 2010) na kufanikiwa kushinda ktk jimbo ambalo sasa lina matatizo ya fedha kama tuliyokuwa nayo sisi kabla ya mwaka jana. Kwangu mimi huu ndio uamuzi wa Busara. Sitakiwi kung'ang'ania ubungo tena imara.

D) Viongozi na wanachama wa ukonga wameniomba nigombee ukonga,
Viongozi wengi na wanachama wa ukonga, baada ya kuona utendaji wangu walioniomba nigombee nafasi mojawapo ktk uchaguzi unaokuja hivi karibuni. Nikawakubalia. Hiyo nayo ni sababu mojawapo.

Mwisho;
Ni matumaini yangu kwamba yale mazuri tuliyoyafanya pamoja mimi na viongozi wenzangu watayaendeleza wenzangu wanaobaki.

ALUTA CONITINUA.

MIKAEL P AWEDA
 
Mimi ni niligombea uenyekiti wa Chadema na kuwa mkiti wa kwanza wa kikatiba Ubungo nikiwa mkazi wa Ubungo- Ubungo kisiwani. Ni namwanachama ninayetumia muda na pesa zangu nyingi kuijenga Chadema kwa uwezo wangu wote.
Nilipoingia Ubungo haikuwa na uongozi wa kikatiba katika baadhi ya maeneo,(walikuwepo wa kukaimu) nikasimamia chaguzi zote kutoka kata ya Manzese hadi Kibamba(Nimetumia muda na pesa) Shahidi wa yote haya Mbunge mwenyewe (Mnyika). Nilifanya naye kazi kwa karibu sana.
Mkuu najua hatuwezi kukurudishia muda wako, unaonaje ukipiga hesabu za gharama zako tukurudishie? Unaonekana utakuja kuleta kashfa huko mbele ya safari
 
cha msingi kama katiba inaruhusu sioni ubaya wake let the democracy takes its roots, kama watu hawamtaki he will be
voted out so there is nothing to fear. demokrasia ndio jawabu chama ni mali ya watu let the people decide for themselves.

Exactly.
 
Mkuu najua hatuwezi kukurudishia muda wako, unaonaje ukipiga hesabu za gharama zako tukurudishie? Unaonekana utakuja kuleta kashfa huko mbele ya safari

Chama chochote lazima kichangiwe na wanachama wote. Mimi nachangia kila mwaka ada ya uanachama and that is Consititutional. Pia tunatakiwa kuchangia na michango mingine ruzuku haitoshi kufanya kila kitu. Chama cha watu huchangiwa na wanachama wake. Ndo maana CCM huwa hawachangi, wanavuna tu. Mwisho wakajagundua kuwa chama kimeshanunuliwa na mafisadi and there is no way out. Sisi hatutaki fedha za mafisadi tunataka kila mwanachama achangie. Hivi ninachangisha watu kwa ajili ya ofisi ya kata ya kitunda. Mkuu naomba mchango wako.
 
Chama chochote lazima kichangiwe na wanachama wote. Mimi nachangia kila mwaka ada ya uanachama and that is Consititutional. Pia tunatakiwa kuchangia na michango mingine ruzuku haitoshi kufanya kila kitu. Chama cha watu huchangiwa na wanachama wake. Ndo maana CCM huwa hawachangi, wanavuna tu. Mwisho wakajagundua kuwa chama kimeshanunuliwa na mafisadi and there is no way out. Sisi hatutaki fedha za mafisadi tunataka kila mwanachama achangie. Hivi ninachangisha watu kwa ajili ya ofisi ya kata ya kitunda. Mkuu naomba mchango wako.
mkuu ni kweli, nakuunga mkono, chama ili iwe chama cha wanachama wote, lazima michango itoke kwa wanachama, siyo kwa mafisadi. Binafsi nimejitolea sana kujenga matawi ya chadema kwenye kata yangu yenye mitaa sita, pamoja na kuwa ni mwenyekiti wa kata, lakini pia nimewashawishi wanachama na wananchi wapenda mabadiliko kuichangia chama. Mkakati uliopo ni jinsi gani ya kuanzisha miradi ya maendeleo, ili mwisho wa siku tuachane na michango ya mifukoni. Mipango inaendelea vizuri.
 
Acheni siasa za kizamani, nilijiuzulu tarehe 1/07/ 2011. Katibu wa Chadema jimbo la ubungo na mkoa wa Kinondoni wana nakala zao.

waache siasa chafu. aliloongea AWEDA ni ukweli mtupu na mimi nakri kupokea nakala ya barua hiyo nikiwa kama katibu wa mkoa wa kinondoni na katibu wa makatibu kanda ya dar es salaam, sasa mtoa hoja nadhani siyo mwanasiasa wakisasa ni wale waliyozoea propaganda za kiccm ccm.
 
Siku nyingine uwe na uhakika na kile utakachokilea,acha uzushi na uchochezi.kwa nini umeshindwa kuwasiliana na muhusika kabla ujapost upupu wako?mwenyewe kajibu huoni kama ni unafki huo?na wewe ndio unaekivuruga chama?be smart next time.
 
ww mleta mada unahisi hicho ni kitu kikubwa sana kiasi kwamba CDM itayumba?haujakumbuka ni mambo mangapi makubwa sana yameonekana ni tatzo kwa chama na leo yametatuliwa?kama brain yako inabana kweli utawaza sana kuhusu ili lakini kama ubongo wako unaweza kujiongeza ukaweza kuthink appropriately basi hii ishu ni minor sana...easy guy!
 
Nimesikia, Mikael P Aweda alikuwa m/kiti wa Chadema Ubungo akiwa anaishi Ubungo Kisiwani, manisipaa ya kinondoni. Sasa amehamia manisipaa ya ILALA na nimesikia anajenga kitunda . Sasa kama anaishi ilala aendele kuwa kiongozi kinondoni? Binafsi sioni tatizo kwa kuwa ninamfahamu sana nitampigia simu nijue undani wa suala hili.
Mbona hii kitu haina shida, lete mada nyingine
 
Sure. Jimbo si mali ya mtu, ni ya wanachama wote.

Aweda acha kujifurahisha na kufurahisha forum,

Wewe si mwanasiasa makini kama unavyotaka kuwaaminisha watu.

Bado nakusanya taarifa zako jinsi unavyokiuka kanuni na taratibu za kuendesha chama jimboni ukonga, na zikishakamilika nitarudi hapa hapa kuwaeleza watanzania hususan wapenzi na wanachama wa chadema jinsi unavyoshindwa kujiheshimu.

Nina taarifa za wewe kuingilia shughuli za kiutendaji za kamati ya utendaji jimbo la ukonga kwa kushirikiana na katibu wa jimbo, hiyo fedha unayotamba kuitumia kujenga chama safari hii itatumika kukubomoa!
 
Mkuu najua hatuwezi kukurudishia muda wako, unaonaje ukipiga hesabu za gharama zako tukurudishie? Unaonekana utakuja kuleta kashfa huko mbele ya safari

Na chadema isipokuwa makini na huyu bwana kuna hatari ya kuvuruga mshikamano uliopo ukonga, anajisifia vijisenti alivyonavyo, tukimuacha aendelee hivi mbele ya safari anaweza kutudai ama kukifisadi chama ili kuzirudisha. Kama ulivyomshauri ni bora apige mahesabu tumrudishie mapema kuliko kumuacha atatuharibia mbele ya safari huyu.
 
Back
Top Bottom